Mfumo wa Uchumi wa Dunia (World Economic Order) unaopendelea nchi za Magharibi ndiyo chimbuko la matatizo yote haya nchini.

dndagula

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
1,488
1,482
Tukiacha ushabiki wa kisiasa na itikadi, Sasa ninaanza kufahamu kwa nini Mwalimu Nyerere, Mandela, Augustino Neto na wengine walipiga kelele kuhusu Mfumo wa uchumi Duniani kugandamiza nchi za Afrika na Dunia ya Tatu.

Lakini pia ninaanza kuona kwa nini Mwalimu alipigia chapuo sana South South commission kama njia mojawapo ya kujenga ushirikiano wa kujikomboa nchi zinazoendelea.

Hali iliyopo sasa ya utandawazi na kuondoka kwa vita baridi na nchi zisizofungamana na upande wowote imechochea sana mataifa makubwa kupata hamasa ya kuingilia uhuru wa kisiasa na kiuchumi wa nchi nyingine bila hofu au pingamizi.Hali hii ndiyo kinachotokea katika nchi za kiafrika.

Mbinu wanazotumia mataifa haya kwa sasa ni pamoja na

1. Kuchochea machafuko kwa njia ya maandamano ya kisiasa kwa kofia ya haki za kuandamana huku waijua athari zake.

2. Kutumia fedha" financing" kwa NGO, Vyama vya siasa, magazeti, mitandao na matumizi ya teknolojia ya habari kwa ujumla kuuza itikadi zao na kuchochea uasi.

3. Masharti ya misaada.

4. Kupenyeza watu wa kushirikiana nao kwenye jamii yetu na ikibidi kwenye vyombo vya serikali, Bunge, Serikali na maeneo wanayolenga kwenye vyombo vya ulinzi hususani matumizi ya teknolojia.

5. Kuingilia mfumo wa maisha, mitizamo na utamaduni na desturi zetu. Hususan kuwaghiribu vijana ili kufanya uasi.

6. Mikataba ya kimataifa "treaties" "conventions"ni nzuri kwa muonekano wa nje lakini ni nyavu za kukamatia nchi zetu na kutushikisha adabu kiustaarabu.

7. Uwekezaji wenye sura ya "win lose" wanaupenda sana ikitokea hivyo.

8. Kisingizio cha ugaidi au demokrasia au haki xa binadamu isiyokidhi viwango vyao na kwa tafsri yao nayo ni sababu ya kuingilia mambo ya ndani ya nchi.

Kwa ujumla mataifa makubwa yanatumia njia nyingi mno na "sophiscated"kulingana na mazingira ya nchi husika lakini kikubwa ni kuhakikisha wanatafuta njia ya kufaidi raslimali zetu mujabara.

Ukitaka uanze kugombana nao jaribu kuwabana tu kwa kulinda uchumi wako kwa"protectionalism" wanasahau kuwa hata wao wana sera za kulinda uchumi wao i.e USAv/s Urusi, China na hata ugomvi wa USA na EU kipindi cha Trumph.

Nafafanua haya ili tujitambue na kukubali hali tuliyomo kutokana na utajiri wa raslimali. Ripoti za benki ya dunia 2020 zinasema Tanzania ni Nchi ya 8 kati ya Nchi 20 tajiri katika Afrika.

Hili ndilo linatuponza katika ulimwengu wa utandawazi kama mazingira mapya ya unyonyaji usipokuwa makini mbali na fursa zake kadhaa. Yapo mazuri lakini na mabaya yake yapo. Misaada ina uzuri wake na ubaya wake hasa yenye masharti magumu.Kwa sasa ni kipindi cha kubadilisha mbinu za mapambano.

The struggle continues.
 
Endelea kuwananga wahisani jiwe akusikie!
Ndiyo maana kuishi kwako ni hasara kwa taifa. Watu ka ninyi mtakufa mmoja baada ya mwingine, yaani mtakufa kihoro ili nchi iendelee. Si umeona wale wajinga wenzako walijifanya kututukania taasisi yetu ya wananchi ya urais, nadhani unahabari sisi wazalendo tumewakata wote hawana ajira mpaka sasa. Mtakomaaa kabisa wapumbavu kabisa na ujue bado mnashugulikiwa maana kila mtanzania alishajua ujinga wenu kila mkikatiza mnazomewa kama mmejinyea mavi
 
Ndiyo maana kuishi kwako ni hasara kwa taifa. Watu ka ninyi mtakufa mmoja baada ya mwingine, yaani mtakufa kihoro ili nchi iendelee. Si umeona wale wajinga wenzako walijifanya kututukania taasisi yetu ya wananchi ya urais, nadhani unahabari sisi wazalendo tumewakata wote hawana ajira mpaka sasa. Mtakomaaa kabisa wapumbavu kabisa na ujue bado mnashugulikiwa maana kila mtanzania alishajua ujinga wenu kila mkikatiza mnazomewa kama mmejinyea mavi
Huna tofauti na karai tupu wewe
 
nchi za Korea, Singapore, Japan, China, Qatar n.k zimewekeza kwenye elimu na kufanya kazi, watu weusi wao ni kuibiana, kuuwana na kulalamikia wazungu tu
 
Back
Top Bottom