WAKU-GOOGLE
JF-Expert Member
- Jan 20, 2015
- 950
- 623
Wakuu kabla ya mfumo huu wa TCU wanafunzi waliohitaji kujiunga na vyuo mbalimbali walichukua form za chuo husika na kutuma maombi ya kozi ambazo walihitaji kusomea na hii iliongeza chance ya mtu kusomea kozi inayoendana na malengo yake au dreams zake, lakini kwa sasa kwa kupitia TCU mtu atahitaji kuomba kozi nyingi ( mfano mwanzo ilikuwa kozi 12 ila sasa ni 5 ) ambazo kiuhalisia mtu hawezi kuwa na machaguo mengi kiasi hicho wengi wanakuwa na kozi labda mbili wanazozipenda lakini kwa sababu watahitajika kujaza nafasi nyingi na kati ya hizo nyingi wanakuwa wamejaza ili zijaze nafasi zote 12 au 5 kwa sasa ambazo wanatakiwa kujaza.
Wanapochaguliwa kwenda vyuoni ndo kasheshe inaanzia hapo kwani wengi huenda kusomea kozi wasizozipenda na hivyo mtu kutofikia malengo yake ya maisha kama alivyotarajia.
Pia sekretarieti ya ajira sidhani kama inaumuhimu kwani mwanzo wahitimu wa vyuo waliomba katika halmashauri na hii ilipelekea watu wengi kuajiriwa kwa sababu kila halmashauri inakuwa inajua mahitaji yake ya wafanyakazi hivyo kuajiri kila anapohitajika mfanyakazi..... lakini kwa sekretarieti ya ajira ambayo inasimamia ajira zote TZ hali sivyo kwani nafasi zinazotangazwa huwa hazikizi mahitaji ya wafanyakazi katika sekta mbalimbali nchini.. hebu fikiria sekretarieti inaweza ikatoa tangazo moja la kazi na ikapita wiki nzima bila tangazo lolote lingine la kazi kutangazwa hivi ni kweli Tanzania nzima sekta zote zilizopo, mikoa yote iliyopo kweli wiki itapita bila wafanyakazi kuhitajika?
Mi naona ilitakiwa shughuli hizi ziwe-Decentralized kama ilivyokuwa mwazo badala ya kufanyika centralization inayoendelea hapa Nchini.
Kwa swala la kuomba nafasi vyuoni lingekuwa kama ilivyokuwa mwanzo mwanafunzi anaenda chuo husika kilicho na kozi anayoipenda yenye ndoto zake na mwisho wa siku atafikia malengo yake na si hii bahati nasibu ya TCU unaweza pelekwa kozi ambayo hujawahi wazia.
Nawasilisha mawazo yangu wakuu.