Utaratibu wa kupata results transcript nactvet ubadilishwe ni kero kubwa mno

bukugu

Member
Jan 5, 2023
20
36
Wakuu Habari zenu.

Nimeandika uzi huu baada ya kupata usumbufu wa zaidi ya miezi miwili nikifuatilia transcript, ili kushauri nini kifanyike kuondoa kero hii inayowakuta wengi.

Kwanza itambulike wanafunzi wote wanaohitimu na kufaulu masomo Yao katika vyuo vyote vinavyosimamiwa na nacte especially ngazi diploma na certificate wanatakiwa kupata cheti na transcript baada ya kuhitimu lakini vyeti pekee ndio hutumwa vyuoni na transcript itapatikana baada ya muhitimu kuiomba online na kuifata katika tawi lolote la nacte

Changamoto zilizopo katika utaratibu huu ni kama ifuatavvyo;

1. Gharama za kusafiri hadi kwenye ofisi za kanda kwa ajili ya kufatilia transcript

2 Changamoto ya mtandao endapo mtu akikosea wakati wa kutuma ombi la transcript inalazimika kufunga safari hadi ofisini kwao ili kufatilia na njoo kesho ni nyingi sana

3. Mfumo una changamoto ya kuleta taarifa za mtu aliesoma kozi zaidi ya moja, unaleta taarifa za kozi ya mwisho kuisoma au unayoisoma kwa wakati huo lakini ukihitaji transcript za kozi ulizosoma huko nyuma lazima usafiri adi ofisin kwao na mara nyingi tatizo hili hutatuliwa makao makuu tu.

USHAURI;
1. Transcript zitumwe kwa kuambatana na vyeti vyuoni ili mtu anapofata cheti anachukua na transcript yake hapo hapo ...hii itakata mzizi kabisa wa tatizo hili sababu kila muhitimu anayefaulu na kupata cheti anahitajika kuwa na transcript pia haina maama kuprint na kutuma vyeti pekee chuon na Kisha kubaki na transcript ili zifatwe maofisini.

2. Kama issue ni kukusanya mapato kupitia fees zinazotozwa wakati wa kuomba transcript. Hili linaweza kuwa solved kwa kuweka utaratibu wa kila mwanafunzi kulipia transcript fee akiwa katika mwaka wake wa mwisho wa masomo utaratibu huu upo kwa michango mingine pia ambayo hulipwa kwenda nacte kila mwaka wakati wanafunzi wakiwa bado wapo vyuoni mfano Quality assurance.

3. Wanafunzi wanaosoma na kuhitimu kozi zaidi ya moja ngazi ya diploma au cheti watapata transcript ya kila kozi baada ya kuhitimu kama zitatumwa na vyeti kwa pamoja hii itaondoa kabisa tatizo hilo.

MWISHO: Mapendekezo hayo yataondoa zaidi ya asilimia 70% mpaka 80% ya watu ambao hufika katika maofisi ya nacte kwa sababu ya transcript hivyo ofisi hii itajikita zaidi kwenye kusimamia ubora wa elimu na ku-solve matatizo mengine ambayo ni ya msingi zaidi Kwamfano tatizo la vyuo kuwatapeli wanafunzi kwa kuendesha program ambazo hazitambuliki na baraza na baraza kushindwa kutambua hujuma hizo kwa wakati mpaka wanafunzi kusoma kwa mwaka mzima au miwili halafu wanakuja kutotambulika.

Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom