Mfumo wa pesa kizungumkuti

seanherms

JF-Expert Member
Apr 27, 2014
528
409
Salaam wakuu

Leo kijana wenu nimewaza sana kuna jambo silielewi..lakini naamini hapa wapo wahusika wakunisaidia au hata wale wenye ujuzi

Hivi pesa inapotengenezwa(kiwandani sijui) taifa husika linaenda kuinunua au wanabadilishana vipi?yaani ukiweka oda ya kutengenezewa hela wewe unapeleka nini unapoenda kuchukua pesa zako?

Na kama kuna biashara hufanywa hua wanabadilishana na kitu gani?

Je kweli wanainunua kwa pesa?yaani umuuzie ng'ombe maziwa au nyama.duuuuh!yeye anaitengeneza sasa wewe unampa nini?

Na je?inapotengenezwa ni kua ya zamani inateketezwa au au zinazidi kujazana?

Karibuni mnisaidie wakuu

Shukran.
 
Hapo hapo... ni kiasi gan hutengenezwa kwa mwezi...? Na ikija inaingilia wapi....? I mean anapewa nan
 
hata mm nayataman kweli majibu ya hayo maswali, naona wachumi wametoka kidogo.....ngoja niendelee kusubiri
 
Serikali inayohusika inalipia gharama za kuchapisha fedha. Kuna kampuni maalum kwa kazi hiyo, nyingi ziko Uswizi. Serikali inatoa matakwa yake, inapewa gharama za kuchapisha hizo fedha na kusafirisha. Halafu mzigo ukiwa tayari serikali inawalipa waliuochapa fedha. Mara nyingi kwa kutumia dola za Marekani.

That's as far as I know.

Habari ya kuchapisha fedha haihusiani ha uchumi halisi moja kwa moja. Unaweza kuchapisha fedha kedekede wakati huna uchumi mzuri, hili huweza kusababisha mfumuko wa bei "inflation" au mpasuko wa bei "hyper-inflation".

Uchumi wenyewe upo katika uzalishaji, ugavi na urari kwa mujibu wa matakwa ya soko.
 
Serikali inayohusika inalipia gharama za kuchapisha fedha. Kuna kampuni maalum kwa kazi hiyo, nyingi ziko Uswizi. Serikali inatoa matakwa yake, inapewa gharama za kuchapisha hizo fedha na kusafirisha. Halafu mzigo ukiwa tayari serikali inawalipa waliuochapa fedha. Mara nyingi kwa kutumia dola za Marekani.

That's as far as I know.

Habari ya kuchapisha fedha haihusiani ha uchumi halisi moja kwa moja. Unaweza kuchapisha fedha kedekede wakati huna uchumi mzuri, hili huweza kusababisha mfumuko wa bei "inflation" au mpasuko wa bei "hyper-inflation".

Uchumi wenyewe upo katika uzalishaji, ugavi na urari kwa mujibu wa matakwa ya soko.

sasa mkuu anaekutengenezea hela unampa ela tena?mmmmmh kweli kizungumkuti
 
Mara nyingi malipo ya kutengeneza pesa huwa ni kubadilishana vitu vyenye thaman kubwa baina ya serikali/nchi inayotengenezewa pesa na kampuni inayohusika ktk kutengeneza hizo pesa,mara nyingi nchi hutoa akiba yake ya dhahabu,almasi,tanzanite au madini mengine yenye thaman kubwa kama malipo ya kutengenezewa pesa kulingana na makubaliano watakayokua wameafikiana.
 
Na vile vile labda me ndo cjakuelewa swali lako au vp!unaposema pesa mpya znapotengenezwa una maana currency mpya au notes mpya?

Kama jibu ni currency mpya,basi inapotokea new currency inatengenezwa,ile ya zamani itaondolewa kwenye mzunguko,then mara nyingi huwa zinakua destroyed either kwa kuchomwa moto au kwa namna nyingne.na kama jibu lako ni notes mpya,kinachofanyika ni kwamba,commercial banks ndo huwa zina kazi ya kupokea notes zote chakavu na zisizo chakavu then huwa wanaenda kuzideposit kule central bank,sasa central bank huwa inaangalia ni notes gani ambazo zimechakaa sana ndo baadae wanaamua kutoa notes mpya kwenye mzunguko kwa kuzingatia number za notes husika,zile chakavu nazo huwa zinakua destroyed chin ya uangalizi wa central bank e.g BOT kwa hapa kwetu.

Suala lingine,pesa huwa hazitengenezwi kila wiki kama unavyodhani,pesa huwa zinatengenezwa pale inapotokea kuna mahitaji ya kufanya hvyo,kinachofanyika,pesa huwa zinatengenezwa then zinawekwa kwenye reserve ya taifa ambayo ni central bank,sasa central bank ndo huwa ina mamlaka ya kuziingza pesa hzo kwenye mzunguko kwa kuzingatia vitu kama demand and supply,purchasing power of money,volume of money in circulation nk.
 
mmmm hapo bado... labda Kiranga
.... 10000 tunatengenezewa kwa gharama gan..?
 
Last edited by a moderator:
sasa mkuu anaekutengenezea hela unampa ela tena?mmmmmh kweli kizungumkuti

Hela mbona ni bidhaa tu, inauzwa na kununuliwa kwa hela hata baada ya kuchapishwa.

Unapoenda benki kuomba mkopo, ukapewa mkopo kwa interest rate si unakuwa umenunua hela kwa hela hapo, au vipi?
 
Huu mfumo wetu wa elimu kweli ni shidaaaa. Mpaka mtu anajiunga na jamii forum hajui maana ya pesa, ilianza vipi, inahusiana vipi na uzalishaji, ina maana gani mzunguko wa fedha, kwa nini kuna noti chakavu na mpya? Hii nchi sasa ipo hatarini. Wengi waliopo jamii forum ni watu ambao wameshamaliza sekondari. Lakini elimu ya kawaida ya dunia hwaijui. Maana yake wamenyimwa haki hiyo mpaka mwisho wao. Hii inatisha sana. Kuzaliwa mjinga, kuishi mjinga na kufa mjinga. Basi tujipange walau kizazi kijacho wasiishi ujinga huu.
 
gram moja ya dhahabu.

mkuu unachojibu unahakika nacho au unahisi tu? Thamani ya dhahabu gram moja soko la dunia likiyumba huwa ni elf 54 halafu leo utengeneze noti ya thamani ya elf 10 kwa elf 58 hiyo si ni biashara kichaa kabisa? Au mie cjaelewa labda ulmanisha uzito wa noti ya elf 10 ni sawa na gram 1 ya dhahabu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom