Mfumo wa kuchezesha wachezaji wa Academy kwa Tanzania upo?

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,111
115,905
Kwa wale tunaofatilia Sana mpira wa Ulaya mtakua mnajua jinsi wenzetu wana mifumo wa kuruhusu wachezaji wa Academy kucheza mechi yeyote wakati wowote na timu kubwa.

Mchezaji wa academy anakuwa hawekwi kwenye list ya waliosajiliwa lakini wakati wowote akionekana anafaa anapandishwa tu kucheza na wakubwa bila kusubiri msimu wa usajili, huu mfumo unawapa nguvu Sana wachezaji WA Academy kupata uzoefu.

Nauliza huu mfumo tunao Tz? Sijawahi sikia Simba au Yanga wameleta mchezaji kucheza ligi kuu ambae alikuwa academy unless awe ameshatajwa kwenye usajili mwanzo wa msimu.

Naomba kuuliza huu mfumo upo na kama haupo why usiletwe?
 
Navyojva mchezaji wa academy au timu b,wanaruhusiwa kuwa timu ya wakubwa wasizidi watano.

Mchzaji huyo anaeza cheza ligi bila kusajiliwa, mfano pale yanga yule clement mzize
 
Clement msize ametokea academy ya yanga. Na kuna mchezaji alikuwa anacheza namba 6 aliuzwa kutokea yanga kwenda biashara nadhani.
Hujanielewa nahisi...alipokuwa academy alikuwa anacheza ligi kuu hata mechi moja moja kama wenzetu??au wachezaji WA Academy hawachezi Hadi wasajiliwe rasmi??
 
Navyojva mchezaji wa academy au timu b,wanaruhusiwa kuwa timu ya wakubwa wasizidi watano.

Mchzaji huyo anaeza cheza ligi bila kusajiliwa, mfano pale yanga yule clement mzize
Ukishasema wasidi watano manake hawakubaliwi....ina maana hao watano lazima watajwe kabla ligi haijaanza...wakati ... wenzetu mradi yupo academy...wakati wowote akiiva anacheza ligi kuu
 
Ukishasema wasidi watano manake hawakubaliwi....ina maana hao watano lazima watajwe kabla ligi haijaanza...wakati ... wenzetu mradi yupo academy...wakati wowote akiiva anacheza ligi kuu
watano ktk mechi,we katika kikosi ukiona wanafaa wanacheza bila usajili
 
Tanzania sio Simba na yanga


Winga tepsie Evans Azam wamempandisha kutokea
Chini na amefanya vzr na wapo wengi kwa Azam

Kiuhalisia timu zetu hazina academy Bali Kuna timu za vijana na kuhusu vijana kutoka chini kupewa nafasi timu kama mbeya city imefanya hivyo sana Richardson ng'ondya kipaji chake kilionwa na mbeya city kwenye ndondo mtaani wakamchukuwa na hajakaa sana timu ya vijana akapandishwa hivyo hivyo kwa selemani Ibrahim kipaji chake kilionekana uyole saizi yupo geita nk

Mtibwa ndio wamezalisha sana vijana kutoka timu b Wana uzao mkubwa ligi kuu kwa miaka mingi
 
Klabu zenyewe hazina academy bali timu za vijana waliokomaa tayari. Vijana wa miaka 17,18 n.k wanakusanywa na kuunda timu ya vijana.
 
Back
Top Bottom