SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,114
- 7,863
Kabla hata ya derby ya Simba na Yanga, kulizuka utata kuhusu upangwaji wa golikipa wa Simba Beno Kakolanya katika mechi muhimu za Simba wakati Aishi Manula akiwa majeruhi. Utata huu ulikuja baada ya kusemekana kuwa Beno amesaini kuchezea Singida Big Stars (SBS) kuanzia mwishoni mwa msimu huu. Ikaonekana Beno anaweza kuisaliti Simba kwa manufaa ya SBS (na hata Yanga kutokana na ukaribu wa timu hizi mbili) katika mechi hizi za mwisho.
Dirisha dogo la usajili lilishafungwa, timu zote sasa hivi zipo katika harakati za kumaliza ligi. Inawezekana majadiliano ya uhamisho wa Beno yalianza kitambo, labda tokea dirisha dogo lililopita na labda yalikwama au yalisitishwa mpaka mkataba wake utakapoisha mwishoni mwa msimu.
Sasa kwa nini kumetokea kutomuamini Beno ghafla hivi? Sasa hivi Beno analipwa mishahara na bonus kama wachezaji wengine ila haaminiki na club hadi kupelekea kipa chaguo la 3 kucheza badala yake. Swali ni lini Beno alisaini kuchezea SBS?
Je, sheria za usajili zinasemaje pale wakala wa wachezaji au maofisa wa timu kuwasiliana na mchezaji wa timu nyingine katika kipindi ambacho siyo rasmi cha usajili kwa nia ya kumshawishi mchezaji huyo kujiunga na timu nyingine?
Maana ya madirisha ya usajili ni nini iwapo kunatoa fursa kwa wachezaji kusajiliwa katika kipindi ambacho siyo rasmi na matokeo yake kuleta mikanganyiko na sintofahamu kama hizi za sasa?