Mfumo wa internet Mbezi Stend

Mfumo wa internet Mbezi Stend

fundi msati

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2013
Posts
219
Reaction score
91
Habari Wana JF,
Kunajambo niliiona pale kituo kikuu Cha mabasi Cha magufuli mbezi kwanza nilikipenda kisha kikanishangaza ila kimenishawishi kukifanyia kazi.

Kuna siku nilikuwa safarini kuelekea mkoani nikiwa na kisimu changu mwenyewe maisha yanaenda nilipofika Mbezi nilikuwa nimechelewa sana nikakosa usafiri. Kwa muda ule mpk ifike alfajiri, usiku ule nikawa pale nasindikizwa na burudani ya simu yangu ghafla ikaanza kunipelekesha mpka nikalazimika kureset, ilipoamka ikanitaka kutumia Wifi na kila nikigeuka huku na huku kupata msaada watu wengine wakawa wamelala

Nikatoka pale nikawa naangaza huku na huku nikawaona vijana wawili wameweka benchi nje ya maduka yao wanaendelea na stori zao, nikaenda nikawaomba msaada kuhusu shida yangu mmoja akanielekeza sehemu sahihi ya kupata msaada kufika pale nikaona matangazo kwamba huduma ya internet inapatikana nilisoma maelezo nikaambiwa naweza kulipa Kianzio cha sh 200 na kuendelea nilipolipa kwa kutumbukiza 200 yangu nika Scan palepale nikapata wifi.

Mpaka sasa bado naiwaza ile huduma na nahisi kama ni kabiashara katamu kwa hapa dukani kwangu jamani ajuae zaidi fursa changamoto ubora zaidi wa hii issue tafadhari mnisaidie maalifa na gharama zake japo Kwa makadirio.

Natanguliza shukran
 
Back
Top Bottom