Mfumo wa Digital: 'Local Channels' watoa kilio kwa serikali

Mfumo wa Digital: 'Local Channels' watoa kilio kwa serikali

In short serikali ilikurupuka hawakuangalia majority na vipato vyao walikiangalia wao tu na ndugu zao. To hell**

chezea rushwa wewe,!? watu wameshaagiza manowari imejaa ving'aaa muuzi unafikiri wataacha kusukuma sirikali ifanyemaamuzi wayatakayo?
 
Mpaka 2015 cha moto tutakuwa tumekiona.
 
Ni kweli wanahaki kabisa ya kuzima mitambo yao,Serikali yetu hii inaendesha kwa maslahi ya mtu mmoja,ni kweli mfumo wa (Digital) djitali ni mzuri na ina mambo mengi sana(maana hadi sasa hakuna anayefaidi mfumo wa Digital kwakua wananchi wengi wanazo tv za analojia) kama tukiingia jumla,lakini kinachoniudhi mimi,ilikubaliwa kimataifa ifikapo mwaka 2015 basi mitambo yote ya analojia (Analog) zisitumike tena sasa sijui kwanini serikali imewalazimisha wananchi wake kuingia mapema tena bila maandalizi ya kutosha,lakini pia ni kuwalazimisha wameliki wa tv station kurusha matanagazo yao kwa kupitia kwenye vyombo vya watu wengine (Starmedia,Easy tv,agape tv n.k) ni kwanini wasingewaruhusu waendelee kurusha wenyewe bila kulazimka kupitia media nyingine ambazo wanalazimiswa kulipa. Kurusha wenyewe ingewezekana na ingewarahisishia sana wananchi kwani pamoja na ukweli kwamba lazima wangeitajika wanunue ving'amuzi(Receiver) lakini wngekua na uhuru wa kuchgua king'amuzi wakipendacho,namaanisha wangenunua kama wanavyonunua deki ya cd dukani bila kulazimika kupitia kwenye kampuni za kulipia kama ilivyo hivi sasa. Ingekua unaenda dukani nunanunua kin'amuzi chochote ukipendacho then unapata channel zote ambazo ni (free to air) hazilipiwi kuliko ilivyo sasa hizo za bure kuna wakati nazenyewe wanzifunga baada ya muda wazirudisha lengo ni kuwasumbua tu wananchi ili wakalipie.
 
Nafikri tatizo hasa ni katika mikoa iliyotegemea nalog hasa dar! kwa mikoani watu wana kula digital 10 years ago via cable servise !
 
CCM wanataka mpaka 2015 kuwe hakuna analojia, ni njia ya kuwadhibiti wananchi wasipate habari.
Wameshaona wananchi wanaelewa sana mambo. Hivyo wanatafuta njia za kuwazibiti!
Ndiyo uzuri wa visual aid katika kufafanua jambo....yaani kwa walimu wanaoutumia zana bora za kufundishia wala hawapati tabu kufundisha.

Televisheni ni zana bora kabisa kwa kuwataarifu wananchi kinachoendelea....hivi wakizima. si ndo itakula kwetu kabisa sisi wananchi?.

Lakini nadhani Jamiiforums.com yaweza kutumia fursa hii kuangalia namna ya ku'exploit' hii nafasi ya ombwe(kama watazima mitambo yao) la upatikanaji wa habari, kwa kuanzisha forum ya video clips ambazo zitakuwa zimebeba habari za kutwa nzima ya siku hiyo....lakini zihaririwe na moderator maalum ambaye atakuwa anazirusha saa mbili usiku na kuziondoa saa moja asubuhi siku inayofuata. Utaratibu huo pia uendelee kwa siku zinazofuata.

Cha msingi ni kuhakikisha video hizo zinawekwa kwenye format ambayo itaweza kusomwa na applications/systems za aina nyingi za simu na kompyuta na zana nyingine za ki-elekroniki. kwa simu zitakazo shindwa basi hata audio ya clips hizo zisikike.

Wazo hili ninaruhusu lifanyiwe marekebisho inavyopaswa na litekelezwe hapa hapa Jamiiforums.com na si mahala pengine. Hairuhusiwi kutumia wazo hili mahala pengine bila idhini ya wote kwa pamoja mtoa wazo (yaani member wa JF mwenye JF ID ya MpigaKelele) na Jamiiforums.com
 
Kweli serikali inayoishi kwa rushwa ni balaa na mzigo mkubwa sana kwa raia wake,kuanzia VEO mpaka rais wote wajanjajanja
 
hakukuwapo na haja ya kufunga kabisa watu wangejichuja tu wenyewe,:yo: anayetaka matangazo yake angalipia akaangalia. sasa hii ya jumla na huyo mzee wa miaka 7o yuko kijijini television yenyewe kapelekewa na wajuu zake amekoasa kuona Nyerere wake maana wale wezee wetu bado wanaamini Nyerere yupo. wameingia kwenye mkumbo.Nadhani kulikuwapo namna ya kufanya ili kuweka mlinganyo , sasa inategemea interest ilikuwa wapi!!!. SERIKALI NI SIKIVU ITALIFANYIA KAZI.
 
  • .......Binafsi nililiona hili siku moja baada ya mitambo ya anolojia kuzimwa nilishuhudia nyumba nyingi hasa za uswahilini wakiachwa bila kuangalia TV.. niliandika humu na hadi leo asilimia kubwa ya waTZ bado hawajanunua ving'amuzi..
  • .
  • Sio utani badhi ya watu wameshazoea kutokuangalia TV.. Si unajua Mungu alivyo tuumba wanadamu kusahau na kuzoea???

  • Wengi wanazoea kwa kuwa sio chakula kwamba akikosa kuangalia TV kuna madhara atakayopata au atakufa..

  • Kwa maana hiyo serikali itambue wazi kuwa tofauti ya walionacho na wasionacho ni kubwa mno na inazidi kuongezeka...

  • SERIKALI itoe Uhuru kwa wananchi waangalie TV kwa njia gani digial au anolojia. vinginevyo kwa kweli hali ni ngumu na itaendelea kuwa ngumu
 
Madai yao hayana msingi,pengine kama wanataka kuthibitisha kwamba Tanzania ni Dsm. Mikoani bado mitambo ya Analojia ipo hewani,itakua inazimwa kwa awamu. Ningewaelewa kama wangeiomba serikali kuondoa ushuru na kodi ktk decoder ili bei ishuke,watu masikini waweze kununua. Walipewa muda wa kutosha lakini kama kawaida yetu wakadharau,wakaona hata hili zoezi litashindwa kama usajili wa namba za simu.

Kwa hiyo hapa wewe ulitakaje kama hoja yao kwa sasa hawaletewi matangazo, ulitaka waitishe matangazo yote ya biashara kabla ya digitali au ulitaka wawanunulie wananchi ving'amuzi? Tumieni akili japo hiyohiyo ya kimasburi. Suala sio walipewa muda, hiyo "post-normative thinking". Fact ni kwamba wako kwenye no loss, no profit, hivyo wakitoka hapo; offcourse lazima wafunge, na ni ukweli kwamba idadi ya waona tv imepungua sana, hivyo ving'amuzi bado viko katika mikono ya uuzaji wa ki-"hot deal" haijafika kwa Chinga bado. Nyie mwazani mnavyopata fedha zenu kwa perdiem na madeal mengine bac na sie wa mbambay mnadhani tunalipwa hivyo. Yote haya ni matokeo ya "quantity" ya graduates na wala siyo " quality" ya graduates. Mi ndio maana nimehama nchi hiyo, wanaishi binaadam lakini akili za "wanyama". Samahani kama nimekukwaza.
 
Kama hawa jamaa walikuwa na nia njema ya kuwahurumia Watanzania ile haki ya kupata habari, then Mzee Mengi, angekigawa bure hicho kingamuzi chake cha Digitek, na kwa vile chenyewe ni cha digital wakati hiki cha Star Time ni cha analogue, mtu angeona signal ya digital asinge thubutu tena kurudia "takataka" ya analogie!, hivyo Digitek ingepiga bao la kisigino kuwakomba watazamaji wote, na hivyo kukomba matangazo yote!.

Tena ili kuonesha anawajali sana wananchi, ITV ingerusha bure vipindi vya nje kama hivi ambavyo tunawapelekea, ili wananchi wapate habari zao na kuona vipindi zaidi vya logal contents na hili lingefanyika, mngeona hadi Isidingo zetu wenyewe na "soap" za Kiswahili!.

nadhani wewe Pasco siku hizi Umri inversely proportional na fikra zako. Kati ya TBC na ITV ipi ilitakiwa inunue king'amuzi na igawe bure? Kati ya Mengi na Mkuu wa kaya, nani alitakiwa anunue king'amuzi na kukigawa bure?
 
Tatizo ni kwamba watanzania wengi tunawahesabu wanaoishi mjini tu. TV ni kwa watu wa mjini na siyo kwa wakulima na wafugaji wa vijijini. Watanzania walio wengi hupata HABARI kwenye REDIO ambazo pia huwapa burudani ya Muziki na Matangazo. wao hawapambanui digitali wala analogia ili mradi wanapata taarifa za habari kutoka TBC taifa, BBC, SAUTI YA UJERUMANI, Radio one na Radio free africa. Mimi naona tuendelee mbele na Digitali ila tuiboreshe. WaTz kila kitu huwa tunasema ni Ghali hata kama kuna Ving'amuzi vya Saizi yetu kama vile Star times ambayo bei yake haifiki elfu 60 kuimiliki. Local Channel kama ITV, STARTV, CH10, EATV, TBC1 hupatikana bure hata kama hujalipia. Labda wamiliki wa hizi Local Channels waseme kama wao wanatozwa pesa nyingi kujiunga na Star Times. Vya bure kwa dunia ya Sasa hakuna kila kitu Pesa hata kujisaidia Msalani!
 
wasirushe matangazo...nchi ya migomo hii hata rais nae atagoma.
 
Wananchi wenzangu mnanishangaza sana! mnadhani hao MOAT wanatutetea?

Hivi analogia ikirudi channel ngapi zitafika hata Bukoba mjini? Zamani cable tv ikikata hakuna altenative pale Bukoba ni TBCCM tu!!

Wanaokosa matangazo ni wakazi wa Dar tu ambao wanakijiunafuu wa maisha!

Hawa wamiliki wameona profit zita drop na watashindwa kushindana!

Hebu fikiria MTV Vs Clouds tv kwi kwi kwi!!! Lazima walalame!
 
Unaenda hatua mbili unarudi nyuma hatua kumi....
 
nadhani wewe Pasco siku hizi Umri inversely proportional na fikra zako. Kati ya TBC na ITV ipi ilitakiwa inunue king'amuzi na igawe bure? Kati ya Mengi na Mkuu wa kaya, nani alitakiwa anunue king'amuzi na kukigawa bure?
Mkuu Zine, sio kosa lako na ndio maana Watanzania ni masikini wa kutupwa na tunaendelea kuwa masikini kwa kunyonywa na kukamuliwa na hawa mabebari na mabeberu mpaka tubaki mifupa mitupu!.

Chukulia king'amuzi ndio digital handset, huyu Mzee angekuwa na kampuni ya simu enzi za technology transfer ya simu toka analogy kwenda digital, pia angeomba simu za analogie ziendelee!, what for?!.

Makampuni ya simu ya wenzetu wanatoa handset bure na kuzilipia ndani ya subscriptuion fee!. Ningekuwa mimi ndio Mengi, ningeleta ving'amuzi vyangu vya digitek, milioni 20!, na kuvigawa bure, huku nikiwakata kwenye subscription!, katika profile ya ITV, naeleza wazi katika taifa la watu milioni 45, watu milioni 20, wanaangalia ITV!, unadhani nani angeendelea kununua king'amuzi cha Star Time ambacho ni cha analoguie?!. Nani angeendelea kutangaza na TBC yenye horrible uninteresting programs?!.

Ifike mahali Mzee Mengi, apunguze kulia kulia lia na kumwaga "crocodile tears!", ukifuatilia trend yake, Mzee ni mliaji mzuri, toka kile kile cha "mchezo mchafu" wa Kilimanjaro hotel, kalia na Masilingi, Masilingi Chali!, Kalia na Masha, Masha chali!, kalia na Tido, Tido chali!, sasa anataka kulia na Prof. Nkoma, tena Prof, amemuheshimu sana kumjibu, otherwise, this time ana taka ku press the wrong button!.

Mark my words, mtaniambia!.

Pasco.
 
In short serikali ilikurupuka hawakuangalia majority na vipato vyao walikiangalia wao tu na ndugu zao. To hell**

Agree with u, watu wengi sasa TV zimekuwa za kuangalia movie tu, Wauza cd za movie na waazimishaji biashara imeshamiri!
 
Mkuu Zine, sio kosa lako na ndio maana Watanzania ni masikini wa kutupwa na tunaendelea kuwa masikini kwa kunyonywa na kukamuliwa na hawa mabebari na mabeberu mpaka tubaki mifupa mitupu!.

Chukulia king'amuzi ndio digital handset, huyu Mzee angekuwa na kampuni ya simu enzi za technology transfer ya simu toka analogy kwenda digital, pia angeomba simu za analogie ziendelee!, what for?!.

Makampuni ya simu ya wenzetu wanatoa handset bure na kuzilipia ndani ya subscriptuion fee!. Ningekuwa mimi ndio Mengi, ningeleta ving'amuzi vyangu vya digitek, milioni 20!, na kuvigawa bure, huku nikiwakata kwenye subscription!, katika profile ya ITV, naeleza wazi katika taifa la watu milioni 45, watu milioni 20, wanaangalia ITV!, unadhani nani angeendelea kununua king'amuzi cha Star Time ambacho ni cha analoguie?!. Nani angeendelea kutangaza na TBC yenye horrible uninteresting programs?!.

Ifike mahali Mzee Mengi, apunguze kulia kulia lia na kumwaga "crocodile tears!", ukifuatilia trend yake, Mzee ni mliaji mzuri, toka kile kile cha "mchezo mchafu" wa Kilimanjaro hotel, kalia na Masilingi, Masilingi Chali!, Kalia na Masha, Masha chali!, kalia na Tido, Tido chali!, sasa anataka kulia na Prof. Nkoma, tena Prof, amemuheshimu sana kumjibu, otherwise, this time ana taka ku press the wrong button!.

Mark my words, mtaniambia!.

Pasco.

Mkuu Pasco, yawezekana uko sahihi kabisa lakini kuna masuala kadhaa huna budi kuyazingatia. Industry ya cim ni tofauti sana na industry ya habari kwa njia ya televisheni. Kwa kiasi kikubwa undeshaji wa Tv hususan kwenye nchi zinazoendelea umejiegemeza sana kwenye "public utility" wakati uendeshaji wa cim ni "private motive utility", hivyo mabadiliko haya kama yangelitokea katika cim(katika kipindi hiki) huenda yangeweza kuji-stabilize yenyewe kwa urahisi. Na pia industry ya simu sasa hivi unaweza uka-temper nayo utakavyo lakini si tv. Pia makampuni yetu mengi hayajafikia kiwango cha "economies of scale" ya kufanya hivyo unavyoshauri. Anagalia ukuaji wa sekta ya mawasiliano ya cimu na angalia kasi ya ukuaji wa sekta ya habari-tv, kumfanya mtu amiliki cim na kuitumia ni rahisi sana kuliko kuliko kumfanya mtu amiliki tv na kuitumia(High volatage), watu vijijini huko just mtu mmoja akiwa na charging system inatosha kuwezesha kijiji chote kuchaji cim zao na "kuchangia" makampuni ya cim. Pia teknolojia ya cim, isipokuwa hewani kutokana na charge, once utakapoiwasha unakuta missed call zote ulizopigia so unakuwa umepotea na muda lakini hukupotea kimawasiliano, Hii ni tofauti na tv mkuu, Umeme na bulkiness ya teknolojia yake ni mzigo kidogo. Lakini pia unaposema si kosa langu sjui unamaanisha nn hapa, na unaposema mabepari wanaotunyonya je unamaanisha hawa wenye tv au unamaanisha hawa wenye (Multinational Companies, MNCs)?. Mimi sizungumzii mtu, wether ni mengi au nani, nazungumzia uhalisia wa tukio hili lilivyotokea na hoja yao nini? Unajua mkuu industry ya tv ngumu sana ina series nyingi za ukamilifu wake; Uwe na Umeme, uwe na TV, uwe na muda wa kukaa kuangalia hiyo tv(kwani kuangalia kupitia mobile phone kama huku nchi za ulaya sio common).Kwa hiyo mfumo wake ni kuacha abiria zaidi kuliko kujaza abiria na kuondoka nao. Hivyo kama wenye tv wanasema kumekuwa na upungufu wa wafuatiliaji wa tv, wako sahihi; Nini solution? Huenda kurejea katika analogia sio suluhu kwani ni kuahirisha tatizo, Serikali ifanye intervention ya namna rahisi na bora ya kupatikana ving'amuzi badala ya kuwaachi nyie kina " pasco" mfanye dili la kuwaibia watu, hili ndio tatizo lenu wenye madaraka huko bongo, hamtosheki na vya halali mpaka mfanye haramu!!!
 
Hawakusema watafunga , lakini tunajua gharama zikizidi mapato ni nini kitakochofuata. Kama wafanya biashara wanahaki ya kulalamika pale biashara zao zinapoathirika. Wana commitments za wafanyakazi na gharama nyinginezo za kila siku. I support them. Kuwepo na system mbili parallel ili walalahaoi tusiyupe mitungi yetu ya TV.
Let's be objective here!! Ving'amuzi vya Startimes ni Sh. 39,000/=, plus first bundle ya TZS 9000 ni Sh. 48,000/=. Mimi binafsi yangu, tangu ninunue mwaka jana July, nimelipia mara moja tu na hadi sasa naona FREE CHANNELS ambazo zipo tano.

Sasa tuje huyu mwananchi maskini ambae hana uwezo wa kulipa hiyo TZS 48,000/=. NI kweli, wapo! Sasa masuala ya kujiuliza na haya hapa:
1. Hivi mwananchi ambae piga ua ameshindwa kabisa kupata TZS 48,000/=; huyu kweli huwa ananunua sabuni za Ariel na nyinginezo zinazotangwazwa kwenye TV wakati kuna sabuni za mafungu kibao mitaani ambazo bei yake ni nusu ya ile zinazotangazwa?!
2. Hivi kweli mwananchi huyo kweli huwa ananunua Pampers za watoto zinazotangazwa kwenye TV wakati kanga kuu kuu za mama mzazi zipo za kumwaga achilia mbali NEPI?!
3. Hivi kweli mwananchi kama huyo huwa ananunua zile Always na Angels wakati kuna vitu vinaitwa GOZI?
4. Hivi kweli huyu ananunua mimaji mnayotangaza kwenye TV wakati kila pahala kuna maji ya Kandoro ya TZS 50?
5. Hivi kweli huyu yupo interested na mi-internet bundles yenu inayotangazwa kwenye TV wakati hata hiyo Browser haijui?!
6. Hivi kweli huyu ana mpango na FastJet yenu mnayoitangaza kwenye TV?
7.....ONGEZA MWENYWE.....manake yapo mengi ambayo sana sana wanaona mnawaletea kejeli tu!

You know where my point is?! Sioni namna yoyote ni namna gani matangazo yanashuka kwavile tu Watanzania maskini wameshindwa kununua ving'amuzi! Maskini kama huyu wala time na hayo mnayoyatangaza hana...., hana si kwa sababu hataki, hana time coz' hata hela yenyewe ya kununulia hivyo vitu hana!! We ushaona vitenge vinatangazwa kwenye TV? Hizi ndio nguo za akina sisi tusio na uwezo wa kununua ving'amuzi!! Hata ukitumia mwaka mzima mfululizo kutangaza zile za Hussein Pamba Kali, achilia mbali za Woolworth, huko hatuji!! Tuje kufanya nini wakati Tandika napafahamu?!

Hoja ya msingi ninayoina mimi labda hiyo ya kuwanyima uhuru wa habari, lakini ya mapato, effect yake ni ndogo sana! Inawezekana ni kweli advertisers wamepunguza matangazo yao bila kufahamu kwamba population ya bidhaa zao wala sio hii ambayo hata uwezo wa TZS 48,000/= hawana!
 
Hawakusema watafunga , lakini tunajua gharama zikizidi mapato ni nini kitakochofuata. Kama wafanya biashara wanahaki ya kulalamika pale biashara zao zinapoathirika. Wana commitments za wafanyakazi na gharama nyinginezo za kila siku. I support them. Kuwepo na system mbili parallel ili walalahaoi tusiyupe mitungi yetu ya TV.
Let's be objective here!! Ving'amuzi vyaStartimes ni Sh. 39,000/=, plus first bundle ya TZS 9000 ni Sh. 48,000/=. Mimibinafsi yangu, tangu ninunue mwaka jana July, nimelipia mara moja tu na hadisasa naona FREE CHANNELS ambazo zipo tano.

Sasa tuje huyu mwananchi maskini ambae hana uwezowa kulipa hiyo TZS 48,000/=. NI kweli, wapo! Sasa masuala ya kujiuliza na hayahapa:
1. Hivi mwananchi ambae piga ua ameshindwa kabisakupata TZS 48,000/=; huyu kweli huwa ananunua sabuni za Ariel na nyinginezozinazotangwazwa kwenye TV wakati kuna sabuni za mafungu kibao mitaani ambazobei yake ni nusu ya ile zinazotangazwa?!
2. Hivi kweli mwananchi huyo kweli huwa ananunuaPampers za watoto zinazotangazwa kwenye TV wakati kanga kuu kuu za mama mzazizipo za kumwaga achilia mbali NEPI?!
3. Hivi kweli mwananchi kama huyo huwa ananunuazile Always na Angels wakati kuna vitu vinaitwa GOZI?
4. Hivi kweli huyu ananunua mimaji mnayotangazakwenye TV wakati kila pahala kuna maji ya Kandoro ya TZS 50?
5. Hivi kweli huyu yupo interested na mi-internetbundles yenu inayotangazwa kwenye TV wakati hata hiyo Browser haijui?!
6. Hivi kweli huyu ana mpango na FastJet yenumnayoitangaza kwenye TV?
7.....ONGEZA MWENYWE.....manake yapo mengi ambayosana sana wanaona mnawaletea kejeli tu!

You know where my point is?! Sioni namna yoyote ninamna gani matangazo yanashuka kwavile tu Watanzania maskini wameshindwakununua ving'amuzi! Maskini kama huyu wala time na hayo mnayoyatangazahana...., hana si kwa sababu hataki, hana time coz' hata hela yenyewe yakununulia hivyo vitu hana!! We ushaona vitenge vinatangazwa kwenye TV? Hizi ndionguo za akina sisi tusio na uwezo wa kununua ving'amuzi!! Hata ukitumia mwakamzima mfululizo kutangaza zile za Hussein Pamba Kali, achilia mbali zaWoolworth, huko hatuji!! Tuje kufanya nini wakati Tandika napafahamu?!

Hoja ya msingi ninayoina mimi labda hiyo yakuwanyima uhuru wa habari, lakini ya mapato, effect yake ni ndogo sana!Inawezekana ni kweli advertisers wamepunguza matangazo yao bila kufahamukwamba population ya bidhaa zao wala sio hii ambayo hata uwezo wa TZS 48,000/=hawana!!! Hamna mistake mbaya kwenye masuala ya masoko kama kutofahamu unamtangazia nani....!!!
 
Back
Top Bottom