Mfumo wa Digital: 'Local Channels' watoa kilio kwa serikali

Mfumo wa Digital: 'Local Channels' watoa kilio kwa serikali

Pasco upo ndugu yangu? sikia ndugu zako wakiongozwa na Mengi plus strategist Ruge!!
Nimewasikia kwa masikio yangu mwenyewe!, wakiongozwa na "Muzee wa Kulalamika!" the deal wanayoomba, its about making money na sio kuwapigania wananchi ile "haki ya kupata habari!".

Namhurumia Ruge na Nyala, maskini hawamshutukia, mwenye mali Diallo, alishashtuka siku nyingi, na kamwe hutakaa umoene in person kwenye hiyo kampuni inayoitwa "moat" ambayo ni " ka mradi fulani!".

Mzee wetu huyu anaelewa fika, kuwa digital migration sio suala la choice, its a must na halikuibukia TCRA wala serikali yetu bali limeibukia ITU, hili tishio la kufunga matangazo ni danganya toto tuu, ila kiukweli huu sasa ndio wakati wa vyombo hivi vya habari uchwala uchwala, just to pack and go, kwa mtindo wa "struggle for existence and survival for the fittest!". Ukiangalia ITV matangazo yapo kama kawa, tena nadhani yamezidi!, ila jamaa anashindwa kuilipia Capital TV kwenye vingamuzi vya maana zaidi ya ZUKU na Easy TV, hivyo kutafuta ubwete wa kuirudisha analogia ili aendelee kupeta!.

Kama hawa jamaa walikuwa na nia njema ya kuwahurumia Watanzania ile haki ya kupata habari, then Mzee Mengi, angekigawa bure hicho kingamuzi chake cha Digitek, na kwa vile chenyewe ni cha digital wakati hiki cha Star Time ni cha analogue, mtu angeona signal ya digital asinge thubutu tena kurudia "takataka" ya analogie!, hivyo Digitek ingepiga bao la kisigino kuwakomba watazamaji wote, na hivyo kukomba matangazo yote!.

Tena ili kuonesha anawajali sana wananchi, ITV ingerusha bure vipindi vya nje kama hivi ambavyo tunawapelekea, ili wananchi wapate habari zao na kuona vipindi zaidi vya logal contents na hili lingefanyika, mngeona hadi Isidingo zetu wenyewe na "soap" za Kiswahili!.

Naamini TCRA hawawezi kuufanya ujinga kama huu tena wakimjibu watakuwa wamemuheshimu sana, ningekuwa mimi ni TCRA, ninge muignore tuu kwa sababu majibu yote anayo in black and white, anataka kujifanya kulilia wananchi for public sympathy tuu andelee kuzimake!.

Pasco.
 
Mzee Mengi anasema hata Uingereza iliwachukua miaka 10 kuamua kuzima analogia!

Anadhani sababu ni umaskini wa Waingereza kushindwa kumudu gharama za ving'amuzi kama sababu anazotoa huku?

Suluhisho si kurudi analogia bali upatikanaji wa Ving'amuzi kwa gharama nafuu na local channel ziwe bure!

Mikoani tena huko ndani kabisa walianza kutumia ungo kitambo,mtu akizichanga kununua Tv anaweka na gharama za ungo na sababu kubwa ni hizi Tv zetu nyingi mwisho wake kibaha!

Hiyo Clouds tv mikoani wameijua kupitia digitali! tena sasa hv kupitia digitali ndio wanazipata hizi local channel tofauti na zamani ukiwa mikoani lazima uwe na ungo!
 
Watanzania walipo lalamika kukosa vipind vya television, haikuwauma na wala hamkujua kama katiba imekiukwa ila kwakuwa mnakosa mapato mmejua kama katiba imekiukwa.
So mnachojali nimaslahi yenu ss nasisi hatutaki. kwanza mmetupunguzia gharama za matumizi yasiyo ya lazima japo yanaumuhimu.
 
Kwa hiyo suala kumbe ni mapato au?

Sio mapato tu mambo ni mengi sana na the poorest of poor country tunajifanya kimbelembele ati kwenda na wakati.Ninawaunga mkono moat na Tunaiomba tcra ikubali mifumo yote mpaka hapo itakapofika deadline ya dunia nzima.Mbona kenya wamekataa na uganda.Tanzania tuna uwezo gani wa kufanya hivyo???????????
 
Pamoja na pasco kusema ukweli lakini je huko kijijini ni wangapi wenye ungo??.ITU wamesema mwisho ni 2015.Nchi maskini kama tz tunakimbilia nini.Hata cost inakuwa kubwa kwani studio zipo dar analog signal hawaoni lakini inarushwa kwenda mikoa mingine ambapo hawajazima analog kwanini wasilruhusu matangazo yote kwa pamoja ili itakapofika 2015 ndipo analog izimwe??
 
Mkuu jitahidi unapopost habari inayowagusa watu basi jitahidi uielewe ili kuepuka upotoshaji. Bwana mengi yeye aliishauri TCRA ingeruhusu mfumo wa analogia uendelee kwa maana huu mfumo wa digital unawanyima wananchi wengi ambao ni wenye kipato kidogo, haki yao ya kikatiba ya kupata kutokana na kukosa ela ya kununulia ving'amuzi.

Mwakilishi wa SAHARA Media yeye ndiye aliyezungumzia hasara inayotokana na mabadiliko haya ambapo ameeleza kuwa kutokana na kukosa watazamaji wengi kwasasa, hata matangazo ya biashara yamepungua kwasababu wanaotangaza biashara zao wanaona kwasasa matangazo hayo hayawafikii watu wengi kama ilivyokua hapo zamani. Hali hii imepelekea gharama za uendeshaji kuwa ngumu sana. Sijasikia hilo la kufungwa kwa local channel kwangu Binafsi.

Hapo kwenye blue,
Check vizuri kwenye article hii hapa toka IPP Media....
Media owners want analogue broadcasts back

By David Kisanga

12th March 2013

Say closing shop imminent if no action taken.
.
.
Dr Mengi, who is also IPP Executive Chairman, called on the government to assess the situation as soon as practicable so as to enable the entire citizens to access information freely as guaranteed by the country's Constitution.
Elaborating on how migration to digital broadcasting has affected television stations, he said advertisers now buy much less airtime than previously for fear that their advertisements would not reach as many viewers as expected since the switch has shut out many viewers.
"This might result in some local television stations ceasing to broadcast, eventually forcing them to close shop because the switch to digital technology has enormously eaten into their incomes," he noted.
He said Tanzanians should not be surprised when the time comes for some television stations to opt out of the broadcasting industry, warning: "That is where we are heading … If the government won't work on this issue immediately, some media owners will be left with no choice but to close down their television stations."

Source: :: IPPMEDIA
 
Kwa kweli wafunge tu ili serikali ijifunze sababu kuna channel tangia tuhamie hiyo wanaiita digitali cjawah Ziona kabisaa.
 
Mkuu jitahidi unapopost habari inayowagusa watu basi jitahidi uielewe ili kuepuka upotoshaji. Bwana mengi yeye aliishauri TCRA ingeruhusu mfumo wa analogia uendelee kwa maana huu mfumo wa digital unawanyima wananchi wengi ambao ni wenye kipato kidogo, haki yao ya kikatiba ya kupata kutokana na kukosa ela ya kununulia ving'amuzi.

Mwakilishi wa SAHARA Media yeye ndiye aliyezungumzia hasara inayotokana na mabadiliko haya ambapo ameeleza kuwa kutokana na kukosa watazamaji wengi kwasasa, hata matangazo ya biashara yamepungua kwasababu wanaotangaza biashara zao wanaona kwasasa matangazo hayo hayawafikii watu wengi kama ilivyokua hapo zamani. Hali hii imepelekea gharama za uendeshaji kuwa ngumu sana. Sijasikia hilo la kufungwa kwa local channel kwangu Binafsi.
Si unajua watu wanavyopenda promo so akisikia ushuzi yeye anaandika kanya. akili za mawenge
 
Nasema na narudia kusema mfumo wa digitali ni wa hovyo kuliko analogia ulimbukeni wa kupapatilia teknolojia. Kwangu hata LCD mwiko nitatumia tube tv mpaka kifo. Hakuna faida ni hasara tu.
Huyu anazungumzia "ulimbukeni". Nakumbuka mwaka 1982 wakatizinaanza daladala Dar es Salaam, mtu mmoja naye alisimama na kulaani ulimbukeni wa watu wanaopapatikia kulipa shilingi 5/= wakati UDA za shilingi 3/= zipo na akaapa kutopanda kamwe daladala. Dijitali ndo hiyo. Imefika, imeanza, na haitoondolewa kama ambavyo anolojia itaondolewa.
 
waache kukuza mambo,kama hao sahara media watatafuta mchawi wao kuwa hawapati matangazo huku startv imekuwa kama tv ya chama tawala!utafute mchawi eti ni TCRA?hao waathirika wa digital sana sana ni wakazi wa jiji la dsm,ambao walikuwa wana2mia antena kupata mawasiliano ya tv,lakini mikoani toka zamani wana2mia digital(dish,na cable)kupata matangazo,leo mtuaminishe kuwa eti ni haki ya kikatiba kupata habari?hata kabla ya mfumo huu ni wa tz wangapi wanapata hizo habari?hususani vijijini!semeni mfumo huu wa digital una waumiza ninyi ki biashara kwa kulipia hayo makampuni yanayo rusha matangazo yenu,kwani nyie mmebaki na kazi ya uzalishaji vipindi tu,na sio usambazaji wake,Ndio mnageuka na kujifanya mna huruma na mtanzania!Hata ruge naye alikuwepo naye anawasikitia wa tz kukosa haki ya habari!wakati wao ndio mashabiki wa mambo ya dhuruma wafanyiwao wa tz,kupitia radio yao clouds fm?LETENI HOJA NYINGINE 2 HIYO YA KITOTO.
 
startv ipo dstv chini ya tbc1 inaitwa star
 
Hivi kwanini digital isiwe ni mtu kuamua mwenyewe kama anataka aingie kama hataki apate analojia? mara picha,mara rangi!
 
Wamiliki wa vituo vya utangazaji vya televisheni nchini, wamesema watasitisha kurusha matangazo ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa kutokana na kushindwa kumudu gharama za uendeshaji. Hatua hiyo inatokana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzima mitambo ya analojia na kuhamia dijitali Desemba 31, mwaka jana kitendo walichodai kimepunguza mapato yanayotokana na
matangazo.

Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (Moat), Reginald Mengi alisema hakuna haja ya kurusha
matangazo kwa hasara. Mengi alisema kutokana na kuanza kwa mfumo wa dijitali, watangazaji wamesitisha kutoa matangazo kwa sababu wananchi wengi hawana ving'amuzi. "Kama mamlaka itashindwa kurudisha ule mfumo wa analojia kuwa sambamba na
dijitali hadi wananchi watakapokuwa na ving'amuzi, tutazima televisheni zetu ndani ya mwezi mmoja ujao," alisema Mengi. "Ibara ya 18 ya Katiba imekiukwa kutokana na wananchi kunyimwa fursa ya kupata habari, hivyo hali hii hatutaki iendelee," alisema Mengi.
Mengi ambaye pia ni mmiliki wa vituo vya televisheni vya ITV, EATV na Capital TV, alisema licha ya nchi za Afrika, Tanzania imekuwa ya kwanza kuzima mitambo ilhali wananchi hawakuwezeshwa kumudu gharama za ving'amuzi.

"Nchi ambazo zimeendelea kwa kila kitu kama Uingereza, Marekani, Japan na kwingineko kuzima mitambo ya analojia walitumia zaidi ya miaka minane kwa nini sisi tumewahi hivi wakati hatujajipanga?" alihoji Mengi.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Sahara Media Group na mmiliki wa Kituo cha Star Tv, Samwel Nyalla alisema hivi sasa wanaendesha biashara hiyo kwa hasara. Nyalla alisema hadi mwaka 2015, hali itakuwa mbaya kutokana na kukosa ving'amuzi. Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA, Habby Gunze alisema wao hawakualikwa katika mkutano huo hivyo hawajui chochote. Gunze alimtaka mwandishi kwenda ofisini leo.

"Sisi hatujui chochote na kama unataka maelezo mengine njoo kesho (leo) ofisini kwetu uonane na Mkurugenzi Mkuu (Profesa John Nkoma), ili tuzungumze kwa ‘fact' (kwa ushahidi) kipi kinachoendelea," alisema Gunze. Nukuu "Kama mamlaka itashindwa kurudisha ule mfumo wa analojia kuwa sambamba na dijitali hadi pale wananchi watakapokuwa na ving'amuzi tutazima televisheni zetu ndani
ya mwezi mmoja ujao labda TBC ndiyo itakayobaki".
 
Na watakuwa wamesaidia sana serikali maana naona lengo lao ni tuangalie Yombayomba TBC.

Na kuangalia usanii wa TBC badala ya uhalisia wa mambo yanavyotokea nchini.
 
Nitashangaa tukirudi nyuma. Ngoja nisubiri kauli ya TCRA/ Serkali
 
CCM wanataka mpaka 2015 kuwe hakuna analojia, ni njia ya kuwadhibiti wananchi wasipate habari.
Wameshaona wananchi wanaelewa sana mambo. Hivyo wanatafuta njia za kuwazibiti!
 
Na watakuwa wamesaidia sana serikali maana naona lengo lao ni tuangalie Yombayomba TBC.

Na kuangalia usanii wa TBC badala ya uhalisia wa mambo yanavyotokea nchini.

Nasikia eti ZE COMEDY ORIGINAL nayo inarusha matangazo tu. Wameshaacha kuchekesha na wanacheka wenyewe tu kwa kuigiza ukichaa kichaa????

Sijui Se.. yuko wapi?
 
kweli kabisa huu ni ushenzi na mpango wa ccm watu kukosa habari
 
kama kuna kitu kitaondoa hii serikali madarakani ni itv na star tv wakiacha kurusha matangazo
 
Back
Top Bottom