Tony Gwanco
JF-Expert Member
- Jan 22, 2013
- 5,913
- 1,219
Wamiliki wa vyombo vya habari, wao wametoa tamko kuitaka serikali kupitia TCRA kufungua mitambo ya analogia la sivyo watakata matangazo, wakiongozwa na mmiliki wa vyombo vya IPP ndg. R. Mengi. Wamedai kuwa tangu mfumo huu uanze wamekosa mapato!
"Katiba imekiukwa kutokana na wananchi wengi kunyimwa fursa ya kupata habari, hali hii hatutaki iendelee' amesema ndugu Reginald Mengi"
Dar es Salaam. Wamiliki wa vituo vya utangazaji vya televisheni nchini, wamesema watasitisha kurusha matangazo ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa kutokana na kushindwa kumudu gharama za uendeshaji.
Hatua hiyo inatokana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzima mitambo ya ANALOJIA na kuhamia dijitali Desemba 31, Mwaka jana' kitendo walichodai KIMEPUNGUZA MAPATO yanayotokana na matangazo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wamilki wa vyombo vya Habari Tanzania (Moat), Reginald Mengi alisema hakuna haja ya kurusha matangazo kwa hasara.
Mengi alisema kutokana na kuanza kwa mfumo wa dijitali, watangazaji wamesitisha kutoa matangazo kwa sababu wananchi wengi hawana ving'amuzi.
"Kama mamlaka itashindwa kurudisha ule mfumo wa analojia kuwa sambamba na dijitali hadi wananchi watakapokuwa na ving'amuzi, tutazima televisheni zetu ndani ya mwezi mmoja ujao" alisema Mengi.
Source: Mwananchi
Digital Broadcasting Regulations of 2011
MISCELLANEOUS PROVISIONS
17.-(1) There shall be the transition period for migration from analogue to digital broadcasting which shall commence on the 1st July, 2011 and end on 31st December, 2012.
(2) During the transition period, there shall be dual illumination (simulcast) period running from 1st July 2011 to 31st December 2012.
http://www.tcra.go.tz/regulation/digitalOtherBroadcastingNetworks.pdf read more.