Mkuu wangu Pasco, hapo kwenye blue ni jana tumejadili hoja yako ya namna gani Wa-TZ tunavyoshindwa kuwa creative enough!!! Unajua wala hapahitaji madegree ya biashara kufahamu kwenye suala zima la digitali, hapa biashara ipo kwenye subscription fee kuliko kwenye bei ya ving'amuzi! Kinga'amuzi unanunua mara moja tu, lakini fee ni kila mwezi...! So, kama ulivyosema, kwa mjanja angekuja na ving'amuzi akagawa hata bure na kama not economical, basi akawa mteja anamkata kidogokidogo kupitia subscription fee!Makampuni ya simu ya wenzetu wanatoa handset bure na kuzilipia ndani ya subscriptuion fee!. Ningekuwa mimi ndio Mengi, ningeleta ving'amuzi vyangu vya digitek, milioni 20!, na kuvigawa bure, huku nikiwakata kwenye subscription!, katika profile ya ITV, naeleza wazi katika taifa la watu milioni 45, watu milioni 20, wanaangalia ITV!, unadhani nani angeendelea kununua king'amuzi cha Star Time ambacho ni cha analoguie?!. Nani angeendelea kutangaza na TBC yenye horrible uninteresting programs?!.
Ifike mahali Mzee Mengi, apunguze kulia kulia lia na kumwaga "crocodile tears!", ukifuatilia trend yake, Mzee ni mliaji mzuri, toka kile kile cha "mchezo mchafu" wa Kilimanjaro hotel, kalia na Masilingi, Masilingi Chali!, Kalia na Masha, Masha chali!, kalia na Tido, Tido chali!, sasa anataka kulia na Prof. Nkoma, tena Prof, amemuheshimu sana kumjibu, otherwise, this time ana taka ku press the wrong button!.
Mark my words, mtaniambia!.
Pasco.
Hapo kwenye red, sincerely anakera....huyu mzee kwa kulia lia ndo mwenyewe! Hapo umetaja viongozi wa serikali tu, achilia mbali wafanya biashara wenzake!! Akianza na Dewj wa DTV hadi Manji!