Mfumo mpya wanatumia watu kutapeli watu

Captain mopao

Senior Member
Feb 25, 2021
133
379
Habari ndugu na jamaa naomba niwape story fupi, kama siku tatu nyuma nilienda mjini asubuhi nikafanya shughuli yangu nikageuka wakati nipo njiani nikakutana wadada wawili wamekaa mahali mmoja wao akaniita kwa ishara nikasogea mpaka mahali walipo mmoja akaanza kuongea na mimi, akanijulisha kua wao wanakaa gairo na wamepungukiwa nauli hivo wanaomba kias chochote kiwasidie.

Muonekano wao ulikua ni wanaonekana mi wadada wa mjini wamejichubua sana alafu mmoja wao alikua kambeba mtoto km wa miaka miwili ivi, the way walivokua na mtoto wanatia huruma sana nikawasaidia pesa kias wakanishukuru nikaondoka, jana nikawa naenda tena town kwenye mitikasi yangu nikakutana nao tena walewale wapo vile vile ila safari hii niliwakuta maeneo tofauti wakaniita kwa dizaini ile ile nikawaambia sina pesa dada zangu, sikutaka kuwaumbua pale na hii kitu imetokea kwangu mara mbili.

Mwaka jana kuna mdada nikikutana nae ana nae kabeba mtoto akaniambia ametoka tabora kuja kutafuta kaz akaniambia mwanae hajala tangu asubuh nikamsaidia pesa baada km ya week,, nikakutana nae tena

Hivi ina maana maisha yamekuwa magumu kiasi watu wanabuni mbinu za kutafuta pesa dah jibu sijapata ndugu zangu ndo mambo yalivyo kwa sasa hapa Dodoma
 
Yani saidia saidia za barabarani lazima ujikute unasaidia la mnywa gongo, anakupiga sound unampa hata buku, anaenda kulewa chakali kilabuni.
 
Uwe unaenda na pale Nyerere Square uone wanavyokuja omba omba wa kila aina! Kuanzia watoto, walemavu, wazee, mabaharia walio kamilika, nk.

Kiufupi hali mtaani imekua ni ahueni ya jana.
 
Hizo mjini zipo sana, mimi ilishatokea kama mara tatu Dar stend Mbezi mwisho. Nilikutana na Dogo kijana wa kiume kama miaka 15 aun 16 akiwa na amevaa uniform aka nisalimu shikamoo, baada ya hapo akanambia yeye anakaa Chanika lakini anasoma shule fulani iko kibamba au kiluvya inaitwa gogoni. Ombi lake lilikuwa nikuomba nauli kwa madai mzazi wake ni mgonjwa.

Nikampatia shilingi elfu 5 kwa kuwa sikuwa na chenji. Baada ya siku tatu nikakutana naye kaja na hoja ile ile lakini muda huo tayari ni muda ambao alipaswa kuwa darasani. Nikamwambia sina.

Wki moja baadae nikakutana naye ikabaidi siku hiyo nimbane ndo nikagundua yule dogo ama hasomi au anatumia sare za shule kujipatia kipato.
 
Siyo utapeli mpya upo sana, mtu na watoto anaomba nauli arudi Mwanza, Mtwara, wengi hudai wametelekezwa na wanaume, wanadaiwa kodi blah blah!
Mjini shule kijijini maguvu!

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Back
Top Bottom