Mfumo mbovu wa Airtel wasumbua wateja wa Airtel money

LUS0MYA

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
862
1,097
Imekuwa jambo la kawaida sasa ukifanya malipo ya huduma kama Luku au King'amuzi kupitia airtel money fedha hazifiki kwa wahusika na unapouliza wahudumu wa airtel wanajibu kirahisi kuwa kuna tatizo la kimtandao halafu watarusisha muamala ndani ya masaa 36.

MASWALI YA KUJIULIZA
1. Kwanini fedha itolewe kwenye akaunti kama kuna tatizo la mtandao?tulitegemea mfumo u reject muamala ili fedha ya mteja ibaki kwenye akaunti yake.

2. Msemo kuwa hela ipo hewani ina uhalisia gani?je kama kuna wafanyakazi wasio waaminifu hizi pesa zinaweza kuwa ni mabilioni haziwezi kuwekwa kwenye fixed account bila ridhaa ya wateja?
 
Wanazitumia kwa muda wa siku nne au tano au hata wiki kulipia madeni yao halafu baadae ndio wanarudisha
Kwahiyo tuandamane ili kila senti wailipie riba, tigo ndio wezi zaidi
bora tujiunge ttcl tumenzi magu
 
Back
Top Bottom