Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,161
- 10,877
Wakati duniani kote kuna harakati kubwa za maandamano ya wananchi wanaotaka mabadiliko ya utawala kwa nchi zao.Harakati hizi zinakwenda sambamba na mauwaji makubwa ya waandamanaji kutoka kwa watawala.Wapo ambao baada ya hasara wanazozipata wanafanikiwa kupata wanachokitaka.
Wale ambao hawajafanikiwa kuleta mabadiliko mara nyingi huwa ni sababu ya ukatili mkubwa wa walio madarakani ambao wengi wakishakukalia kiti huwa hawapendi kuondoshwa.
Baadhi ya madai ya waandamanji huwa ni ya msingi na muhimu kusikilizwa kwa namna fulani ikiwemo kujiuzulu kwa watawala.Hata hivyo mengi ya madai ya waandamanaji hao hayana msingi na ni fikra za kisehetani tu kuivuruga dunia.
Hali mojawapo ya kutoridhika kwa wananchi juu ya mifumo inayowatala ni kutokana na kukosa mahitajio muhimu ya kimaisha ikiwemo ya matumizi ya kila siku na hata amani. Wengine huwa wanaandamana kutaka makubwa zaidi ikiwemo uhuru uliopitiliza.
Tukiangalia mifumo ya kiutawala inayoongoza dunia kwa sasa ni mfumo wa kidemokrasia na ule wa ufalme.Tukichukulia kwamba mifumo yote miwili hiyo haijakuwa sababu ya dunia kupata utulivu na kwamba kila mmoja ya mifumo hiyo kwa mifano mbali mbali ina kasoro na ni kweli imekuwa sababu ya matatizo dunia inayoshuhudia kila uchao.
Kwa kuzingatia yale yanayotokea Iran,Marekani,Uiengereza,Tunisia,Sudan.Na yale yanayoendelea Venezuela,Colombia,Chile na kwengineko. Je, upo uwezekano wa kuleta mabadiliko kwenye mifumo hiyo ili kuifanya hali ya dunia iwe shwari ?,na kama haiwezekani.Jee kuna mfumo mwengine wowote utakaofaa kuitawala dunia?.