Mfumo dume utaimaliza CHADEMA

Mfumo dume utaimaliza CHADEMA

lord atkin

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2018
Posts
205
Reaction score
769
Wengi tunaamini kinachowafanya chadema wafikirie kususia ubunge au hata kuwasakama akina mdee siyo uchaguzi kutokuwa huru na wa haki bali ni mfumo dume ndani ya chama chetu hiki.

Uchaguzi nchi hii haujawahi kuwa huru na wa haki, lakini hatujawahi kususia Ubunge na Udiwani. Mwaka 2010 tulikataa kumtambua Rais na kumtangaza Slaa kuwa Rais wa mioyo yetu kwa kuwa tuliibiwa kura siyo za Urais tu hata Ubunge katika Majimbo mengi, majimbo mengi tuliyotangazwa mwaka wa 2010 ni yale wananchi walitumia nguvu ya umma kuyadai, hata hivyo hatukususia ubunge. 2015 vivyo tulitoka mpaka bungeni jpm akihutubia lakini ubunge tuliendelea nao.

Je, tulihalalisha haramu? Leo hii tunasusa kwa Grace? Hatuwaamini kwamba wataweza kututetea? Wabunge 20 siyo wachache 2005 CHADEMA ilikuwa na wabunge 11 kina Zitto, Slaa, Mdee, Chacha Wangwe n.k na walifanya makubwa, waliibua ufisadi mkubwa sana wakainusuru nchi.

Wengi tunaamini viti maalumu vingekuwa vya wanaume majina ya kina Mbowe, Mnyika, Lissu, Msigwa yangeshafika Bungeni zamani. Au Lissu angeshinda Urais halafu tudhulumiwe Wabunge wengi tusingesusa Urais.

Kususa hakujawahi kuwa suluhisho maalim Seif alisusa Zanzibar hakuna kilichobadilika zaidi ya chama chake cha CIF kufa mnataka CHADEMA ife, mkitaka ife basi tumieni jazba na mihemko kutatua mgogoro huu wa viti maalum.

Tafadhari mbowe tumia busara Period.
 
Hao wakiingia bungeni wanawazuia vipi kufanya siasa, au misimamo yao kuhusu uchaguzi, lazima chama kama chama kijiamini.
 
Back
Top Bottom