Mfugale awavimbia Waziri Mkuu na Waziri wa Ujenzi kwa kivuli cha Rais Magufuli?

Mi naona kuna tatizo kubwa zaidi kwanza kumekuwa na maagizo yanayotolewa kuwa ondoa mtu fulani pale au pale wakati huyo mtu kiutendaji haripoti kwa huyo anayeelekeza aomdolewe.

Utaratibu mtu kama utendaji wake una mapungufu yanaonekana na boss wake anayemsimamia sasa anapotokea kiongozi wa juu anaruka wasimamizi anakwenda kuondoa mtu ambaye siyo yeye anayemsimamia haieleweki ametumia utawalam gani kuona mapungufu ya mtu ambaye hasimamiwi na yeye na hivyo kuwajengea hofu watendaji wa chini bila sababu.
I say wewe huelewi kabisa haya mambo! Yaani waziri Mkuu asimwajibishe mtu kwa kuwa sio yeye anamsimamia! Ni sawa na kusema Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hawezi kumfukuza kazi mlinzi aliemkuta anaiba kwa kuwa mlinzi halipoti kwa Mkurugenzi Mkuu!
 
Wewe unachonganisha, Waziri Mkuu alieleweshwa na akeelewa vizuri. Mhandisi alibaki pale kama Bridge Engineer na siyo Regional Manager, kulikuwa na uhitaji wa haraka ndio maana alibaki.
Hivyo ndivyo alivyojibu Mfugale au ndivyo unavyotaka Mfugale angejibu? Kwa hiyo kuna meneja mpya wa Tanroads Mororgoro sio Andalwisye? Na Mfugale hawezi kujieleza kwamba Andalwisye ameletwa site kama engineer lakini alishaondolewa kama meneja wa Tanroads Mororgoro? Na Tanroads nzima ina Andalwisye tu kama injinia wa kujenga daraja rahisi kama hili lililovunjika? Haya madaraja yakivunjika mikoa mingine ni Andalwisye anaenda huko?

Hivi unamfanya Wazirir Mkuu hana uwezo wa kufikiri?
 
Sidhani kama Majaliwa atasahau hili. Akija kuwa raisi kitu cha kwanza ni kubadilisha jina la flyover ya Tazara. Na usisahau kwamba Majaliwa alikuwa na moto sana mwanzoni, siku moja akazimwa hadharani na raisi na kuambiwa hata yeye anaweza kutumbuliwa kama wengine. Hiyo ilimnyamazisha sana Majaliwa.

Lakini tambua kwamba Magufuli anajua hilo. Sio rahisi Majaliwa kuja kuwa raisi katika mazingira kama hayo.
Katika Historia ya Tanzania, amewahi kutokea PM au WM, kuweza kuwa Raisi.
Tuanze na:
1.Msuya
2. MALECHELA
3. SALIM AHMED SALIM
4. LOWASSA
5. PINDA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ibanezafrica,
Amri ni amri Mkuu. Wangapi wametumbuliwa na Magufuli kwa kuonewa, sembuse huyu Andalwisye ambaye sio daraja tu, bali kunakuwa na mashimo makubwa katika barabara za eneo lake ambayo hayashughulikiwa na hata yanasababisha ajali zinazoua watu na kuharibu mali za watu.

Waziri Mkuu alikuwa right kabisa kusema aondolewa. Tena ali[paswa kutumbuliwa, nilishaandika sana humu JF kuhusu uzembe wa Tanroads kuacha mashimo makubwa barabarani kwa muda mrefu na kusababisha ajali zenye kuleta vifo wakati pesa ya kurekebisha barabara tunatoa kupitia kununua mafuta
 
Hakukuwa na haja ya kumwondoa huyo meneja, kwani serikali inafahamu fika hiyo barabara inahitaji matengenezo upya kwasababu ya umri na pia imechoka, hata wangepeleka report ya ukaguzi unaweza kuta wangeambiwa wangoje, kwani miradi mingapi ipo kwenye foleni.

Mambo mengine yakitokea watu hapata sehemu ya kutafutia sababu hata kama hazina mashiko.
 
msisahau kua Mfugale kama bosi wa TANROAD anayo mamlaka ya kumteua mtu yeyote mwenye utaalamu kushughulikia Sight Fulani kwa hiyo PM hakupaswa kuuliza uwepo wa mtaalamu sight bali angeuliza ucheo wa huyo mtaalamu na ofisi mambo ya sight mwachie mtaalamu wewe angalia end result tu.
 
Hakukuwa na haja ya kumwondoa huyo meneja, kwani serikali inafahamu fika hiyo barabara inahitaji matengenezo upya kwasababu ya umri na pia imechoka, hata wangepeleka report ya ukaguzi unaweza kuta wangeambiwa wangoje, kwani miradi mingapi ipo kwenye foleni.Mambo mengine yakitokea watu hapata sehemu ya kutafutia sababu hata kama hazina mashiko.

Taarifa ni kwamba daraja lilizibwa na matakataka na ndio maana maji yakatafuta njia mbadala na kula kingo na hatimae daraja kubomoka. Hicho ndicho Majaliwa aliita uzembe, sio daraja kuwa limezeeka. Unajua lifetime ya daraja lililojengwa hadi useme lilichoka?
 
Fitina na mambo ya hovyo hovyo vimezidi sana huko maofisini hadi wataalamu wanaonekana hawana maana, kumwondoa regional engineer mbele ya kamera ni sawasawa na kumdhalilisha huyo mtaalamu
 
msisahau kua Mfugale kama bosi wa TANROAD anayo mamlaka ya kumteua mtu yeyote mwenye utaalamu kushughulikia Sight Fulani kwa hiyo PM hakupaswa kuuliza uwepo wa mtaalamu sight bali angeuliza ucheo wa huyo mtaalamu na ofisi mambo ya sight mwachie mtaalamu wewe angalia end result tu.
Acha kuzungusha maneno. Ingekuwa ndivyo Mfugale angeshajibu kuwa amehamishwa kutoka Morogoro karudishwa site tu kutoka wizarani
 
Taarifa ni kwamba daraja lilizibwa na matakataka na ndio maana maji yakatafuta njia mbadala na kula kingo na hatimae daraja kubomoka. Hicho nicho Majaliwa aliita uzembe, sio daraja kuwa limezeeka. Unajua lifetime ya daraja lililojengwa hadi useme lilichoka?

Nimekusamehe wewe na meneja wa Tanroads mkoa wa morogoro kwa uzembe.
 
Acha kuzungusha maneno. Ingekuwa ndivyo Mfugale angeshajibu kuwa amehamishwa kutoka Morogoro karudishwa sight tu kutoka wizarani
Ya nini yote hayo wakati watu wapo kazini kwa nini PM aongelee kwenye CAMERA wakati kuna ofisi, kwa nini asimwite mfugale Ofisini kwake ndio maana mtu anampa makavu wanapenda mno CAMERA uongozi hauko hivyo.Kumbuka cinema ya presider na mhandisi na yule mzee wa TBA
 
Fitina na mambo ya hovyo hovyo vimezidi sana huko maofisini hadi wataalamu wanaonekana hawana maana, kumwondoa regional engineer mbele ya kamera ni sawasawa na kumdhalilisha huyo mtaalamu
Fanya mpango ujumbe huu umfikie Raisi Magufuli kwanza. Tukiafanikiwa hapo tutafanikiwa kote
 
Ya nini yote hayo wakati watu wapo kazini kwa nini PM aongelee kwenye CAMERA wakati kuna ofisi, kwa nini asimwite mfugale Ofisini kwake ndio maana mtu anampa makavu wanapenda mno CAMERA uongozi hauko hivyo.Kumbuka cinema ya presider na mhandisi na yule mzee wa TBA
Sawa, kama Waziri Mkuu alikosea kitu gai kinampa Mfugale haki ya kukosea kwa kuwa Waziri Mkuu alikosea? Protokali haiendi hivyo. Fanya hivyo kwa meneja wako uone utaishia wapi.
 
Back
Top Bottom