Mfanyakazi wa kike aliniharibia kazi. Nimfanye nini?

Mfanyakazi wa kike aliniharibia kazi. Nimfanye nini?

''If you know you have been forgiven, it is that forgiveness that will create in you a forgiving heart towards others.
When we love our enemies and pray for those who persecute us, this releases us from the destructive emotions of anger, bitterness, revenge and others. Like Christ, you should be more concerned about your offenders and their relationship with God and less about nursing your own grudges and self-pity. Remember, the person most hurt by unforgiveness is YOU!''
Prophet T. B Joshua
 
Huyo binti ruka nae tu kwa manufaa ya vizazi vijavyo maana ukimuacha atapata kichwa na anaweza kurudia kumfanyia hivyo mtu mwingine akijua wanaume ndivyo tuliyo tutapotezea..

Mimi nakushauri mfanyie kitu ambacho hatasahau lakini lisiwe kosa kisheria ambalo litakuweka ndani..



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu heshima kwenu,

Mimi ni kijana mwenye miaka 27, nilimaliza shahada ya kwanza katika moja ya chuo kikuu maarufu Tanzania mwaka 2013.

Mwaka 2014 niliajiriwa katika shirika moja nyeti la umma lenye matawi mikoa yote.

Ni hivi, mwaka uliofuata aliajiriwa binti mmoja wa kawaida tu na mimi ndiyo nikampokea ktk mkoa niliokuwa nafanya kazi. Yule binti alianza mahusiano ya siri ya mapenzi ya haraka na Supervisor wetu bila mimi kujua (kwa mujibu wa rafiki yake wa kike ambaye ni mfanyakazi mwenzetu).

Huyu supervisor ni mtu mzima haswa na ameoa na ana watoto 5.

Pia, yule binti alikuwa na mazoea ya karibu na mimi yasiyo ya mapenzi.

Sasa siku moja akaniomba nimpe kampani ya dinner na kwa kuwa mimi sijaoa na mara nyingi huwa nakula mgahawani nikaona siyo mbaya.

Kiukweli mara kadhaa yule binti alilalamika kutofurahia mazingira ya kazi na aliniomba kama naweza nimfanyie mpango wa kuhama lakini mimi nikamueleza wazi kuwa sina uwezo labda amcheki Supervisor

Kwa hiyo siku hiyo ya dinner akanieleza kuwa amemwomba Supervisor amsaidie amemuahidi atamsaidia na atahama.

Siku hiyohyo wakati tunaendelea na dinner akapigiwa sm na Supervisor akaulizwa uko wapi akasema yuko na (mimi) tunapata dinner. Akakata simu mara moja.

Hiyo ilikuwa Jumamosi.Baada ya dinner akanambia hajisikii kurudi mapema hivyo kama kuna sehemu ya kusikiliza muziki hivi tukapoteze mda. Nikasema hamna shida. Tukaenda kwenye lounge moja hivi na ilipofika saa 5 usiku nikamwambia tuondoke.

Tukiwa njiani nikimsindikiza anapokaa ili nimwache halafu mimi niende home ghafla tulivamiwa na wanaume 5 wenye silaha ambapo walianza kutushambulia mimi na yule binti wakachukua simu zetu zote.

Kesho yake tulitoa taarifa polisi tukapewa RB tukaenda kupata matibabu

Nilimpa taarifa Supervisor wetu lakin hakuonesha ushirikiano wowote ule.

Kuanzia hapo Supervisor akaanza kunichukia na kutoonesha ushirikiano na mimi huku wakiendelea kuwa close na binti yule.

Siku moja rafiki wa karibu wa yule binti alinieleza kuwa Supervisor na binti yule wana mpango wa siri wa kufanikisha binti ahame lakini kwa kuniharibia mimi. Hakunieleza kinagaubaga kivipi.

Baada ya mwezi mmoja binti aliandika barua ya kuacha kazi ambapo baada ya mwezi mmoja tena mimi nikaandikiwa barua ya kuachishwa kazi kutoka makao makuu.

Nilifuatilia nijue A to Z ya sababu ya kuachishwa kwangu kazi kwa mujibu wa kiongozi mmoja mwandamizi akanieleza kuwa YULE BINTI alikuja hapa kulalamika kwa mwajiri kuwa UMEMBAKA SIKU MLIYOENDA DINNER na hata Supervisor wako alivyoita alichomekea mambo mengi kuwa hauna nidhamu, hujui kazi, ni mbishi, n. k. hata hivyo akanambia hyo ni siri na niwe makini na amenambia hilo kwa kuwa yeye hajapendezwa nacho na ananifahamu vzuri historia yangu kazini ila hakuwa na uwezo wa kubadilisha maamuzi ya mwajiri.

Kwa mujibu wa rafiki wa binti amesema kuwa hiyo mbinu alifundishwa na Supervisor kuwa aache kazi ili akiulizwa kwanini anaacha aeleze kuwa mimi niimbaka hivyo anajisikia aibu hawezi kuendelea na kazi (ili aweze kuhama).

Baada wiki kadhaa yule binti alihamishiwa mkoa mwingne (karibu na kwao) lakini mimi nikaambulia kulimwa barua ya kufukuzwa kazi kwa utovu wa nidhamu (bila hata kushirikishwa)

Mara kadhaa nimefatilia kulalamika ili nirudishwe kazini bila mafanikio yoyote.

Nikaamua kumwachia Mungu na kufanya shughuli zangu binafsi (biashara) na baadaye nikafanikiwa kupata scholarship Marekani ambapo hadi sasa nipo huku na mwakani Mungu akipenda namaliza shahada ya Uzamiri na nitarudi Tanzania kuendelea na maisha yangu.

Lakini wakuu mimi mara kadhaa kumbukumbu za ukatili niliofanyiwa zinanijia mara kwa mara kiasi kwamba inakuja roho ya kulipiza kisasi.

Kwa sasa yule binti nimepata taarifa kwamba amehamishiwa Dar kwa kuwa aliolewa na mfanyakazi mwenzake ambaye anafanya kazi makao makuu.

Kwa kumwogopa Mungu (na nipo tayari kuwajibika mbele za Mungu) naapa kuwa SIJAWAHI KUFIKIRIA KUWA NA MAHUSIANO NA BINTI YULE NA WALA SIJAWAHI HATA KUMTONGOZA. NILIMHESHIMU KAMA MFANYAKAZI MWENZANGU NA NILIMSAIDIA NA KUMSHAURI KWA KADRI YA UWEZO WANGU ILI AWEZE KUHIMILI MAZINGIRA YA KAZI NA ASIJISIKIE MPWEKE.

Kama nilivyoeleza hapo juu, roho ya kulipiza kisasi inanijia mara kwa mara kila napokumbuka mema niliyomfanyia binti yule (ambayo sijayaeleza hapa) kulinganisha na ubaya alionilipa kwa maslahi binafsi.

JE, MNANISHAURI NICHUKUE HATUA GANI? MUNGU AWABARIKI WOTE MTAKANISHAURI. ASANTENI.

Sent using Jamii Forums mobile app

ungemtaja hata jina ili mumewe ajue anakaa na kibwengo,kama ameweza kuframe njama ya kukuharibia maisha atashindwa nini kumdhuru mumewe anayemjua madhaifu yake?
 
Back
Top Bottom