TANZIA Mfanyakazi wa CRDB afariki akifanya mazoezi Daraja la Tanzanite

TANZIA Mfanyakazi wa CRDB afariki akifanya mazoezi Daraja la Tanzanite

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Mfanyakazi wa benki ya CRDB, Stanley Josiah amefariki dunia akiwa anafanya mazoezi kwenye Daraja la Tanzanite.

Taarifa za kifo chake hicho zimethibitishwa leo Jumamosi Juni 14,2025 na Mkurugenzi wa Mawasiliano

Benki ya CRDB, Tully Mwambapa, alipozungumza na Mwananchi Didital.

Tully amesema mpaka mauti yanamkuta, Josiah alikuwa mkuu wa kitengo cha operesheni za mikopo Benki ya CRDB.

"Benki imepoteza mtu mahiri sana hivyo menejimenti na wafanyakazi inaungana na familia yake katika safari hii ya mwisho," amesema Mwambapa ambaye ameeleza kuwa msiba upo nyumbani kwa marehemu, Tabata Kinyerezi.

"Benki inashirikiana na familia tangu taarifa ya ajali ilipotokea hadi sasa kufanya maandalizi yote muhimu hadi siku ya kumpumzisha mwenzetu kwa taratibu tulizojiwekea kama benki," amesema na kuongeza kuwa, mwili wa marehemu unatarajiwa kupumzishwa Jumanne ijayo Juni 17, 2025 nyumbani kwako huko mkoani Mbeya.

Hata hivyo taarifa ambazo Mwananchi imezipata, zinasema alifika asubuhi mapema ofisini na kuacha gari yake ofisini kwa ajili ya kwenda kufanya mazoezi ya kukimbia.

Chanzo hicho cha habari kinasema, mara nyingi hufanya hivyo kila siku asubuhi.
IMG_5168.jpeg
 
Hivi kabla sijaanza mazoezi inabidi nimcheki dokta?
Muhimu sana kucheki pressure. Kufanya jogging sio jambo la lazima kwa kila mtu kulifanya muda mwingine ni vema kufanya mazoezi ya viungoa madogo madogo kama kustrech then unafocus na maswala ya chakula tu. Muhimu ni kubalance diet yako mazoezi si lazima kukimbia hata kutembea ni mazoezi mazuri sana.
 
Watu wanakimbiakjmbia bila mpangilio,maZoezi ni kama yamevaniwa sahvi

Anyway poleni

Ova
Wengine wana cardiomegaly, AKI na mapresha ya juu sana. Wengine utakuta usiku alikua amekula mitungi mikali sana ana hang over lakini utawakuta wanakimbizana barabarani.

Hata wacheza mpira kabla ya kufanya mazoezi au kusajiliwa lazima wafanye vipimo kadhaa kujiridhisha kama afya zao zinaweza kumudu mazoezi magumu.

Sasa wabongo ndio tunafanya mazoezi kufata mkumbo mwisho wa siku kifo kikitokea tunasema mipango ya Mungu.
 
Angekata moto akiwa anapambana na lishangazi lodge yangekuwa maneno; na kingekuwa kifo cha aibu. Kwa kumwangalia yuko above 50 na katika umri huo ishu za presha, magonjwa ya moyo, kisukari na cholesterol ni kawaida tu. Na ubaya ni kwamba unaweza kuwa na ishu hizi na usijue. Ndiyo maana ni muhimu sana kabla hujaanza program yo yote ya mazoezi na hata serious dieting kufanyiwa uchunguzi wa kitaalamu ili kujua kama moyo wako uko salama pamoja na presha.

Anyway. Kaumaliza mwendo tena akifanya kitu alichodhani kwamba kingemwongezea siku za kuishi. Apumzike salama 🙏🏿🙏🏿🙏🏿
 
Tukiachana na sababu za kifo cha marehemu!!

Kuna kipindi nilianza mchaka mchaka alifajiri!
siku hiyo ya kwanza nilikimbia speed sn km kilometer 1, oor kusimama hv kizungu zungu kikali, macho giza nikaona maruweruwe, huku moyo kama unataka pasuka, nikalala chini nikihisi kufa huku nikihema kwa taabu sana😁😁

Itoshe kusema kwamba nilirudi home na toyo!
wacha niendelee na afya yangu, mwili utajiset wenyewe tu 🙏
 
Back
Top Bottom