Half american
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 45,122
- 111,813
Dah!Mfanyabiashara wa utalii ajinyonga Moshi
Azizi Msuya (39), mkazi wa Sambarai, Moshi, amekutwa amefariki dunia nyumbani kwake Alhamisi, Oktoba 2, 2025, akidaiwa kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limethibitisha tukio hilo na kueleza kuwa uchunguzi wa awali umehusisha msongo wa mawazo uliotokana na madeni aliyokuwa akikabiliana nayo.
Msuya alikuwa akijihusisha na biashara ya kusafirisha watalii. Uchunguzi zaidi unaendelea.View attachment 3482567
Mwamba kaumaliza mwendo inasikitisha sana.Dah!
Sana mkuu, usione mtu ana pesa na maisha mazuri mambo ni mengi, huyu mwamba nilikua namjua. Nawaza kwa nini asingeuza baadhi ya mali zake alipe madeni kama chanzo ni hicho.Madeni yanaumiza sana
Sana mkuuInasikitisha sana
Msongo wa mawazo mkuu kwani ni ndugu hawa?Hawa wakina msuya sjui wanashida gani?
Ni miezi mitatu imeisha toka daktari bigwa wa watoto katika hospital ya kibosho ajinyonge kisa msongo wa mawazo.
Umaskini unatisha kuliko kifoNawaza kwa nini asingeuza baadhi ya mali zake alipe madeni kama chanzo ni hicho.
sikijui kifo ila umasikini ni hatari inayopelekea kifo.Umaskini unatisha kuliko kifo
Inasikitisha mno na watoto wake bado wadogo sana, hii mikopo ni hatari kwa afya. Kwa umri wake na mafanikio aliyokuwa nayo alikuwa ananiinspire sana.Inasikitisha sana. Unaacha familia iteseke unajinyonga kisa madeni. Nchi inadaiwa na haijinyongi
Aiseeee. Somo ni kutotamani mali ya mtu mwingine maana hujui mtu huyo hizo mali kazipata vipi au anapitia changamoto gani ili awe na mali hizoInasikitisha mno na watoto wake bado wadogo sana, hii mikopo ni hatari kwa afya. Kwa umri wake na mafanikio aliyokuwa nayo alikuwa ananiinspire sana.
Kweli kabisa marehem alikuwa akiishi maisha fulani hivi ya ndoto za vijana wengi, utajiri ni siri.Aiseeee. Somo ni kutotamani mali ya mtu mwingine maana hujui mtu huyo hizo mali kazipata vipi au anapitia changamoto gani ili awe na mali hizo
Siijui ac yake.Account yake insta tuweke R.I.P zetu inatosha. Ila awamu hii mzunguko wa hela mtaani na kubiashara ni taiti isivyo kawaida, wengi wasipojipa ujasiri wa kuvuka inakuwa kama huyu
Mkuu uko sahihi kabisa. Mambo yakizidi dawa yake ni kuuza baadhi ya vitu na kulipa madeni. Matajiri hawalali kisa madeni.... kuna baadhi utakuta ni kama wanawafanyia kazi mabenki maana wameshakabidhi hati zote za nyumba na ardhi pamoja na kadi za magari. Shida inakuja ni ile mtu anaogopa aibu watu kumsema amefilisika.Sana mkuu, usione mtu ana pesa na maisha mazuri mambo ni mengi, huyu mwamba nilikua namjua. Nawaza kwa nini asingeuza baadhi ya mali zake alipe madeni kama chanzo ni hicho.