Mfanyabiashara Monaban alia Mali zake kuhujumiwa

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Mfanyabiashara maarufu jijini Arusha,Philemon Mollel (Monaban)amelalamikia hatua ya baadhi ya Mali zake zilizoko katika Kiwanda cha kusagisha nafaka cha NMC kuanza kuhujumiwa na kuuzwa mitaani kinyume na utaratibu.


Mollel ametoa kilio hicho wakati akiongea na waandishi wa habari Mara baada ya kukamata mifuko ya vifungashio zaidi ya 1,000,000 aliyokua ameagiza kutoka ndani na nje ya nchi na mingine aliyozalisha katika kiwanda hicho kabla ya Serikali kumpokonya ikiwa inauzwa mtaani na wafanyabiashara wadogo.


Pia Mollel ameingiwa na wasiwasi kuhusiana na Mali zakr zingine alizoacha kiwandani hapo yakiwemo Mahindi,Mtama ,Ngano na Vipuri na spare za Machine ambazo zipo ndani ya kiwanda hicho wakati akisubiri shauri la maridhiano baina yake na Bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko lililopo mahakamani.


"Nimesikitishwa kuona Mali zangu zikihujumiwa na sielewi Nani anahusika kuzitoa kiwandani hapo huu ni uonevu mkubwa na unania mbaya ya kunidhoofisha kibiashara" amesema Mollel


Amesema kuwa hatua hiyo ilimlazimu kuingia mtaani kufanya msako kwenye masoko akiwa na askari polisi na kufanikiwa kuwakamata vijana wapatao 13 wanayoisambaza mtaani wakiwemo wauza chipsi wanaoitumia kufungashia chips wateja wao.


Mfanyabiashara huyo amesema kuwa Mara baada ya serikali kumpokonya Kiwanda hicho na kuikabidhi Bodi ya Nafaka na mazao mchanganyiko aliacha Mali nyingi alizokuwa amezalisha ambazo kimsingi hazihusiani na mgogoro wake na Bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko,lakini ameshangaa kuona Mali hizo zikizagaa mtaani.


Amesema shauri la mgogoro huo bado lipo mahakamani na wanasubiri uamuzi wa Mahakama kuhusu mkataba wake was uoangaji katika kiwanda hicho pamoja na Mali zake lakini ameshangazwa kuona Mali hizo zikiuzwa na wamachinga mtaani.


"Nasikitika kuona Mali zangu zikihujumiwa wakati jambo hili bado lipo mahakamani ,naiomba Serikali isaidie Mali zangu zisije zikapotea " Amesema Mollel.


Molel ameiomba Serikali kupitia Vyombo Vya dola kuchunguza kwa makini jambo hilo na kuwachukulia hatua waliohusika kutoa Mali hizo kiwandani na kuziuza nje kinyume na utaratibu.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ,Jonathan Shana amesema jambo hilo lipo katika hatua za uchunguzi ili kubaini wahusika halisi wa tukio hilo.

Na pindi upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.


Ends...





IMG_20191228_135528.jpeg
IMG-20191227-WA0004.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ndio uhujumu uchumi.
Watu wanamzuwia mfanyabiashara kufanya uzalishaji na malighafi zake zinaonekana kuzagaa mitaani wakati zipo chini ya mikono ya wenye mamlaka fulani.

Mambo kama haya maendeleo tutayasikia tu.
Kama ni kupigwa faini au kupewa onyo ifanyike na aruhusiwe na uzalishaji. Anasaidia kupunguza tatizo kubwa la ajira na pia anazalisha chakula cha mifugo, jambo kubwa zaidi kuna uwezekano wa bidhaa zake kuvuka nchi jirani kirahisi.

I wish wakubwa kama waziri na Mh.Raisi waone hii habari.
Viwanda vingi vimehujumiwa kwa mtindo huu, sijuwi uchumi wa viwanda tutaufikiaje?!!
 
Back
Top Bottom