Mfanyabiashara bilionea Dar es Salaam, adai kutishiwa maisha, akimbia kwa pikipiki kutoroka asiuawe hadi Arusha

Arudushe kibunda Cha watu aache janjajanja hizo pesa zitamtokea puani
Suala inaweza lisiwe ni kurudisha tuu bali ni kuvunja mkataba. Ukinipa oda yako na ukatuma advansi ina maana na mimi nitaanza maandazi ya manunuzi, ambayo pia ni gharama. Sasa ukiibuka na kusema sihitaji tena huduma hapo lazima muangalie gharama ambazo tayari mimi nimeingia. Imagine ukikata tiketi ya Bus tuu, achilia ya ndege, halafu baadae ukaja kusema nimeahirisha safari basi ujue pesa yako itakatwa.
 
Usinifanye unaijua sana sheria mkuu, hata mimi naijua pia.
Hapa kwenye hili tukio la huyu mfanya biashara option alionayo ni kuchagua uhai/uhuru ama lolote kumtokea.
Yaani anacho kifanya kwa sasa ni kushindana na walio mzidi nguvu kwasababu anatafuta haki. Wakati mwingine tunapaswa kukubali kupoteza pesa na mali ili kunusuru nafsi zetu mkuu.
Na usisahau kwamba awamu hii mwenye nguvu ndio anahaki
Sasa kama wewe ni mnyonge na una give up easily wengine hawako hivyo mkuu, kuna biashara ambazo ili ufanikiwe ni lazima na wewe uwe mafia kidogo.. Hata hii mbinu ya kukimbia na kuiweka public inaonyesha jinsi huyo jamaa alivyo ngangari kwenye biashara. Ikiwa kila ukibanwa kidogo unarudisha pesa basi jua utafilisika chap chap
 
Hizi kesi za utapeli many times ni kwa wachagga tu tunaziona japo sina hakika mtuhumiwa ni tapeli,

So, huwezi ukasikia wasukuma wenzangu au watu wa pwani n.k, mara nyingi ni watu wakaskazini tunasikia japo sio wote, yule mushi nae kamdhulumu yule mama kiwanja na kujenga, na ndani amepangisha watu, na serikali kuamua ibomolewe arudishiwe haki yake yule mama aliedhulumiwa kiwanja. Pole sana mama, haki ya mtu haipotei

Jamani wakina Mushi ambao mnatabia za kutapeli na kuwadhulumu watu fanyeni biashara kihalali, huko Dar kwa wajanja hampawezi, huko sio Ngaramtoni, mromboo au kwa sakina mtakufaa.
 
Yaani bilionea anahangaika kulipa 129M kweli hongo kila mfanyabiashara ni bilionea.
Bongo tunakuza sana mambo.

Tanzania mtu akimiliki m100 utasikia oh yule ni milionea bwana, sasa kama huyo mushi wanasema ni bilionea, je wakina Bakhresa na GSM tusemeje! 😄 wakati huku kwetu kanda ya ziwa kuna watu wana hela na hawajionyeshi.
 
Mfanyabiashara maarufu wa Magari Jijini Dar es Salaam, Samweli Shami maarufu Bilionea Shami, amedai kutishiwa maisha na watu aliodai ni vigogo wa polisi jijini humo na kulazimika kuyakimbia makazi yake kutoka dar akitumia usafiri wa pikipiki na kukimbilia jijini Arusha.

Akiongea na vyombo vya habari jijini Arusha, Bilionea Shami ambaye anamiliki kampuni ya magari ya Ongezeko Trading Co ltd,alisema amelazimika kuishi kama digidigi kwa takribani mwezi mmoja kuwakimbia polisi waliokuwa wakimsaka kwa madai kwamba wametumwa na kigogo wa serikali.

Alidai kupigiwa simu na Kamanda wa polisi kanda maalumu ya dar es salaam, Muliro Jumanne Muliro akimtaka kurejesha kiasi cha sh milioni 129 alizopokea kama Malipo ya awali kwenye mkataba wa sh milioni 958 waliokubaliana kuiuzia malori 9 ya mtumba yenye tela zake ,kampuni ya Afrinexus Logistics ltd ya mjini Mtwara baada ya kampuni hiyo kuvunja mkataba kinyume na utaratibu.

Shami alisema kampuni yake ya Ongezeko Trading co Ltd ya jijini dar es salaam, iliingia makubaliano hayo September 12, 2023 ya kuiuzia malori kampuni hiyo ya Afrinexus Logistics kwa makubaliano kwamba baada ya siku 21 za kazi malori hayo yangeingia nchini kutoka China.
Alisema baada ya makubaliano hayo, kampuni ya Afrinexus Logistics ilianza kuingiza fedha kidogo kidogo kwa awamu 6 kwenye akaunti yake ambapo siku ya kwanza aliingiziwa sh milioni 27.2,siku inayofuata sh mil 25.5, sh milioni 16.15, sh milioni 29.57, sh milioni 5.1, na sh milioni 25.5 na fedha hizo kufikia jumla ya sh, milioni 129 .

"Niliwauliza kwanini wanaingiza fedha kidogo kidogo, walinijibu ni masuala ya kibiashara, hawawezi kutoa fedha zote kwa mkupuo mmoja "

"Baada ya malipo hayo ya awali ,kampuni ya Afrinexus Logistics walinipigia simu kuniambia kuwa wameshapata malori ya haraka hivyo hawatahitaji tena,jambo ambalo ni kinyume na utaratibu "

"Niliwauliza itakuwaje na mimi nilishatoa oda China, waliniambia nisijali tutaongea,basi niliwajulisha huko mchina waliniambia walishafanya oda kwenye meli na itanilazimu wanikate dola 18,000 "

Alisema mapema mwaka huu, Februari 3,alipigiwa simu na Kamanda Muliro akimwambia afike ifisini kwake na baada ya kuitikia wito huo akiwa na mwanasheria wake,Muliro alimwambia ameagizwa na kiongozi mkubwa wa serikali(jina tunalo) arejeshe kiasi cha sh,milioni 129 huku akimsisitiza kuwa hatatoka ofisini kwake bila kutoa kiasi hicho cha fedha .

"Nilifika ofisi ya Kamanda Muliro nilimkuta akiwa katika hali ya kupaniki akawa ananifokea sana kuniambia kunatuhuma kutoka kwa mtu mkubwa sana serikalini kuwa wewe ni tapeli umefanya biashara za kitapeli lipa pesa za watu,nilijitahidi kumuuliza iwapo kama ameona mkataba wa mauziano aliniambia hahitaji mkataba lipa pesa za watu"

"Baada ya mabishano ya muda mrefu sana Kamanda Muliro aliniambia ndugu yangu Samweli wewe ni mdogo wangu usibishane na dola ukishaambiwa mtu ameshika mpini wewe umeshika makali hauta muweza, nakushauri kama mdogo wangu nenda kalipe hizo fedha na kuanzia sasa hutatoka hapa mpaka utuambie utalipaje hizo fedha"

Nikiwa hapo ofisini walinibana sana na kushikilia gari yangu na baadaye waliniambia nijidhamini nilienda nyumbani na kesho yake nilirejea ofisini kwa kamanda Muliro, waliendelea kunibana nikapiga simu kwa rafiki yangu akanikopesa milioni 20,tulienda benki usiku na askari polisi tukachukua pesa na kuziingiza kwenye akaunti ya Afrinexus Logistics na baadaye walinirejeshea gari yangu kwa masharti nikalipe fedha hizo"

Alisema askari hao wakiongozwa na Kamanda Muliro waliendelea kumpigia simu yeye pamoja na mke wake wakimwambia kwamba asipolipa hizo fedha watamfungulia kesi yoyote na wamekamata lori lake lililokuwa Mkoani Simiyu wakishinikiza alete pesa na wametishia kuliuza iwapo ataendele kukaidi .

"Wameingilia mawasiliano yangu ya simu na akaunti zangu za benki kila pesa inayoingia wanaona na wametishia kuzima WhatsApp yangu niliamua kwenda kulala hotelini ila walinifuatilia na kuja kuzingira hoteli niliyolala"

"Nilifanikiwa kutoroka kwa kutumia usafiri wa bodaboda hadi mto Wami nilipofanikiwa kupata usafiri mwingine wa kuja Arusha"

Alisema kwa sasa anajipanga kulifikisha suala hili mahakamani na tayari ameanza mchakato wa kukutana na mwanasheria wake ili likaamuliwe kisheria kuliko utaratibu unaotumiwa na upande wa pili wa kutumia nguvu ya polisi.

"Kwa sasa polisi wananitishi maisha wanasema hao unaosikia wanaonekana kwenye viroba ni watu kama wewe"

Samweli alimwomba Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati suala hili kwa kuwa yeye ni Mfanyabiashara anayetambulika ili suala hili liamuliwe kisheria.

Kamanda Muliro hakuweza kutoa ushirikianao baada ya kupigiwa simu akidai yupo kwenye msiba wa Hayati ALLY HASSAN MWINYI.


Ends..
"UNANIJUA MIMI NI NANI?"...imerudi...da!!
 
Tanzania mtu akimiliki m100 utasikia oh yule ni milionea bwana, sasa kama huyo mushi wanasema ni bilionea, je wakina Bakhresa na GSM tusemeje! 😄 wakati huku kwetu kanda ya ziwa kuna watu wana hela na hawajionyeshi.
Hela nyingi za watu wa kanda ya ziwa ni za kichawi (ndugu)
Tatizo ni ushamba wa pesa na umasikini ndio maana kitu kidogo kina kuzwa haswa.
 
Na ukitaka ujue watanzania ni wajinga angalia comment za watu
Tumeingia mkataba alafu kesho unakuja unataka uvunjwe kienyeji enyeji ndo maana waekezaji kila siku wanatupiga hela kama nchi

Mkataba haivunjwi kienyeji enyeji ndo kitu watu wengi hawakijui
Wengine wanajua lakini wana uoga wa kipumbavu!
 
Back
Top Bottom