mswele
JF-Expert Member
- Dec 18, 2014
- 687
- 419
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Mary Nzuki amesema wanamshikilia mfanyabiashara Lucas Sasha kwa kosa la kumuua mpita njia Mahmoud Ally kwa kumpiga risasi maeneo ya Tabata Kisukulu wakati wa sherehe za Christmas.
Kwa mujibu wa maelezo aliyoyatoa Sasha amesema kuwa kulikuwa na kundi kubwa la vijana waliokuwa wanapita mbele ya nyumba yake hivyo akadhani kuwa amevamiwa na vibaka, akaamua kupiga risasi.
Kamanda Nzuki amesema mfanyabiashara huyo anamiliki bastola hiyo kihalali, kwa sasa Polisi wanamshikilia kwa ajili ya uchunguzi wa tukio hilo.
Chanzo: HABARI LEO