Mfanyabiashara Arusha amwaga machozi kanisani

buswelu moja

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
226
147
Mwandishi wetu, Arusha

Katika hali isiyo ya kawaida mfanyabiashara maarufu ambaye pia ni mkurugenzi wa makampuni ya Rainbow Shuttle and car hire pamoja na Rainbow crater lodge, Mathew Shamba Mollel amejikuta akimwaga machozi mbele ya madhabau katika kanisa la KKKT usharika wa Moshono wakati wa ibada ya Shukrani kanisani hapo.

Mfanyabiashara huyo alifika mapema leo katika misa ya asubuhi kanisani hapo akiongozana na ndugu, jamaa na marafiki ambapo baada ya kupewa nafasi ya kusema neno katika ibada hiyo ghafla alianza kumwaga machozi akiwa madhabauni.

Akizungumza kanisani hapo Mollel alisema kwamba mgogoro wa ardhi baina yake na aliyekuwa mkuu wa wilaya mstaafu nchini marehemu ,Dahn Makanga ni miongoni mwa mambo ambayo hayatafutika katika historia ya maisha yake.

Mollel, alisema kwamba mgogoro huo wa ardhi ambao ulipelekea yeye kufunguliwa kesi ya kughushi nyaraka mbalimbali katika mahakama ya hakimu mkazi na baadae mahakama kuu kanda ya Arusha ni miongoni mwa kumbukumbu ambazo hazitafutika katika maisha yake jambo ambalo limempelekea binafsi kutoa Shukrani.

Alisema pamoja na kushinda kesi zote mahakamani lakini ana sababu ya kipekee kumshukuru Mungu kwa kuwa amepitia mapito na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kunusurika kifo wakati akipambana na kesi inayomkabili mahakamani.


"Nimewasamehe wote ambao walinikwaza wakati wa kesi yangu ya mgogoro wa ardhi na hata wale ambao walitaka kutoa uhai wangu kutoka moyoni mwangu natamka Nimewasamehe "alisema Mollel

Kwa upande wake mchungaji kiongozi wa usharika wa kanisa hilo, Sion Peter aliwataka waumini wa kanisa hilo sanjari na watu wote nchini wawe na moyo wa kusamehe bila kujali uzito au ukubwa wa jambo alilotendewa.

Mchungaji huyo Alisisistiza kuwa watu wanapaswa kuachana na tamaa za mali bali kuwajali watu wenye uhitaji na kujitolea kuwapatia misaada mbalimbali na sio kupenda mali kuliko kumpenda Mungu.

Mwisho.

Pichani ni mfanyabiashara ambaye pia ni mkurugenzi wa makampuni ya Rainbow Shuttle and car hire pamoja na Rainbow crater lodge, Mathew Shamba Mollel akiwa katika kanisa la KKKT usharika wa Moshono wakati wa ibada ya Shukrani Leo kanisani hapo.

Picha nyingine akiwa na mchungaji kiongozi wa kanisa hilo, Sion Peter
IMG-20200119-WA0045.jpeg
IMG-20200119-WA0043.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo ushauri wa mchungaji una mfaa zaidi Mollel mwenyewe,maana wafanyabiashara wakubwa wengi wao ni wanyang'anyi na wenye roho ngumu kweli kweli hawaoni shida kukupoteza ili wamiliki hekari moja yako.

macson
 
Hili thehebu la KKKT linanyenyekea sana watu wenye pesa na kusahau jukumu lao la kutunza roho za waumini bila kujali kipato.

Hiyo nafasi aliyopewa mpaka ya kulia madhabahuni ni kwa sababu ya alichonacho. Sidhani kama kuna utaratibu wa waumini kusimama mbele na kuongelea yanayowasibu katika maisha yao ya kila siku.
 
Hili thehebu la KKKT linanyenyekea sana watu wenye pesa na kusahau jukumu lao la kutunza roho za waumini bila kujali kipato.

Hiyo nafasi aliyopewa mpaka ya kulia madhabahuni ni kwa sababu ya alichonacho. Sidhani kama kuna utaratibu wa waumini kusimama mbele na kuongelea yanayowasibu katika maisha yao ya kila siku.
Sio KKKT pekee. Leo nimesali RC kuna ile moment ya kutaja waliotoa shukrani maalum. Wote waliotoa chini ya elfu 50 walikuwa wanaitwa "mkristo mmoja ametoa shilingi...." lakini waliotoa juu ya elfu 50 walitamkwa "bwana/bibi fulani ametoa shilingi kadhaa kwa ajili ya...". Hata majuzi hapa Diamond alitoa zawadi ya msikiti kule Kigoma, kinyume na mafundisho yao.
 
Kuna DC Maganga wa Geita nayeye ana kesi ya wizi wa shamba, Hawa jamaa sijui wakoje?
 
Back
Top Bottom