TANZIA Mfanyabiashara Andrew Mollel afariki dunia (mmiliki wa Happy Sausages)

... kwa sura yake tu jinsi anavyoonekana mwili kutepeta; yule mgeni hatari akibisha hodi hata kuitika hawezi! Mwili umetepeta sana. RIP.
kwani umiambiwa hiyo ndo picha alipiga siku ya kufwaliki?
 
Mfanyabiashara maarufu mkoani Arusha, Andrew Mollel ambaye alikuwa mwanzilishi na Mkurugenzi wa kampuni mbalimbali mkoani Arusha amefariki dunia na kuibua simanzi kwa wakazi wengi wa jiji hilo.

Akizungumza na Mwananchi leo, Februari 28, Mbunge wa jimbo la Monduli , Fredrick Lowassa amesema kifo cha Mollel ni pigo kubwa katika jiji la Arusha kutokana na mchango wake.

Lowassa amesema taratibu za mazishi wa Mollel zinaendelea kufanywa na wanafamilia lakini, kubwa ambalo Arusha watamkumbuka ni kuandaa michoro ya mradi mkubwa wa nyumba za PPF zilizopo eneo la Kijenge jijini hapa ambalo lilikuwa ni eneo lake.

Mollel alikuwa pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Happy Sausages ,Kijenge Animal Products Limited, Georges Center Ltd na AGM Holding na pia mjumbe wa bodi mbali mbali hapa nchini.

Mollel pia alikuwa ni rafiki wa karibu wa Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa.

Kifo cha mfanyabiashara huyu ni mfululizo wa vifo vya wafanyabiahara kadhaa katika jiji la Arusha katika siku za karibuni.

Taarifa zaidi za kifo cha mfanyabiashara huyu zitaendelea kutolewa
View attachment 1714082
JamiiForums siku hiziimegeuzwa bang la matagazo ya vifo, basi muwe mnalipia matangazo haya ya vifo kwa JamiiForums.
 
Hapana wa Elerai Constructions, Northern Engineering ni Lema.
Sio kweli, kuna Northern Electrical na kuna Elerai Constructions co.

-Wa Northern Electrical ni ADAM MOLLEL

-Wa Elerai Construction ni LEMA na ambaye sasahv serikali imemfilisi sana kupitia ile kampuni inayotoa matofali mazito ya kerai i.e

Kerai Construction Company
 
RIP mzee wetu, nina rafiki waliokuwa wamepata tenda wanasupply kwenye biashara yako.

Mkuu Nguseroh kuna siku moja taarifa ya kifo itakuwa yako, watu wako wa karibu watakuwa wanapigiwa na kuambiwa tuna habari mbaya, "Nguseroh katutoka" kwasabu wote ni njia moja tuonyeshe heshima kidogo hata kwenye nyuzi zinazomuhusu marehemu maana watu wake wa karibu wanazisoma au watazisoma. Ujumbe unaoandika unakaa hapa kwa miaka mingi sana mbeleni. Inshort, humu ni moja ya eneo la msiba. Onyesha heshima kwa kuepuka kutoa maoni ya ngono au kejeli zisizo na umuhimu kwenye eneo hili la Tanzia.
Mkuu heshima kwako. Ujumbe wako umenigusa kichiz inabid nijirekebishe. But my hands are tide there's nothing i can do stopping boosting my soul (cha Arusha)

Lord help me!
 
Back
Top Bottom