Mzee Mwanakijiji,
Mkandara, ninachosema mauaji ya Albino hayawezi kuzimwa nje ya sheria. Hiyo ndiyo tofauti yangu na wewe na hata Waziri Mkuu. Kusema kwamba tukomeshe mauaji ya albino ndipo tuangalie sheria haiwezekani ni sawa na kuweka mkokoteni mbele na farasi nyuma.
Mkuu nadhani wewe ndiye unaweka mkokoteni mbele ya farasi...
Mauaji ya Rwanda yalitokana na Ubaguzi wa muda mrefu kati ya makabila mawili - Wahutu na Watusi ktk ardhi ndogo, hayo maneno ni kichombezo tu kinachofuata nyuma kama huo mkokoteni..
Mashariki ya kati pia ni ubaguzi kati yao wakipigania ardhi ndogo ambayo kila mmoja wao anadai ni yake.. maneno yanafuata kama sababu tu, ni sawa na sisi hapa tunabishana kwa maneno lakini issue iliyopo ni mauaji ya Albino. Kama haya wauaji hasingekuwepo mimi na wewe tusingechukua muda hapa kuyazungumziawala tusingemsikia Pinda..
Na kutokana na maneno ya uchocheaji ndiyo maana nikauliza kama wewe na Pinda mna kitu kingine nje ya hoja hii kwa sababu sioni kabisa sababu ya uchochezi unaojaribu kuupandikiza ikiwa hakuna sababu iliyotangulia.. Siwezi kukuita wewe ni mchochezi au kujaribu kufikiria nini matokeo ya hoja zako kwa sababu nina hakika kuna kitu kilichotangulia kabla...Hata kama Pinda ataomba samahani bado hutakubali, Na ili kupata uhakika zaidi nilikuuliza kihsa ni kakubali uliposema kwamba Unachukizwa na Pinda kushindwa kuwalinda Albino..Hiyo pekee ilitosha kabisa lakini hoja ulizoendelea kuzijenga zilikuwa nje kabisa ya sababu kubwa!..
Mkuu wangu hizi sheria na sijui katiba ni upuuzi mtupu kwangu mimi kwa sababu ni Katiba hiyo hiyo inayomlinda Mkapa.. Ni katiba hiyo hiyo inayo wanyima haki vyama vya Upinzani na ni katiba hiyo hiyo inayoshindwa kuwa protect Albino kisheria wakati katiba hiyo inaweza kuwa protect Vifaru,Tembo n.k..tena tumeweka askari wenye bunduki na risasi za moto dhidi ya wawindaji wenye pinde na mishale..Mkuu siwezi kabisa kuitazama katiba kwa maneno ya Pinda isipokuwa nitaitazama katiba na sheria zetu kwa nini zimeshindwa kuwalinda Albino..Na Pinda, Masha na Said Mwema wajiuzuru kwa sababu wameshindwa kazi yao kuwalinda raia wao.
Muuaji yeyote wa hawa Albino anatumia silaha - iwe kisu, rungu au mkuki yaani ni it's a premeditated murder isiyo ya kawaida kwani sijui ni psychological feature gani zina arouse desire zao za utajiri...ila nachoweza kusema ni kwamba hawa jamaa wanapotoka kuwinda Albino wako vitani, kama wanyama vile Predators, hivyo nasi tuangalie zaidi ni jinsi gani tunaweza kuwalinda Albino kabla ya sheria.
Majeshi ya marekani yapo huko Iraq na Afghanstan wanapenda sana watumie sheria na katiba lakini wanajua wanapambana na watu wa aina gani hivyo wao pia wanajiandaa na silaha za kuteketeza.Kama adui atasalimu amri au kukamatwa ndio sheria inafuata lakini kabla ya hapo ni vita tu!..
Hivi kweli ktk akili yako unafikiri unaweza kuwakamata hawa watu kirahisi kiasi kwamba uwafikishe mbele ya sheria kama vile kibaka wa mtaani anayeiba simu na kutoka mkuku..Hatuwezi kuzuia wizi nchini wala nchi za nje ni kitu ambacho kitaendelea kila siku ya maisha yetu na ndio maana tunaunda sheria kali na hukumu zake dhidi ya crimes kama hizi, lakini mauaji ya Albino ni beyond vitu vyote hivi -tumevuta mipaka ya Utu na hakika mauaji haya yanaweza kabisa kukomeshwa!..
Nakumbuka JK alipoingia madarakani kitu cha kwanza ilikuwa kukomesha majambazi, na hakika bila kauli wameuawa wengi sana, wenye bahati ndio wameipata sheria, nadhani unakumbuka wale Wakenya na yuile mama mfanyabiashara waliouawa Moshi..Toka siku ile majambazi wameingia mitini..Kwa hiyo maneno sii lazima kuchochea bali inaweza kabisa kuondoa magugu ktk shamba la ngano...
Mkuu wangu tusijidanganye, wanaoua Albino sii wachawi, ni watu wazima wenye akili zao timamu kwa hiyo wanaua sii kwa kutumia mitulinga ya uchawi ila wanatumia silaha na kibaya zaidi hao Albino sasa hivi ni sawa na Endangered spicies - samahani kwa kutumia lugha hiyo. Muhimu nakuomba unielewe kwamba nachosisitiza mimi ni kuweka nguvu zetu ktk kuwalinda watu hawa kabla hatujafikiria nje ya rai ya Mh. Pinda...
Mkuu Pinda kachemsha politically..hakutakiwa kusema aliyosema lakini binafsi vita dhidi ya wauaji wa Albino ni vita ya kufa na kupona..Ama zao ama zetu!