Mfanano wa wasaniii katika Sanaa na tansia kwa ujumla

Dagger-v

JF-Expert Member
Mar 6, 2020
2,212
2,000
Habari za muda huu jf members , Poleni na Covid19's fever
Let's us Go back to our topic.

Katika Sanaa huwa ni nadra Sana kutokea wasanii wawili au zaidi kuwa na aina moja ya Sanaa ambayo ukiiangalia n km zinafanana iwe kwenye kuimba, au kuigiza ...katika Sanaa yetu hapa Bongo tumebahatika kupata baadhi ya wasanii ambao ...aina ya nyimbo zao au uigizaji wao kwenye movie n km ulikua unafanana mpaka nashabiki wakaanza kuwafanyia comparisons.

Hawa n baadhi ya wasanii na presenters waliowahi kutokea kufanana kupitia Sanaa zao mpka nashabiki wakaanza kuwafananisha

Steven kanumba Vs Vicent kigosi(Ray)

Kupitia Bongo movie Hawa jamaa waliteka sana nyoyo za watu , lakini ukiachilia kukubalika ikifika mahali n km walikua wanafanana kuanzia life style mpaka uigizaji na aina ya movie wanazozitoa mpaka wakaingia kwenye beef la chini chini

Salama jabiri Vs Dj fetty

Hawa n moja ya presenters wawili ambao walikua wanafanya vizuri Sana kipindi Cha nyuma ....Ila Kuna kipindi nashabiki walianza kuwa compare kua Kati yao Nani n mkali na hii ilikua n kutokana na mfanano wao wa kupresent vipindi vyao

P funk majani Vs Master j

Hawa producers ambayo wanahistoria kubwa Sana katika sanaa ya Bongo na haitaweza kufutika kirahisi coz wametimiza ndoto za wasanii wengi na kuwa insparational kwa upcoming producers
Kuna kipindi watu walianza kuwa compare kutokana na lifestyle na aina ya ngoma zao Hadi ikifika kipindi wakawa na beef ...

Lady Jay dee Vs Ray c

Jide na Ray c hawakua na uimbaji unao fanana Ila katika kipindi chao walikua wao ndo wanafanya vizuri so ilifika time nashabiki wakaanza kuwashindanisha

Yp na y-dash

Hawa washikaji kutoka kiumeni walikua wanastyle zinazofanana na wakashauriwa wafanye music pamoja na katika kipindi chao walifanya vizuri

TID vs Q chief

Wana aina ya music unaofanana Hadi waliamua kufanya band ya pamoja ...

Sumalee vs C-pwaa

Hawa jamaa kuanzia sauti, uimbaji wanafanana walikua na kundi lao baadaye wakavunjika

Gigy money vs Amber lulu

Ukiangalia lifestyle yao na namna wamepata umaarufu wanafanana kwa vingi

Nandy vs Ruby

Hawa wanafanya pouwa Sana Ila waliingia ktk kushindanishwa kutokana na aina ya music unaofanana

Barnaba vs Amini

Barnaba na amini wanafanana kuanzia uandishi na pia hata baadhi ya melody wameshiriki kutengenezea wasanii wa T.H.T

Godzilla vs Bilnass

Hawa n sauti tuu kwa mbali zilikua zinafanana Ila ufanano ulikuzwa na mashabiki tuu Hadi ikapelekea kum deprese Godzilla

Diamond vs Ally kiba

Hawa style za kuimba n tofauti Ila wamenimgia katika kategory hii kwavile ya nguvu ya mashabiki

Stereo vs One the incredible

Stereo na one wameshafananishwa Sana kutokana na style ya uchanaji Tangu enzi za kilingeni

Mario vs Jaymelody

Hawa walitoka kipindi kimoja na style yao ya kuimba n sawa Ila kwa Sasa Mario anafanya vizuri zaidi

Shilole vs Snura

Hawa walikua waigizaji baadaye wakaingia kwenye music japo hawana vipaji vya music Ila kupitia Kiki na unenguaji jukwaani wakatoboa

Bell 9 vs Ben Paul

Hawa Wana aina flani ya music unaofanana na watu wengi huwa wanajaribu kufanya comparisons kuwa yupi n mkali

Ay vs Fa

Kuanzia life style ..smartness upstairs na urafiki baina yao

Mr blue vs Josline

Kuna kipindi dulysykes aliamua kuwashirikisha katika ngoma yake ya dhahabu pasipo wawili hao kujua kwakua kipindi hiko walikua wanabeef kutokana na watu kuwa compareOne love
 

Citizen B

JF-Expert Member
May 13, 2019
6,209
2,000
Harmonise na hamorapa
Gwajima na nabii tito
Mario na kusah
Aristote na wema sepetu
Rakim na mshana

Najua ni nje ya mada lakini umeicheki avatar yangu mkuu?
 

Dagger-v

JF-Expert Member
Mar 6, 2020
2,212
2,000
Harmonise na hamorapa
Gwajima na nabii tito
Mario na kusah
Aristote na wema sepetu
Rakim na mshana

Najua ni nje ya mada lakini umeicheki avatar yangu mkuu?
kwamba unataka kusema sijatumia akili ....na kwann niumize akili wakati mada iko katika jukwaa la burudani

One love
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom