Mfanano wa TCRA na EWURA

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
4,052
12,904
Ewura mafyta yakishuka leo kwenye soko la Dunia Tanzania inaweza kuchumua wiki 2 kushusha ama kutoshusha kabisa, utaambiwa bado kuna shehena ya zamani lakini mafuta yakipanda leo jioni tu unawaona wanapandisha bei, unajiuliza kwani shehena ya zamani yenyewe imeisha ghafla?

TCRA wakiambiwa wapandishe vifurushi dakika sifuri lakini kushusha unaambiwa mitambo haifanyi kazi ghafla namna hiyo.

TCRA na EWURA ni makampuni ambayo yamewekwa mfukoni na wafanya biashara wa mafuta na mitandao ya simu.

Mitandao ya simu inajipangia bei ya vifurushi wanavyotaka, wanajipangia makato ya simu wanavyotaka husikii seeikali ikisema jambo lolote.

Tanzania badala ya teknolojia kurahisisha maisha huku Tanzania ni kinyume chake, mitandao ya simu iko kunyonya wananchi.

Serikali isipokua makini itawekwa mfukoni na haya makampuni na tutakaoumia ni wananchi.
 
Serikali yenyewe haina ubunifu wa kutafuta vyanzo vipya vya kodi! Na kwa ujinga wao wa kunyima wapinzani haki ya kuingia bungeni, ndiyo basi tena. Watakosa zile taarifa muhimu kutoka jambi ya upinzani, za kuvumbua vyanzo vipya vya mapato!

Wataendelea tu kutupandishia kodi kwenye vifurushi, miamala, bia, soda, sigara, nk. Ubunifu kwao ni zero.
 
Back
Top Bottom