Mfalme wa Qatar atua Zenj kwa mbwembwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfalme wa Qatar atua Zenj kwa mbwembwe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kwamwewe, Sep 13, 2010.

 1. kwamwewe

  kwamwewe JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2010
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,315
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Mfalme wa Qatar, Ahmad Bin Khalifa Al Thani amewasili Zanzibar kwa mbwembwe akiwa katika mapumziko ya Eid el Fitri yatakayochukua muda wa wiki moja na kulala katika boti ya kisasa iliyofunga nanga katika mwambao wa bahari ya Zanzibar.

  Mtawala huyo wa Qatar aliwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akiwa katika ndege aina ya Air Bus 340, akiwa na wasaidizi zaidi ya 42 mnamo saa 4 juzi usiku.

  Akiwa ameambatana na mkewe na watoto, baada ya kuwasili alielekea katika bandari ya Malindi na wasaidizi wake walikwenda moja kwa moja katika hoteli ya kimataifa ya La Gema, iliyopo katika kijiji cha Nungwi, mkoa wa Kaskazini Unguja.

  Mfalme huyo amekuwa akilala katika boti maalum yenye huduma zote ikiwemo ulinzi na usalama mkubwa, boti hizo mbili ambazo ziliwasili Zanzibar siku mbili kabla ya kufika kwake.

  Baada ya kuwasili katika bandari ya Malindi boti maalum inayomilikiwa na kampuni ya Azam Marine ilipewa jukumu la kubeba mizigo ya wageni hao kupeleka katika boti za mfalme.

  Wasaidizi wa kiongozi huyo wameibua mjadala mkubwa Zanzibar kutokana na msaada wa kifedha wanaotoa kwa vijana wanaowasidia shughuli zao, baada ya juzi vijana waliokuwa wakiwabebea mizigo kulipwa dola 100 kila mmoja kwa kazi ya saa moja.

  “Kweli leo nimeamka vizuri sikutegemea kupata dola 100 kwa kazi ya saa moja kupeleka mizigo na kuja kwa mfalme ni faraja kubwa kwetu”, alisema mfanyakazi mmoja.

  Hata hivyo, ndege iliyomleta mfalme huyo baadaye iliondoka uwanja wa ndege Zanzibar kulekea Dar es Salaam ambako itaegesha kumsubiri mfalme hadi atakapomaliza mapumziko yake kutokana na uwanja wa Zanzibar kuwa na nafasi ndogo.

  Imeelezwa kwamba mfalme huyo akiwa Zanzibar atajishughulisha na michezo ya baharini, ikiwemo kuzamia, ambapo pia atafanya ziara kama hiyo kisiwani Pemba pamoja na kutembelea baadhi ya visiwa vidogo viliyopo Zanzibar.

  Waziri wa Nchi Afisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma amethibitisha kuwasili kwa kiongozi huyo, lakini alisema ziara yake ni ya kibinafsi na sio ya serikali.

  Hata hivyo, alisema kuja kwa kiongozi huyo ni faraja kwa Zanzibar hasa katika kutangaza sekta ya utalii na kuizihirishia dunia kuwa Zanzibar ni nchi ya amani hasa wakati huu wa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.
  Zanzibar imewahi kuwa na mfumo wa uongozi wa Kifalme kabla ya Mapinduzi ya mwaka 1964.

  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Isije ikawa kaja kukamilisha deal zake uko Znz
   
 3. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  aliwahi kuja hata mara moja kabla ya zanzibar kuanza kuvunja muungano?
   
 4. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Duh isijekuwa ni maandalizi ya Zanzibar kuwa nchi.
   
 5. Margwe

  Margwe JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2010
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sijaelewa mbwembwe zipi hapo?
   
 6. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  $100(TZS 150,00) per hour paycheck.......au hii ni kawaida kwako mkuu? kwa mwezi hii ni kama $ 16,000 for a mere porter...hata Ndulu havuti hela ndefu hivi
   
 7. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Waacheni Wanzazibar wawe nchi hata Muungano wakitaka wavunje tu...Kwanini watung'ang'anie sie wakati nchi imevunda kwa rushwa..Wakati umefika tuamke tuipiganie Tanganyika yetu iliyonajisiwa kwa miaka kadhaa tuache kushupalia ya watu yakwetu yanatushinda.
   
 8. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #8
  Sep 13, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Soma sentensi ya mwisho......ndio wanarudi hivo....ukitoa $100 kwa watu 1,000,000 nchi ni yako...what is $100m to him?
   
 9. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  hapo kaletewa vimwana bikira vya kitanzania kwaajili ya kuwaburudisha , waarabu hawa wamekuwa wakifanya hivi kule Loliondo hawana maadili ni wachafu sana na pesa zao za mafuta.
   
 10. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #10
  Sep 13, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  NCHI isha uzwa hii
   
 11. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #11
  Sep 13, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mbona mavuvuzela haya hayakusikika wakati alipokuja BUSH Tanganyika?.
   
 12. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #12
  Sep 13, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  na huyu huyu ndiye alitaka ardhi yenye rutuba tz alime mpunga, ili kuficha jakaya Mrisho akaibuka na Kilimo kwanza
   
 13. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #13
  Sep 13, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hivi bado Seif hajaingia Ikulu, akiingia si itakuwa balaa?
   
 14. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #14
  Sep 13, 2010
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ukijishuhulisha na yasio kuhusu utapata yasio kuridhi
   
 15. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #15
  Sep 14, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kumbuka amekuja na mke wake!
   
 16. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #16
  Sep 14, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,811
  Likes Received: 1,146
  Trophy Points: 280
  Naona tayari utumwa unarudi zanzibar,hivi tayari tushawaachia hako kakisiwa ama bado??kelele zao zote sababu kubwa ni hiyo,mwarabu arudi awapakate.
   
 17. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #17
  Sep 14, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mhh lets wait and hear if there will be any deal to be signed
   
 18. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #18
  Sep 15, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Acheni wenye pesa zao wapumzike na watutangazie nchi yetu huko ughaibuni. Maana huko Ughaibuni ukitaja Uganda, mara moja watakwambia 'Idd Amin'. Sasa taja Tanzania ni mtafutano, mpaka aingie kwenye mtandao, wapi na wapi.
   
 19. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #19
  Sep 15, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280

  Hahahhahah! acha nicheke kwanza, maana hayo uliyosema yananikuta kila siku. Idd Amin wanamjua kama nini, Kenya wanaijua kwa kufukuza upepo. Tanzania, mmmmmmmmmmmhhhh labda uanzie kilimanjaro mountains. ndo uje Tanzania.
   
Loading...