Mfalme wa Morocco kuzuru Tanzania

Mfalme wa Morocco kuzuru Tanzania

MUTTAZ

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2016
Posts
296
Reaction score
237
Kwa mara ya kwanza, Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, Jumapili hii anaitembelea Tanzania kwa ziara ya kikazi baada ya kuzuru Rwanda.

Miongoni mwa ajenda kuu za ziara yake ni kuishawishi Tanzania kuiunga mkono Morocco kurejeshwa katika Umoja wa nchi za Afrika. Aidha, atatia saini mikataba ya kibiashara na kidiplomasia kati ya Tanzania na Morocco.

Mfalme Mohammed VI pia atazuru pia Ethiopia.

Mwandishi wetu wa Dar es Salaam Arnold Kayanda amezungumza na waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bw Augustine Mahiga na kuandaa taarifa hii.

Source BBC Swahili http://bbc.in/2ezpJeu
 
Morocco kama ulaya vile japo ipo Africa na iliwekewa vikwazo lukuki./
Tushikamane na taifa hili lipo Juu sana hasa katika teknologia ya Nguo./

Growing Morocco’s Textile Industry
***
•sekta ya Nguo inachangia taifa lao kwa 23%./ katika pato la taifa./
 
Kwa nini Morroco ilitoka Jumuiya ya Afrika ya kwanza na kwa nini sasa irudi??
 
Kwanza waache ukoloni huko Sahara Magharibi ndio warudishwe kwenye jumuia ya Afrika. Hich ndio kiliwatoa . Haiwezekani nchi moja ya kiafrika inatawala ingine kwa mabavu baada ya wakoloni wahispania kuondoka mwaka 1975 bila maadili na kuikabidhi Morocco. Umoja wa mataifa umekuja na pendekezo la kufanya kura ya maoni kwa wananchi halisi wa Sahara Magharibi kama wanataka uhuru au kubaki chini ya Morocco, lakini Morocco hawataki
 
  • Thanks
Reactions: MTK

znz tunaifanyaje?
 
Jina rasmi la Morocco ni "al-Magrib al-Aqsa", yaani "Magharibi ya Mbali". Iko km 13 (8miles) kutoka Ulaya. Vazi jeupe kwa wanawake ni ishara ya kufiwa mume (ujane) na hulivalia kwa muda wa siku 40. Hii nchi imetulia kulinganisha na nchi nyingine nyingi katika ulimwengu wa kiarabu.
 
Kwa mara ya kwanza, Mfalme wa Morocco, Mohammed VI, Jumapili hii anaitembelea Tanzania kwa ziara ya kikazi baada ya kuzuru Rwanda.

Miongoni mwa ajenda kuu za ziara yake ni kuishawishi Tanzania kuiunga mkono Morocco kurejeshwa katika Umoja wa nchi za Afrika. Aidha, atatia saini mikataba ya kibiashara na kidiplomasia kati ya Tanzania na Morocco.

Mfalme Mohammed VI pia atazuru pia Ethiopia.

Mwandishi wetu wa Dar es Salaam Arnold Kayanda amezungumza na waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bw Augustine Mahiga na kuandaa taarifa hii.

Source BBC Swahili http://bbc.in/2ezpJeu
Huu ni mtego mkubwa sana kwa serikali ya Tanzania, Morroco bado wanaitawala Sahara Magharibi kimabavu na ndio ilikuwa sababu ya Morroco kujitoa AU, Tanzania imekuwa mstari wa mbele sana kwenye swala la ukombozi, je tutawasaliti Sahara Magharibi kwa maslahi ya kisiasa?!
 
Haya mambo ya ukombozi hayana tena wakati kwa sasa/
YALIISHAGA MIAKA YA 80's./
•kwa sasa ni jinsi ya kunyanyua uchumi wetu tu./ hatuna adui wa kudumu wala rafiki wa kudumu [HASHTAG]#uchumi[/HASHTAG] kwanza.
 
Back
Top Bottom