PGO mwiba kwa maafisa wa Jeshi la Polisi, wanafanya kazi kwa taratibu zipi?

Yoote hayo ya pgo ni kweli lakini amini nawaambia hayataondoa makosa yanayowahusu watuhumiwa nyie muoneni jaji kama vile Yuko upandw Fulani nachelea kuhisi kuwa mwisho wa kesi upande mmoja utalia na kusaga meno
Anaekugonga hakupatii
 
..
20210921_170848.jpg
 
Tatizo lilianzia kwenye jina lao, kwamba wao ni Police force, hiyo Force ndo ipo kwenye akili zao wote kuanzia asiye na cheo hadi IGP, na sasa shughuli au kazi zao zinategemea na malezi ya mtu aliyolelewa nayo toka kwa wazazi wake au hofu yake kwa Mungu.

Wewe fikiria, ina maana kauli zao za kwamba Tii sheria bila shuruti hapa ni sheria gani hizo wanazomaanisha ili hali wao hawajui kilichomo ndani ya sheria yao kuu PGO?
Tii PGO bila shurutiii
 
Acha ujinga na upuuzi wako. Kuna dada kabakwa na kapigwa na simu mbili na pesa kachukuliwa. polisi wamepewa mpaka imei za zile simu na bado wakamtaka aliyebakwa atoe pesa elfu 50000 ili simu ifatiliwe katoa na mpaka Sasa hakuna kitu. Labda ukibakwa wewe wanaweza kufatilia.

sawa bana endeeni kunakwa.
naona unatka kunitoa roho hapa kisa nyinyi kubakwa.
 
Mbona mimi nipo na sina connection yoyote? Sasa kama polisi ni wahuni wanakagua nini?

ndio maana huna ubunge wala usiwani.
kazi yako ni kumtetea mwenyekiti tu.

polisi wanakagua vibaka na wahalifu.
 
Kuna vitabu vya kufikirisha, kimoja Ni hadithi niliyoisoma kwenye muendelezo wa vitabu vya kiada vya kufundishia kiswahili elimu ya msingi. Kuna kinyozi alipewa kazi ya kumnyoa mfalme. Kumbe mfalme alikuwa na masikio Kama ya punda. Siri hii ilijulikana tu na huyu kinyozi. Sharti ilikuwa Ni akivujisha tu Siri hii Basi hukumu yake ilikuwa Ni kunyongwa Hadi kifo.

Siku moja alishindwa kuvumilia ikabidi aende mbali msituni na kuchimba shimo ndipo alipotamka kawa sauti..."mfalme ana masikio Kama ya punda"..kilichotokea baadaye Ni huyo mlame kuikimbia nchi kwa aibu. Baadaye kwenye lile shimo likaota mti. Mti ulipokuwa mkubwa Basi kipindi upepo ulipovuma Ile sauti iliweza kusikika Hadi himaya yote ya mlame kupata na kujua kuhusu mfalme wao.

Polisi wetu wanajaribu kila kukicha kuzuia watu wasipate mahojiano na muenendo mzima wa kesi walioifungua dhidi ya Mbowe na wenzake 3. Kila siku wanakuja na mapya ilimradi hiyo kesi iendeshwe gizani pasipo wananchi kujua yanayoendelea. Hii Ni hatari na ni sawa na kuficha Siri. Siku hukumu ikitoka na Bahati mbaya iangukie kuwa Mbowe amefungwa na wale wenzake, Basi ikapotoshwa kuwa Ni uonevu nadhani Kuna mawili yanaweza kutokea.

1. Imani itaanza kupotea juu ya jeshi letu la polisi dhidi ya raia na hata saa zingine hujuma dhidi Yao kufanyika.
2. Hali ya usalama inaweza kuzorota nchini kwa kuibuka makundi halisi ya kigaidi ambayo haikuwa kusudio zitokee kwa lengo la kulipiza kisasi. Mjue Mbowe Ni kiongozi ambaye ana wafuasi wengi . Huwezi kujua kila mfuasi anawaza Nini kichwani.

Ushauri tu kwa jeshi la polisi kwa kuwa wameamua kuendesha kesi hii waruhusu wananchi wapate muendelezo wa hii kesi bila kuwawekea sababu za kuzuia. Ni Nini ajenda Yao kubwa kuzuia watu kufuatilia kesi ambayo Ni open for hearing? Wanahofia Nini wakati wao ndio walioshitaki?

Je, Siri Yao juu ya kuzuia itakapokuwa wazi watakimbilia wapi? Polisi Ni walinzi wa raia na Mali zao. Wabaki walinde pikipiki, magari na watu walihudhuria mahakamani na siyo kuingilia mahakama na kuwabughudhi watu wanaofuatilia kesi hii.
 
Sijana tumeandikiwa humu mtiriko wa mahojiano na kesi kuhairishwa hadi 24/09/21 hivi.
Ni kweli lakini ilikuwa baada ya mikwaruzano ya kutosha na kisha kuvishinda vikwazo hivyo ambavyo polisi hujaribu kuviweka kila siku...

Hata hiyo tarehe 24/9/2021 tegemea kuwa watakuja na mbinu mpya ya kujaribu kuzuia watu wasijue kuwa kumbe hawa polisi hawatekelezi majukumu yao kwa kufuata PGO inavyowaongoza, lakini bahati mbaya kwao ni kuwa WATASHINDWA TU...!

Yaani, their ignorance is completely EXPOSED....
 
Una ushahidi wa kesi ya ugaidi ambao Chifu Hang ya kishasema utaishangaza dunia, sasa iweje tena UHOFIE kesi hiyo isikilizwe na Watanzania LIVE? Kwanini UHOFIE ndugu, jamaa na marafiki kuingia mahakamani!? Unahofia ushahidi wako utabadilika au kuyeyuka!? Bado tuna safari ndefu sana Mkuu katika kupambana na hawa wahuni.

Ni kweli lakini ilikuwa baada ya mikwaruzano ya kutosha na kisha kuvishinda vikwazo hivyo ambavyo polisi hujaribu kuviweka kila siku...

Hata hiyo tarehe 24/9/2021 tegemea kuwa watakuja na mbinu mpya ya kujaribu kuzuia watu wasijue kuwa kumbe hawa polisi hawatekelezi majukumu yao kwa kufuata PGO inavyowaongoza, lakini bahati mbaya kwao ni kuwa WATASHINDWA TU...!

Yaani, their ignorance is already completely EXPOSED....
 
Kuna vitabu vya kufikirisha, kimoja Ni hadithi niliyoisoma kwenye muendelezo wa vitabu vya kiada vya kufundishia kiswahili elimu ya msingi. Kuna kinyozi alipewa kazi ya kumnyoa mfalme...
Hawawezi kuepuka aibu ambayo wameshaipata ikiwa rank ya RPC amechemka katika kutofahamu MWONGOZO WA KAZI ZAO wanataka tutarajie nini kutoka kwa konstebo???
 
Kuna vitabu vya kufikirisha, kimoja Ni hadithi niliyoisoma kwenye muendelezo wa vitabu vya kiada vya kufundishia kiswahili elimu ya msingi. Kuna kinyozi alipewa kazi ya kumnyoa mfalme...
Kwa kuwa simon sirro ana wish nchi yetu iwe na magaidi , subiri magaidi waje kweli halafu waanze na .....
 
Kuna vitabu vya kufikirisha, kimoja Ni hadithi niliyoisoma kwenye muendelezo wa vitabu vya kiada vya kufundishia kiswahili elimu ya msingi. Kuna kinyozi alipewa kazi ya kumnyoa mfalme. Kumbe mfalme alikuwa na masikio Kama ya punda. Siri hii ilijulikana tu na huyu kinyozi. Sharti ilikuwa Ni akivujisha tu Siri hii Basi hukumu yake ilikuwa Ni kunyongwa Hadi kifo...
Wanapata tabu sana kuumbuka hadharani.. Wanatamani angalau iwe gizani
 
Kosa kubwa lipo kwa chama tawala kiufupi ni ccm ndio mwenye kushikilia PGO,katiba ya zamani,keki ya taifa mpaka usalama TISS.

Chama kimekaa mda mrefu hakina jipya na bado kinazidi kutaka kushika hatamu ya nchi kwa njia yoyote bila kuangalia mbele kutakuwaje.

Chama kitakuja kuleta machafuko ambayo wenyewe imejitengenezea kwa tamaa za madaraka.

Chama kitakuja kutengeneza makundi ambayo sasa wenyewe wanajishtukia kuona mifano kama msumbiji,congo,sudani na nchi zengine.

Chama kinatumia mabavu ili kulinda vizazi vyao kwa njia yoyote.
 
Back
Top Bottom