PGO mwiba kwa maafisa wa Jeshi la Polisi, wanafanya kazi kwa taratibu zipi?

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,050
4,904
Wakuu, kulingana na mwenendo wa kesi inayoendelea mahakama kuu divisheni ya uhujumu uchumi, tumewashuhudia maafisa wa jeshi la Polisi wakionesha kutoifahamu vizuri PGO, kifaa ambacho wao wanakieleza kama nyenzo muhimu katika kazi zao.

Hii inaleta MASWALI mengi Sana, Ni kiwewe Cha kutoa ushahidi au hawana wanalolifahamu juu ya kile kilichoandikwa kwenye PGO.

Hawa watu wanafanyaje kazi zao bila kuelewa taratibu zinazotakiwa?

Imagine mtu ana cheo Kama RPC zen hajui kinachoendelea kwenye PGO? Wanateuliwa na kupewa vyeo hivyo kwa vigezo gani?

Hii ni aibu kwa Taifa!

___________________________________
Ushauri wangu:

Serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani iangalie kwa upya namna Bora ya kuwafundisha maafande waielewe PGO vizuri na kuweka katika matendo kile lilichoelekezwa ndani yake, sio kujificha kwa mgongo wa MAELEKEZO KUTOKA JUU, kumbe wako empty kichwani.
 
Back
Top Bottom