Mfahamu vizuri Bill Gates

nelly poul

nelly poul

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2015
Messages
1,270
Likes
901
Points
280
nelly poul

nelly poul

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2015
1,270 901 280
Bill Gates - (William Henry Gates III) Mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft, mtu tajiri sana duniani na mwanzilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali.

Bill Gates ni mwanzilishi, mwenyekiti na mbinifu mkuu wa programu za kampuni ya ya Microsoft, kampuni ya programu yenye mafanikio zaidi duniani, inayoaminika kwa utengenezaji wa programu zilizo na nguvu na ubunifu hali zikiwa bado zenye utumizi mwepesi. Microsoft sasa inaajiri zaidi ya watu elfu hamsini na tano katika nchi themanini na tano.

William Gates III H anajulikana kama Bill Gates alizaliwa tarehe 28 Oktoba 1955 na kulelewa katika kijiji cha Seattle pamoja na dada zake wawili. Katika umri wake mdogo Bill Gates alivutiwa na utengenezaji wa programu akiwa katika mojawapo wa shule kijijini Seattle. Akiwa huko shuleni Seattle, Bill Gates alikutana na Paul Allen, mwanafunzi mwenzake wakawa marafiki. Hapo ndipo wakaanza kutumia tarakilishi ndogo ya shule kujiendeleza ujuzi wao.

Walijiunga na kampuni ya kompyuta, malipo yao ikiwa ni kutumia tarakilishi yenye nguvu zaidi. Kazi yao ilikuwa ni kutafuta nukshi katika mitambo ya kompyuta, wakati huohuo waliweza kijifunza lugha mpya za kompyuta. Bill akaenda kwenye Chuo Kikuu cha Harvard. Kwa mara nyingine tena akajiunga pamoja na Paulo kuandika toleo jipya la programu ya Msingi wa lugha ya kwanza ya kompyuta ya kibinafsi, iitwayo Altair 8800.Kampuni hiyo iliridhishwa na kazi ambayo Bill Gates na Paul Allen waliofanya na programu hiyo ikapewa leseni. Jambo hili liliwachangia Gates na Allen Kuanzisha kampuni ya Microsoft, iliyokuwa ikitengenezea kampuni zingine programu. Bill Gates aliacha masomo yake katika chuo kikuu cha Harvard na kujishughulisha muda wake wote katika biashara.

Mapumziko yao yalikuja walipotengeneza mfumo wa kuendesha kompyuta uitwao MS-DOS uliotumika katika kompyuta ya kwanza ya kibinafsi ya IBM. Baadaye waliweza kuzishawishi kampuni zingine zinazotengeneza kompyuta kutumia mfumo huo wa MS-DOS. Mfumo huu mpya wa MS-DOS ulipata umaarufu katika soko miaka ya 1980 na baadaye, Microsoft pia ilianza kutengeneza programu kama vile neno sindikizi.

Microsoft ilitangaza mfumo mpya wa uendeshaji wa kompyuta uitwao Windows 1.0 mwaka wa 1983, ambao ulikuwa na grafiksi bora na pia uliwezesha kufanya zaidi ya jambo moja kwa wakati mmoja. Hata hivyo hakuwa bidhaa nyingine iliyotolewa miaka mbili baadaye hadi mwaka wa 1985, kwa kuwa ni programu chache zilizoweza kuendeshwa katika mfumo huu wa Windows 1.0. Hivyo mfumo huu mpya haukupata umaarufu vile.

Kipindi cha miaka mitano baadaye Microsoft ilitoa mifumo mipya ya Windows 2.0 iliyokuwa bora zaidi kuliko mifumo ya hapo awali. Kampuni ya Microsoft iliweza kupata umaarufu zaidi katika soko la hisa, na akiwa umri wa miaka 31, Bill Gates aliweza kuwa bilionea mchanga zaidi katika historia ya Marekani.

Katika mwaka wa 1990 Microsoft ikiongozwa na Bill Gates ilitoa toleo jipya la Windows liitwayo Windows 3.0 na kuboreshwa kiasi GUI. Toleo hili jipya liliweza kuuzwa zaidi ya nakala milioni kumi, likifuatiwa na matoleo mengine ya Windows 3.1, 3.11 na makundi ya kazi ambayo yaliongeza misaada kwa mitandao. Kutokana na mafanikio yao ya maendeleo, Microsoft ilitoa matoleo mengine ya Windows 95 ikifuatiwa na Windows 98, 2000, Millennium Edition na toleo la sasa Windows XP. Kila toleo jipya lilipotolea kampuni ya Microsoft ilizidi kupata umaarufu katika soko la hisa, ikiongezwa na baadhi ya programu kama vile Microsoft Office, michezo n.k. Umaarufu huu umemfanya Bill Gates kuwa mtu tajiri duniani myenye thamani ya wastani wa dola bilioni arubaini na sita.

220px-Bill_Gates_-_World_Economic_Forum_Annual_Meeting_Davos_2008.jpg
Bill_Gates_World_Economic_Forum_2007.jpg

Bill Gates pia ana maslahi katika biashara nyingine akiwa na nafasi nyingi za uwekezaji na vyeo katika kampuni tofauti ikiwemo Corbis Corporation, Berkshire Hathaway Inc, Teledesic Corporation. Mwaka wa 1998 Gates alijitoa jukumu lake kama Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Microsoft na kuzingatia maendeleo ya teknolojia na bidhaa mpya.

Bill Gates alifanya ndoa na Melinda French Gates mwaka wa 1994 na wakabarikiwa na watoto watatu, Jennifer, Rory na Fibi. Wote wawili Bill na Melinda ni waanzilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali. Waliweza kulianzisha shirika la Bill na Melinda Gates Foundation ambalo limeweza kuchangia zaidi ya dola bilioni tatu nukta mbili kuboresha afya duniani, dola bilioni mbili kuboresha fursa ya masomo kwa familia zisizojiweza. Zaidi ya hayo limeweza pia kuchangia dola milioni mia nne sabini na saba kwa miradi ya jamii na zaidi ya dola milioni mia nne themanini na nane kwa miradi maalum na kampeni za kuhamasisihwa kila mwaka.

Ubunifu wa Bill Gates wa kutengeneza programu umekuwa mchango wake katika mapinduzi ya kompyuta na sayansi ya kompyuta.
 
pwilo

pwilo

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Messages
3,354
Likes
856
Points
280
pwilo

pwilo

JF-Expert Member
Joined May 27, 2015
3,354 856 280
Watu wanataka udaku tu
 
talentboy

talentboy

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2011
Messages
1,774
Likes
1,396
Points
280
talentboy

talentboy

JF-Expert Member
Joined Jul 8, 2011
1,774 1,396 280
mkuu mbona uneishia kwenye windows xp tu...hizi windows 7,8 n 10 kwani sio za huyu jamaa?
 
Jonah

Jonah

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2011
Messages
584
Likes
244
Points
60
Jonah

Jonah

JF-Expert Member
Joined Dec 9, 2011
584 244 60
Huyo Paul Allen mbona hajawa tajiri kama mwenzake maana walianza nae pamoja ila mwisho anaonekana Gates mwenyewe ndio anaendesha kampuni
 
Gogle

Gogle

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2013
Messages
1,460
Likes
370
Points
180
Gogle

Gogle

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2013
1,460 370 180
Kijiji cha seattle?!
 
elmagnifico

elmagnifico

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2011
Messages
7,894
Likes
7,574
Points
280
Age
30
elmagnifico

elmagnifico

JF-Expert Member
Joined Jul 7, 2011
7,894 7,574 280
Huyo Paul Allen mbona hajawa tajiri kama mwenzake maana walianza nae pamoja ila mwisho anaonekana Gates mwenyewe ndio anaendesha kampuni
Ukitaja matajiri 20 wa dunia Paul hakosi.
Hiyo ni kawaida kwa maana hata apple anasikika steve jobs wakati kampuni hakuianzisha peke yake.
Bill gates ana bahati kwakuwa kipindi hicho microsoft ilikuwa kampuni ndogo tu wakati Gary Kildal alikuwa anamiliki OS inaitwa CP/M iliyokuwa inatumiwa na pc zote kasoro pc za apple.
Alikuwa tajiri sana, IBM walipotengeneza pc wakamcheki gates wakidhani ndiye mmiliki wa mp/c gates akawambia siyo yeye ila ni Gary.
Kumfuata Gary akazingua, wakarudi kwa gates kumuuliza kama ana OS.
Hakuwa nayo ila akawajibu anayo. Mwenzake Allen yeye alijua wapi pa kuipata.
Akamfuata jamaa anaitwa Peterson ambaye alikuwa ameunda os mfano wa cp/m akiita q-dos.
Microsoft wakainunua bila kumwambia deal lao na ibm.
Wakaibadili jina kuwa m-dos wakaingia mkataba na ibm kuwa itawekwa kwa kila pc itakapotumika watakula percent.
Pia mkataba hauwazuii ms kuwauzia wenzingine nao watumie.
Pc ya ibm ikaja kuwa standard for pc.
The rest is history Gary alipata stress sana
 
Lukwafya bhagasi

Lukwafya bhagasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2017
Messages
1,257
Likes
1,240
Points
280
Lukwafya bhagasi

Lukwafya bhagasi

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2017
1,257 1,240 280
Watanzania zaidi ya million 1 wanakula kupitia pesa ya huyo jamaa ikiwemo na serikali pia
 
N

nyukidume

Senior Member
Joined
Oct 18, 2017
Messages
166
Likes
97
Points
45
N

nyukidume

Senior Member
Joined Oct 18, 2017
166 97 45
Papaa Bill, Bill Gates!!
 
MarkHilary

MarkHilary

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2015
Messages
1,299
Likes
976
Points
280
MarkHilary

MarkHilary

JF-Expert Member
Joined Feb 8, 2015
1,299 976 280
Ukitaja matajiri 20 wa dunia Paul hakosi.
Hiyo ni kawaida kwa maana hata apple anasikika steve jobs wakati kampuni hakuianzisha peke yake.
Bill gates ana bahati kwakuwa kipindi hicho microsoft ilikuwa kampuni ndogo tu wakati Gary Kildal alikuwa anamiliki OS inaitwa CP/M iliyokuwa inatumiwa na pc zote kasoro pc za apple.
Alikuwa tajiri sana, IBM walipotengeneza pc wakamcheki gates wakidhani ndiye mmiliki wa mp/c gates akawambia siyo yeye ila ni Gary.
Kumfuata Gary akazingua, wakarudi kwa gates kumuuliza kama ana OS.
Hakuwa nayo ila akawajibu anayo. Mwenzake Allen yeye alijua wapi pa kuipata.
Akamfuata jamaa anaitwa Peterson ambaye alikuwa ameunda os mfano wa cp/m akiita q-dos.
Microsoft wakainunua bila kumwambia deal lao na ibm.
Wakaibadili jina kuwa m-dos wakaingia mkataba na ibm kuwa itawekwa kwa kila pc itakapotumika watakula percent.
Pia mkataba hauwazuii ms kuwauzia wenzingine nao watumie.
The rest is history Gary alipata stress sana
Duh
 
BLACK MARXIST

BLACK MARXIST

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2013
Messages
1,664
Likes
2,838
Points
280
Age
26
BLACK MARXIST

BLACK MARXIST

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2013
1,664 2,838 280
Ukitaja matajiri 20 wa dunia Paul hakosi.
Hiyo ni kawaida kwa maana hata apple anasikika steve jobs wakati kampuni hakuianzisha peke yake.
Bill gates ana bahati kwakuwa kipindi hicho microsoft ilikuwa kampuni ndogo tu wakati Gary Kildal alikuwa anamiliki OS inaitwa CP/M iliyokuwa inatumiwa na pc zote kasoro pc za apple.
Alikuwa tajiri sana, IBM walipotengeneza pc wakamcheki gates wakidhani ndiye mmiliki wa mp/c gates akawambia siyo yeye ila ni Gary.
Kumfuata Gary akazingua, wakarudi kwa gates kumuuliza kama ana OS.
Hakuwa nayo ila akawajibu anayo. Mwenzake Allen yeye alijua wapi pa kuipata.
Akamfuata jamaa anaitwa Peterson ambaye alikuwa ameunda os mfano wa cp/m akiita q-dos.
Microsoft wakainunua bila kumwambia deal lao na ibm.
Wakaibadili jina kuwa m-dos wakaingia mkataba na ibm kuwa itawekwa kwa kila pc itakapotumika watakula percent.
Pia mkataba hauwazuii ms kuwauzia wenzingine nao watumie.
Pc ya ibm ikaja kuwa standard for pc.
The rest is history Gary alipata stress sana
Gary alikua mzitooo
 
Forum statistics

Threads 1,237,857
Members 475,675
Posts 29,303,701