Mfahamu Ruby, mwanamke mweusi aliyesoma kwa tabu na ukandamizaji wa ubaguzi wa rangi huko nchini Marekani

Echazzy

Member
Jan 20, 2018
65
67
Ruby Bridges alizaliwa mnamo mwaka 1954 akiwa na umri wa miaka 6 alikuwa mtoto wa kwanza marekani mwenye asili ya Afrika alisoma katika shule mchanganyiko na wazungu.

Mtoto huyu aliteseka sana siku ya kwanza anaanza shule serikali kuu (federal government) nchini marekani waliamua kumlimda kila alipotembea dhidi ya wazungu watu wazima na watoto ambao walionesha nia ya wazi ya kumdhuru mtoto huyo.

Wazungu walisimama pembezoni mwa barabara kumuita mtoto Ruby ‘NIGGER’ wakimpa vitisho vya kumuua hata waliweza kutengeneza jeneza lenye mdoli mweusi ndani. Kitendo ambacho Ruby anasimulia kilimpa ndoto za kuweweseka sana usiku.

kutokana na shinikizo hilo walimu wote waliacha kazi kisa Ruby kasoro mmoja (pichani) tu ambaye ambaye alikubali kubaki kumsaidia (Wazungu wote sio wabaya).
Mwaka mzima Ruby alisoma darasa peke yake hata watoto wazungu waligoma kwenda shule kusoma na mtu mweusi.

Ruby akiwa shule hakuwa anakula chakula chochote akihofia kuwekewa sumu. Ila Ruby alisoma japo kwa tabu ikumbukwe marekani walianzisha sera ya kutoa elimu bila ubaguzi wa rangi (mchanganyiko) mnamo mwaka 1956 lakini bado weusi walio changanyika na wazungu walisoma kwa tabu sana.
hivi leo Ruby ana umri wa miaka 65 ni mwanaharakati wa haki za binadamu.
FB_IMG_1634511591506.jpg
FB_IMG_1634511586954.jpg
FB_IMG_1634511578928.jpg
FB_IMG_1634511570266.jpg
FB_IMG_1634511565866.jpg
 
Jana nilikua ninaangalia documentary 1000 years a slave. Jamani watu weusi waliteseka. Kule Jamaica Master anaekununua anakupiga mhuri wa moto usoni ili usiibiwe.
Mi huwa nawaza, hawa wazee hawakuhisi maumivu na kuwafanya washindwe hata kufanya kazi au kufa kabisa. Maana huku wakati wanachukuliwa walitobolewa miguuni na kufungwa minyororo halafu bado wanasafiri toka bara hadi pwani kwa miguu! Daa pole zao kwa kweli.
 
Unaambiwa mamilioni ya watumwa walifia safarini na anaekufa maiti inatupwa baharini. Mpaka papa walishajua kufuatilia meli maana walipata maiti za watu kama chakula.
 
Ruby Bridges alizaliwa mnamo mwaka 1954 akiwa na umri wa miaka 6 alikuwa mtoto wa kwanza marekani mwenye asili ya Afrika alisoma katika shule mchanganyiko na wazungu.

Mtoto huyu aliteseka sana siku ya kwanza anaanza shule serikali kuu (federal government) nchini marekani waliamua kumlimda kila alipotembea dhidi ya wazungu watu wazima na watoto ambao walionesha nia ya wazi ya kumdhuru mtoto huyo.

Wazungu walisimama pembezoni mwa barabara kumuita mtoto Ruby ‘NIGGER’ wakimpa vitisho vya kumuua hata waliweza kutengeneza jeneza lenye mdoli mweusi ndani. Kitendo ambacho Ruby anasimulia kilimpa ndoto za kuweweseka sana usiku.

kutokana na shinikizo hilo walimu wote waliacha kazi kisa Ruby kasoro mmoja (pichani) tu ambaye ambaye alikubali kubaki kumsaidia (Wazungu wote sio wabaya).
Mwaka mzima Ruby alisoma darasa peke yake hata watoto wazungu waligoma kwenda shule kusoma na mtu mweusi.

Ruby akiwa shule hakuwa anakula chakula chochote akihofia kuwekewa sumu. Ila Ruby alisoma japo kwa tabu ikumbukwe marekani walianzisha sera ya kutoa elimu bila ubaguzi wa rangi (mchanganyiko) mnamo mwaka 1956 lakini bado weusi walio changanyika na wazungu walisoma kwa tabu sana.
hivi leo Ruby ana umri wa miaka 65 ni mwanaharakati wa haki za binadamu.
View attachment 1977953View attachment 1977954View attachment 1977955View attachment 1977956View attachment 1977957
Harakati za mtu mweusi zimetoka mbali asee
 
Ubaguzi haujaisha, ila siku hizi unafichwa vizuri.
In the United States racism is rife!!! Kuishi Marekani usiambiwe, kunahitaji moyo; shuruba utakazopambana nazo hasa ukiwa mtu mweusi hujasoma na muhamiaji!!
 
Bora niendelee kuishi hapa kwa mtogole nisije uwa beberu la watu bure.
 
In the United States racism is rife!!! Kuishi Marekani usiambiwe, kunahitaji moyo; shuruba utakazopambana nazo hasa ukiwa mtu mweusi hujasoma na muhamiaji!!

Ubaguzi upo,hata kama wewe umesoma, umezaliwa Marekani.

Ni hivi, ni mindset ya kupewa elimu isiyo sahihi au kupotosha kwa malengo, ni muhimu kwao.

Kutumia education (elimu) or mis-education (upotoshaji wa kielimu) .

Kumuweka chini mtu mmoja (mzungu), juu mwingine (mweusi) kwa mipango maalum awe tegemezi, asiyejiamini, kujitambua, asiye na historia, mwenye historia ya unyonge, kutumika utumwa, kutawaliwa.

Kwamba hawezi, hajawahi kufanya, kuchangia, kuinufaisha dunia kwa chochote.

Ku-control image, jinsi mweusi anaona picha gani zikimuwakilisha, historia gani anaisoma, elimu gani anaipata, vitu gani anafikiri.
 
Bulesi
Ni kama hivi ukiwa supermarket you notice jamaa wanakufualitia sana kwemye CCTV au nyuma yako hasa ukiwa kijana mwanaume.

Ukiendesha gari ya gharama utasimamishwa sana na polisi.

Sheria hiyo hiyo akiivunja mweusi au mzungu adhabu ni tofauti.

Lazima uwe vizuri sana kwenye kazi yoyote kuliko wazungu kukupa madaraka makubwa.

US gov walieneza sana madawa ya kulevya crack cocaine& heroine miaka ya 1970's, 80's kuvunja nguvu ya kudai haki sawa kwa jamii yote, pia tasnia ya muziki ilielekezwa kuwa zaidi kwenye silly stuffs (mambo ya kijinga just sex, bitches, gold chain, cars,big houses,throwing money) badala ya kuwainua, kuwafanya weusi wengi wafikiri, kutafakari kwa kina.
 
Back
Top Bottom