Mfahamu mwanadada Diane Shima Rwigara wa Rwanda

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,875
Anaitwa Diane Shima Rwigara ,aliyezaliwa mwaka 1981 ,Kigali nchini Rwanda ,familia yake ni kabila la Watusi, Baba yake anaitwa Assinapol Rwigara,mama yake Adeline Rwigara ,kaka yake Aristide Rwigara na Mdogo wake wa kike ni Anne Rwigara.

Baba yake alikuwa mfuasi mkubwa wa chama Tawala cha Kagame ,Rwandan Patriotic Front(RFP),ndiye aliyekuwa akikisaidia kifedha baba yake alikuwa tajiri na mmiliki wa viwanda.ila alikufa Feb,4,2015 kwa ajali ya gari ila watu wengi na familia walisema aliuwawa kisiasa (Assassination).polisi walikana kuwa gari lake liligongana na Lori kubwa hakuwawa.

Diane alisoma high school Belgium, na vyuo kadha marekani California, ana shahada ya masuala ya fedha ,kutoka chuo cha Sacramento, US. Pia ana Master ya uhasibu katika chuo cha San Francisco nchini marekani.

Pia aliwahi kuwa mhadhiri idara ya lugha katika chuo cha Stanford.

Mnamo mwaka 2015,baada ya kifo cha Baba yake ndio ulikuwa mwanzo wa waziwazi Diane ,kumkosoa Kagame na uongozi wake bila woga na kudai hata baba yake hakupata ajali ila aliwawa kisiasa.na akaapa kupambana na uongozi dhalimu wa kagame usioheshimu haki za binadamu.

Kumbuka mwaka 2015 ,katika kipindi cha kupiga kura ya maoni (Referendum) kumruhusu au kukataa Kagame kuendelea kugombea ,Diane wazi wazi alikuwa akipinga kuwa Kagame amechoka ,hapaswi kuendelea na kiongozi mzuri ni yule anaondoka kwa heshima ,hivyo Kagame aondoke kwa heshima ila baada ya kura ,Kagame alipata kura nyingi za ndio kuwa ataendelea kugombea hadi 2034.

Mwaka 2017,Uchaguzi ulitangazwa kufanyika Agost 4,2017 ambapo mapema Mwezi Mei ,2017 Diane na yeye akatangaza kugombea Uraisi nchini Rwanda katika uchaguzi dhidi ya Rais Kagame .ambaye amekuwa katika nafasi ya urais Tangu 2000 ,baada ya mauwaji ya Halaiki ya 1994.

Masaa 72 baada ya Diane kutangaza kugombea uraisi kama Mgombea binafsi ,picha zake za uchi zilivuja na kusambaa mitandaoni ,ila aliapa kutokurudi nyuma ,kama alivyowahi kufanya mkutano wa vyombo vya habari na kusema ana nia ya kuondoa umaskini,uhuru wa kuongea,kupambana dhidi ya ugandamizwaji wa haki na demokrasia, kupambana dhidi ya uvunjifu wa haki za binadamu na kuleta mabadiliko makubwa.na hata katika Manifesto yake ya kuwania urais ndivyo alivyoahidi.

Ila bahati mbaya sana ,tar 7 ,Julai 2017 Tume ya uchaguzi ili muondoa katika kinyaganyiro hiko kuwa hajafuata sheria na hana vigezo tena ,kwani katika fomu yake ya kugombea alikuwa amefoji na saini kadhaa na hivyo kufanya saini 572 ambazo ni halali badala ya saini 600 ,ila Diane alipinga akasema amekusanya na kuwasilisha saini 958 ,ambazo nje ya 600 ambacho ni kiwango cha chini kuna za ziada saini zaidi ya 120.


Umoja wa ulaya walipinga sana kitendo hiko,pia Amnesty International,US department.

ila hatimaye aliondolewa na ikapelekea katika uchaguzi August 2017 ,Kagame kushinda 98 % ya kura.

Baada ya uchaguzi Diane alianzisha Kikundi cha kiharakati kiitwacho *The people salvation Movement for Change*
(kundi la ukombozi wa mabadiliko). alilenga ku challenge uongozi wa Kagame ,hasa katika suala la haki za binadamu.

Mapema August 30 ,2017 Kwao Diane Rwigara kulivamiwa na Police na kudai kuchunguza forgery na kukwepa kodi ,2017 sept ilidaiwa Diane kutoonekana ,na baadaye kuonekana mikononi mwa polisi na akafungulowa mashtaka ya uchochezi na ukwepaji kodi na forgery ,ambapo Dada na mama yake walionganishwa.

Mapema 2018,Mamlaka ya mapato Rwanda iliuza mashine yao ya Tumbaku (Tobacco) ili kufidia fedha ya kodi RWF 5 bilion (fedha Bill 5 ya Rwanda) sawa na $ 6 mil.)

Waliendelea kusota ndani ,wengine walitoka kwa dhamana mapema mwaka huu ila yeye alikuwa akiomba mara nyingi bila mafanikio tar 16 ,Nov 2017 Mahakamani ilitupilia mbali Rufaa yake ya kuomba Dhamana kwa sababu kuwa upande wa mashtaka wametoa sababu za msingi kuwa kesi inayowakabili ni kesi nyeti sana ya kodi.

Ila mapema leo Tar 5/October/2018 ,imeachiwa kwa Dhamana.

Ila watu wanajiuliza maswali je wataendelea kukosoa uongozi wa Kagame au watakaa kimya kutokana na machungu waliyopitia?

Imeandaliwa na

Abdul Nondo

abdulnondo10@gmail.com.
 
Bwana mdogo Nondo habari yako , hivi kile cheti cha kuzaliwa cha wazazi wa Bibi yako ulifanikiwa kukipeleka Uhamiaji ?
 
Kuwatoa sio sbb ya wao ama yeye kutokuendelea na mapambano, kwa sbb bado Rais kagame hajafanya malekebisho yoyote ya kuendesha serikali yake kwa misingi ya utawala bora.
 
Back
Top Bottom