Mfahamu mvumbuzi wa injini za boti (Outboard Engine)

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
4,946
12,513
Ole Envirude alizaliwa nchini Norway katika mji wa Gjøvik tarehe 19/04/1877 baada ya miaka 5 familia yake ilihamia nchini Marekani katika eneo la Cambridge, Wisconsin. Tangu utotoni alipendelea masuala ya makenika na alipofikisha miaka 16 alikuwa mtu wa mashine na muunda michoro.

CHANZO CHA UGUNDUZI

Ole Envirude alikuwa na wazo la kuanzisha kiwanda cha kutengeza injini ndogo za mlipuko wa ndani (internal combustion).

Katika maisha yake ya masuala ya uinjinia alikuwa na Msaidizi wake aliyefahamika kama Bessie Cary ambaye aliaminiwa na Ole kufanya kazi za kutunza kumbukumbu za biashara na kuwa msaidizi wake katika kiwanda chake.

SABABU YA OLE ENVIRUDE KUBUNI INJINI YA BOTI

Hadithi inayohusisha na ugunduzi ni Siku moja Ole alipokuwa na msaidizi wake Cary kwenye mapumziko katika ziwa
Okauchee, magharibi ya mji wa Milwaukee.

Umbali wa maili 2.5 ndio Cary akamwambia Envirude kuwa anatamani Ice Cream. Ikabidi Envirude achukue boti ya kutumia kasia kwa kipindi hicho na kwenda kufata Ice cream.

Kitendo cha kurudi Ice cream yote ilikuwa imeyeyuka na ndipo Envirude akashawishika kufanya uvumbuzi wa kutengeneza injini ndogo ya boti itakayo kuwa mbadala wa kasia.

MAISHA YA OLE ENVIRUDE

Mnamo mwaka 1906 walioana na Cary, mwaka 1907 Envirude alianzisha Envirude Motors katika mji wa Milwaukee. Kiwanda chake kilianza haraka kutengeneza injini ndogo yenye pistoni 1 na inayozalisha 1.5Hp ambayo ilipata mafanikio makubwa ya haraka ilipotambulishwa mwaka 1909.

Mwaka 1913 aliuza kampuni yake baada Afya ya mkewe kuwa mbaya na aliweka makubaliano ya kutotengeneza injini kwa miaka 5. Mwaka 1921 alitengeneza injini ya cylinder 2. Na akaanzisha kampuni ya ELTO Outboard Motor Company (Evinrude's Light Twin Outboard).

Mwaka 1929 Evinrude's Light Twin Outboard Outboard Motor Company iliungana na Envirude Motors na Lockwood Motor Company.

Mwaka 1928 mkewe alistaafu na akafariki mwaka 1933, pia mwaka huo huo Envirude akafariki nae na kampuni ikawa chini ya mtoto wao wa kiume Ralph.

1936 kampuni iliungana na Johnson Motor Company na kuitwa Outboard Marine Corporation, kipindi cha vita kuu ya pili ya dunia walitengeneza injini zilizotumika katika boti mbalimbali za kijeshi.

KAMPUNI KWA SASA

Mnamo mwaka 2000 kampuni ya Outboard Marine Corporation ilifilisika na mali zake kuchukuliwa na kampuni ya Bombardier Recreational Products ambao bado wanaendelea kutengeneza injini na bidhaa za Envirude.

Sasa wana injini za piston 1,2,3,4,6,8 pia ndio watengenezaji pekee wa injini za kisasa za Envirude E-Tec zisizo chafua mazingira na zenye nguvu kubwa zaidi ukilinganisha uwiano wa injini na uzito wa injini za nje za boti.

Envirude limekuwa jina kubwa sana duniani. Kwa kutambua mchango wake katika sekta ya boti za utalii,uvuvi na michezo kuna tuzo za Ole Evinrude Award, ambazo hutolewa katika mashindano ya New York Boat Show.

Wengi tumekuwa tukifahamu aina mbalimbali za makampuni ya Outboard engine lakini Ole Envirude ndio mvumbuzi.
Sasa kuna makampuni kama Suzuki,Yamaha,Honda,Mercury na Tohatsu.

"SEA NEVER DRY"

images.jpeg
 
Back
Top Bottom