kina kirefu
JF-Expert Member
- Dec 14, 2018
- 18,481
- 23,070
ndo Ile van anakula uhondo au nyingineNimekumbuka muvi ya no where to run ya vandame, mwamba alikuwa hatari, akiwa, anaelezea muvi za, kivita
ndo Ile van anakula uhondo au nyingineNimekumbuka muvi ya no where to run ya vandame, mwamba alikuwa hatari, akiwa, anaelezea muvi za, kivita
Kama kawa kama dawa kama kawaidaz naitwa dj mark g machine kutoka pande za acheche production"Naitwa captain Gaspar Derrick Mkandala a.k.a Rufufuuuuu"
Jamaa alikuwa mwongo sana Ila alijua kucheza na maneno Hadi muvi unaiona tamu
Lkn kwangu DJ Mark Mzee wa acheche production namkubali zaidi
Akajamba pupupu, akamwagiwa mwaniiii au korosho, akalia hapo analia amrish kapur ng'oho ng'oho.Anaitwa Kapteni Gaspa Derrick Mkandala Lufufu, halafu mbele hapo kuna maneno ya kihaya alipenda kuyaweka Mnaokumbuka vyema Mtatukumbusha.
Baada ya kustaafu kazi ya Jeshi Lufufu aliamua kuanza kutafsiri picha (Movie) za kizungu nk. kwa Kiswahili, jina lake likawa maarufu hapa Nchini Tanzania huku akiwa mtu wa kwanza kabisa kuingiza maneno ya kiswahili kwenye mikanda ya video VHS.
Huyu muasisi wa MaDj wote unaowaona wanatamba hivi sasa alifariki Mwaka 2015 na kuzikwa Moshi Mkoani Kilimanjaro. Baba yake alikuwa Mchaga na mama yake alikuwa Mhaya.
Alikuwa akinogesha movie kwa maneno yake ambayo hatuyajui maana yake mpaka leo ila wapenzi watazamaji walimwelewa.
"Eeeee Tujuane wale wote wa vibanda umiza kipindi kileee tulio kuwa tukirudi tunafikia kwenye kichapo na maji ya baridi juu. watoto wa getini mtupishe kidogo "
Unaikumbuka muvi ipi kutoka kwa huyu mkali....View attachment 2242541
Uchungu wa nyanya chungu ndo utamu wake mkuuMzee wa kamnyweso, makagari, akamchoma Uswadi, anataka kumtafuna uroro, Indaa!!!
Msimsahau Dj Afro Amigo.
Rufufu nimuongo alikua anaelezea matukio badala ya kutafsiri maneno.
Kwangu Dj Mack na Dj Afro ndio the best wanajua kingereza vizuri na hawachoshi kuwasikiliza
First blood sehemu ya kwanza hiyo mkuuu"Rambo utanipeleka Marekani?"
"Rambo kula chakula."
"Unajua sisi makomandoo tunapokuwa kwenye uwanja wa kivita tunakula mara moja kwa siku hatuli tu hovyo hovyo."
Hapa ni kumbukumbu za zamani huyu mwamba ni shujaa wetu enzi hizoMtu mzima unaanzaje kuangalia movie iliotafsiriwa kwa kuingiza sauti? Hizo movie huwa naona hazina tofauti na katuni za watoto za akina Kibena.