Mfahamu "Mkandala Rufufu" mzee wa kukotola

Mfahamu "Mkandala Rufufu" mzee wa kukotola

Mzee wa kamnyweso, makagari, akamchoma Uswadi, anataka kumtafuna uroro, Indaa!!!
Msimsahau Dj Afro Amigo.
Rufufu nimuongo alikua anaelezea matukio badala ya kutafsiri maneno.

Kwangu Dj Mack na Dj Afro ndio the best wanajua kingereza vizuri na hawachoshi kuwasikiliza
Mkuu hapa ni kama umeongea kinyume, hao kina Mack ndio wanasimulia matukio.
 
alikuwa akinikosha akiigiza sauti ya kike, amkumbuka kwenye movie la titanic
"Rambo utanipeleka Marekani?"

"Rambo kula chakula."

"Unajua sisi makomandoo tunapokuwa kwenye uwanja wa kivita tunakula mara moja kwa siku hatuli tu hovyo hovyo."
 
Huyu mtu watu wanampenda sana lakini binafsi kwenye kizazi changu cha filamu nimekuta wakina dj mack na juma khan
 
Mkandala lufufu, lukoma abembeija kanshumika bilagala kankoma bigutuka kutoka mitaa ya hamghembe
 
Mimi Lufufu ndo GOAT wangu hata hizi enzi za Netflix mara moja moja nilkua natafuta movie zake za kibeto
 
Mkandala alkuwa na above all DJs. Kwanza ana sauti zote
Mzee , mwenye nye mapengu, mtoto, teja n. K.

Kuna ile move ya Dragon Bridge ya Dolph Landgreen jamaa walio mteka yule princeses jamaa flan lenye mapengu.
Hakaf wakuu hivi ile movie ya movie ya mtoto can inaitwaje?.
 
alikuwa anafanya makosa sema nchi yetu huwa haifuatilii mambo ya hati miliki za kisanii
Huwezi tafsiri kitabu au picha ya senema yeyote bila idhini ya mtunzi.
Aya kamkamte, hii ni kama gari tu inakuja pickup inatoka WARBUS basi na Toyota nao watushtaki
 
Kazi za DJ Macky ntazipata mtandaoni sehemu gani ? Nyingi zilizopo wanamuiga tu huku wakiwwka Title Ni yeye
Mcheki kwa namba yake anakutumia mwenyewe bila shida, tena pendekeza hata mamuvi makali unayotaman yarejelewe aseeh noma sana
 
Anaitwa Kapteni Gaspa Derrick Mkandala Lufufu, halafu mbele hapo kuna maneno ya kihaya alipenda kuyaweka Mnaokumbuka vyema Mtatukumbusha.

Baada ya kustaafu kazi ya Jeshi Lufufu aliamua kuanza kutafsiri picha (Movie) za kizungu nk. kwa Kiswahili, jina lake likawa maarufu hapa Nchini Tanzania huku akiwa mtu wa kwanza kabisa kuingiza maneno ya kiswahili kwenye mikanda ya video VHS.

Huyu muasisi wa MaDj wote unaowaona wanatamba hivi sasa alifariki Mwaka 2015 na kuzikwa Moshi Mkoani Kilimanjaro. Baba yake alikuwa Mchaga na mama yake alikuwa Mhaya.

Alikuwa akinogesha movie kwa maneno yake ambayo hatuyajui maana yake mpaka leo ila wapenzi watazamaji walimwelewa.

"Eeeee Tujuane wale wote wa vibanda umiza kipindi kileee tulio kuwa tukirudi tunafikia kwenye kichapo na maji ya baridi juu. watoto wa getini mtupishe kidogo "

Unaikumbuka muvi ipi kutoka kwa huyu mkali....View attachment 2242541
Nimekumbuka muvi ya no where to run ya vandame, mwamba alikuwa hatari, akiwa, anaelezea muvi za, kivita
 
Wasanii wetu masikini, wewe ni tajiri?
Ndio ni masikini ila mimi ni masikini kuliko wao.
Najua una fikira labda za kumtetea Diamond na wengine
Ni kweli kwa viwango vya kwetu tunamuona Diamond ni tajiri
Ila ni ukweli ulio wazi nchi yetu sheria ya hati miliki haizingatiwi ipasavyo
Diamond na wengine ingekuwa nchi zingine utajiri wake ungekuwa ni mkubwa zaidi ya hapo kama walivyokuwa kina Michael Jackson
Siandiki haya kuwakandia ila ni kuwatetea
 
Leo umemkumbuka baba Ako unamuezi kivingine

nilipigwa sana kwajili ya huyu dingiyako we jingasana KABURi mlishajengea au bado
 
Back
Top Bottom