Mfahamu Mh. William Mganga Ngeleja

Mfahamu Mh. William Mganga Ngeleja

Hata Yesu, alizomewa na wayahudi lakini Mwisho wa siku aliwakomboa.
Kazi aliyofanya akiwa Waziri inajulikana na wataalamu wanasema Ngeleja ni Baba wa Nishati na Nadini.
Mbona wewe ulikuwa kambi ya Membe? Kwani Membe ni rafiki yake Magufuli.
Nakushauri uendele kula mahindi, kubeba maboksi ili upate ujira dogo.
teh teh naona umeshanibatiza kambi ya membe, CCM bana mnawaza kambi daily.

Ngeleja kafanyia taifa hili kitu gani mpaka cha kukumbukwa??

Ngeleja is a crap dogo, punguza mahaba kwenye siasa
 
Amekutuma uweke CV yake hapa ili iweje? Anaomba kazi gani kwetu? Au JF wanaajiri? Si ungetuma kwao moja kwa moja? kama unampigia debe humu kwa ajili ya ajira ya awamu ya 5 sidhani kama itamsaidia kwani hizo sio za Magufuli!
 
Amekutuma uweke CV yake hapa ili iweje? Anaomba kazi gani kwetu? Au JF wanaajiri? Si ungetuma kwao moja kwa moja? kama unampigia debe humu kwa ajili ya ajira ya awamu ya 5 sidhani kama itamsaidia kwani hizo sio za Magufuli!
Huyu dogo anahangaika tu mkuu.

Magufuli hawezi fanya kazi na mtu kama Ngeleja, ni mtu wa madili feki sana na mpenda misifa, ni type za kina JK na Nyalandu
 
Kwi kwi kwi. Kuna nini hasa? Tulisoma CV zao wote hususan wakati wa mbio zao za kuutafuta urais. Leo unatuletea na kuanza kujijibu mwenyewe, kulikoni?
Wapo watu chungu nzima wenye CV nzuri kupita hii ya Ngeleja, lkn haziletwi hapa kwakuwa hatuna mahitaji nazo kwa sasa.

Kwa hiyo nakusihi muanzisha uzi, uache ushankupe.
 
Tujifunze kusikia tusuio penda ili tujifunze, lengo la Uzi huu ni watanzania wamfahamu Mbunge wa jimbo la sengerema na si vinginevyo tukumbuke Ngeleja ni role model ya vijana wengi hapa nchini

Sio kosa kuweka CV ya kiongozi ambaye ni role model wa Vijana.
 
Huyu dogo anahangaika tu mkuu.

Magufuli hawezi fanya kazi na mtu kama Ngeleja, ni mtu wa madili feki sana na mpenda misifa, ni type za kina JK na Nyalandu
Mh. Ngeleja alifanikisha mchakati wa
kupata Sera mpya ya Madini mwaka 2009.
} Mh. Ngeleja alifanikisha mchakato wa
kupata Sheria mpya ya mwaka 2010.
Baadhi ya mambo mapya na muhimu
yalioingizwa katika Sera na Sheria mpya ya
madini ni pamoja na;-
a\ Sharti la Serikali kumiliki hisa za bure
katika migodi(free carried interest), mfano
migodi wa Buckreef Geita, Serikali inamiliki
hisa za bure 45℅ kupiti STAMICO,
Mchuchuma/ Liganga(NDC 20%) Na ngaka
(NDC 30%).
b/ Migodi yote inatakiwa kununua Huduma
na bidhaa mbalimbali nchini badala ya
kuagiza kutoka nje kama ilivyokuwa awali.
c/ Kipindi cha leseni za wachimbaji wadogo
kimeongezwa kutoka 5-7.
d/ Viwango vya mrabaha vimeongezeka, kwa
mfano, dhahabu kwa sasa ni 4% badala ya
3%(migodi ilianza kulipa mrabaha mpya Mei
1, 2012).
} Mh. Ngeleja alisimamia kuifufua STAMICO
mwaka 2008, awali ilikuwa imeorodheshwa
kufutwa kabisa.
} Mh. Ngeleja alisimamia kumpata mwekezaji
katika mgidi wa Makaa ya Mawe na Chuma
wa Mchuchuma/Liganga kwa kushirikiana na
NDC mwaka 2007-2011.
} Mh. Ngeleja alisimamia kuurudisha mgodi
wa kiwira mikononi mwa serikali kupitia
STAMICO Mwaka 2009/11.
} Mh. Ngeleja alisimamia kampuni za madini
kuanza kulipa kodi ya mapato (30℅) mfano,
resolute (Nzega), Geita Gold Mine (Geita),
Tulawaka (Biharamulo) na TanzaniaOne
(Mererani).
} Mh. Ngeleja alihakikisha maeneo zaidi kwa
ajili ya wachimbaji wadogo yanatengwa na
serikali.
} Mh. Ngeleja aliasisi utaratibu wa Mfuko
Maalum wa kusaidia wachimbaji wadogo
nchini.
} Mh. Ngeleja alipiga marufuku usafirishaji
nje ya nchi wa madini ghafi ya Tanzanite
yenye ukubwa unaozidi gramu 1, mwaka
2010 April.
} Mh. Ngeleja ni Muasisi wa utaratibu wa
kutoa hati ya uasili( Certificate of Origin) kwa
wanaouza madini ya Tanzanite.
} Mh. Ngeleja alisimamia uanzishwaji wa
wakala wa ukaguzi wa Migodi, Tanzania
Mineral Audit Agency (TMAA). Mwaka 2009.
Nb; manufaa ya wakala huu yanajulikana.
} Mh. Ngeleja alisimamia mchakato wa
Tanzania kujiunga na tasnia ya uziduaji
duniani (EITI) kuanzia mwaka 2009.
} Mh. Ngeleja alisimamia kuhamishwa kwa
kitengo cha kukata almasi (TRASORT) kutoka
Uingereza na kuhamia nchini mwezi agosti
mwaka 2010.
 
Mh. Ngeleja alifanikisha mchakati wa
kupata Sera mpya ya Madini mwaka 2009.
} Mh. Ngeleja alifanikisha mchakato wa
kupata Sheria mpya ya mwaka 2010.
Baadhi ya mambo mapya na muhimu
yalioingizwa katika Sera na Sheria mpya ya
madini ni pamoja na;-
a\ Sharti la Serikali kumiliki hisa za bure
katika migodi(free carried interest), mfano
migodi wa Buckreef Geita, Serikali inamiliki
hisa za bure 45℅ kupiti STAMICO,
Mchuchuma/ Liganga(NDC 20%) Na ngaka
(NDC 30%).
b/ Migodi yote inatakiwa kununua Huduma
na bidhaa mbalimbali nchini badala ya
kuagiza kutoka nje kama ilivyokuwa awali.
c/ Kipindi cha leseni za wachimbaji wadogo
kimeongezwa kutoka 5-7.
d/ Viwango vya mrabaha vimeongezeka, kwa
mfano, dhahabu kwa sasa ni 4% badala ya
3%(migodi ilianza kulipa mrabaha mpya Mei
1, 2012).
} Mh. Ngeleja alisimamia kuifufua STAMICO
mwaka 2008, awali ilikuwa imeorodheshwa
kufutwa kabisa.
} Mh. Ngeleja alisimamia kumpata mwekezaji
katika mgidi wa Makaa ya Mawe na Chuma
wa Mchuchuma/Liganga kwa kushirikiana na
NDC mwaka 2007-2011.
} Mh. Ngeleja alisimamia kuurudisha mgodi
wa kiwira mikononi mwa serikali kupitia
STAMICO Mwaka 2009/11.
} Mh. Ngeleja alisimamia kampuni za madini
kuanza kulipa kodi ya mapato (30℅) mfano,
resolute (Nzega), Geita Gold Mine (Geita),
Tulawaka (Biharamulo) na TanzaniaOne
(Mererani).
} Mh. Ngeleja alihakikisha maeneo zaidi kwa
ajili ya wachimbaji wadogo yanatengwa na
serikali.
} Mh. Ngeleja aliasisi utaratibu wa Mfuko
Maalum wa kusaidia wachimbaji wadogo
nchini.
} Mh. Ngeleja alipiga marufuku usafirishaji
nje ya nchi wa madini ghafi ya Tanzanite
yenye ukubwa unaozidi gramu 1, mwaka
2010 April.
} Mh. Ngeleja ni Muasisi wa utaratibu wa
kutoa hati ya uasili( Certificate of Origin) kwa
wanaouza madini ya Tanzanite.
} Mh. Ngeleja alisimamia uanzishwaji wa
wakala wa ukaguzi wa Migodi, Tanzania
Mineral Audit Agency (TMAA). Mwaka 2009.
Nb; manufaa ya wakala huu yanajulikana.
} Mh. Ngeleja alisimamia mchakato wa
Tanzania kujiunga na tasnia ya uziduaji
duniani (EITI) kuanzia mwaka 2009.
} Mh. Ngeleja alisimamia kuhamishwa kwa
kitengo cha kukata almasi (TRASORT) kutoka
Uingereza na kuhamia nchini mwezi agosti
mwaka 2010.
Wewe ni wa kupuuza.

Na kwa kuwa posti hii imeletwa siku ya wajinga duniani, huna budi kupuuzwa tu kwa sababu haya unayoandika hapa ni ujinga mtupu, na bahati mbaya sana na wewe unajua kuwa huu ni ujinga ila siku ya leo inakubeba
 
Huyu dogo anahangaika tu mkuu.

Magufuli hawezi fanya kazi na mtu kama Ngeleja, ni mtu wa madili feki sana na mpenda misifa, ni type za kina JK na Nyalandu
Kumbuka Jk ndio kakupa ujira wa kula mahindi Iringa.
 
Kumbuka Jk ndio kakupa ujira wa kula mahindi Iringa.
He he he
Sijawahi kuishi ringa dogo, punguza kukurupuka.

Halafu haya mahaba kwa Ngeleja umeyaanza lini??

Sio tabia nzuri ujue kuweka CV ya mwanamume mwenzio mtandaoni otherwise anakulipa au una mahaba naye
 
Tatizo la Ngeleja NI FISADI KABISA,ni nani asiyejua hilo?
 
kitu pekee ambacho Ngereja ana faidika nacho ni umasikini wa Hali ya juu unao wakabili wakazi wa jimbo la Sengerema. uzuri wa CV yake umewasaidia nini wakazi wa Sengerema? kwa kifupi pasipo kutumia rushwa asingeshinda kura za maoni 2015.
 
HISTORIA YAKE:
William Mganga Ngeleja alizaliwa Oktoba 5, 1967 mkoani Mwanza, ana miaka 48 alitimiza mwezi Oktoba mwaka jana.

Ngeleja alisoma katika Shule ya Msingi Bitoto mwaka 1976 – 1982 kabla ya kuelekea mkoani Dodoma kwa masomo ya kidato cha kwanza mpaka cha nne katika Shule ya Sekondari Mpwapwa kati ya mwaka 1983 –1986.

Baada ya kufaulu vizuri aliendelea na masomo ya kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Ihungo mkoani Kagera kati ya mwaka 1987 – 1989.

Ngeleja alifaulu vizuri masomo yake na akajiunga moja kwa moja Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) sehemu ya Mlimani akichukua kozi ya sheria mwaka 1991.
Alihitimu na kutunukiwa shahada ya kwanza ya sheria (LLB) mwaka 1994 na kuajiriwa serikalini kama Mwanasheria wa Serikali mwaka 1994–1996. Ngeleja aliamua
kujiendeleza zaidi, akarejea UDSM mwaka 1996 kusomea shahada ya uzamili ya sheria
(LLM) na kuhitimu mwaka 1999.


Kati ya mwaka 1995 hadi 2000 Ngeleja pia alifanya kazi na kampuni maarufu ya uwakili duniani ya Price WaterHouse Coopers, ambayo ina matawi mengi ulimwenguni ikiwamo Tanzania.
Mwaka 2000 aliacha kazi Price WaterHouse Coopers na kujiunga na kampuni ya Vodacom ambako alifanya kazi kama mwanasheria wa kampuni, kwa miaka mitano, hadi 2005.


Katika kipindi chote hiki Ngeleja aliendelea na kazi huku akikisaidia chama chake, CCM, katika masuala mbalimbali na wakati huohuo akifikiria kuingia katika siasa za ushindani.

MBIO ZA UBUNGE
Safari ya kuusaka ubunge aliianza mwaka 2005 alipojitosa kuomba ridhaa ya ubunge
katika Jimbo la Sengerema; akapita mchujo wa kura za maoni na kuwa mgombea wa CCM.

Kwenye uchaguzi alikumbana na Essau Balalukuliliza Pelece wa UDP, Stella Cosmas Chetto wa CUF na Joshua Zebrone Subi wa Chadema akawashinda kwa kupata asilimia 69.3 ya kura zote. Baada ya kuwa mbunge alitumikia nafasi hiyo, kwa mwaka mmoja, kabla yakuongezewa wadhifa wa unaibu waziri katika Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, kwenye wizara ya Nishati na Madini kutokea Januari 2007 hadi Agosti 2008.

Mwaka 2008 kulipofanyika mabadiliko katika Baraza la Mawaziri, baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Ngoyayi Lowassa kujiuzulu kutokana na kashfa ya Richmond, Rais Kikwete aliunda Baraza la Mawaziri jipya na kukuza “ngekewa” ya Ngeleja ambaye alipewa uwaziri kamili wa Nishati na Madini kukamilisha miaka miwili iliyokuwa imebakia kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwkaa 2010. Mwaka 2010 Ngeleja alijitosa tena kwenye kinyang’anyiro cha ubunge kutetea nafasi yake; alishinda kura za maoni na kwenye uchaguzi wenyewe akawa hana mpinzani, yaani wagombea wa upinzani waliingia “mitini” na kumpa “zawadi ya ushindi”.

Baada ya kupita bila kupingwa aliteuliwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini, nafasi
aliyoitumikia hadi Juni 2012 mwaka ambao Rais Kikwete alifanya mabadiliko madogo kwenye Baraza la Mawaziri na Ngeleja hakubahatika kuwepo.

Nafasi yake ilichukuliwa na Profesa Sospeter Muhongo. Pamoja na kuwa nje ya uwaziri, safari yake kisiasa iliendelea kukumbwa na mawimbi mengi. Mwanzoni mwa mwaka jana,
alilazimika kuachia ngazi katika nafasi ya uenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala kutokana na kuwa miongoni mwa viongozi waliopokea mgawo wa fedha zilizochukuliwa kutoka kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.

Alipoitwa kujieleza kwenye Tume ya Maadili, Ngeleja alikiri kuwekewa shilingi 40.4milioni na mmiliki wa Kampuni ya VIP Engineering & Marketing, James Rugemalira lakini mwenyewe alisisitiza kuwa fedha hizo hazikuwekwa kwa nia mbaya. Na kibaya Zaidi yeye mwenyewe hakutoa taarifa kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.


MBIO ZA URAIS

Ngeleja ni mmoja wa watu waliotajwa sana kama watu wanaomuunga mkono Lowassa katika safari ya kuisaka Ikulu tangu alipokuwa Waziri Mkuu chini ya Rais Kikwete na hata
baada ya kujiuzulu nafasi hiyo mwaka 2008.
Na hata Ngeleja alipoteuliwa tena kuwa Waziri wa Nishati na Madini, mara baada ya kuteuliwa kwa mara ya pili Januari 2011, ilisemekana kuwa anamuunga mkono waziri mkuu huyo aliyejiuzulu. Lakini katikati ya mwaka 2013, inasemekana wanamtandao wa urais katika kundi la Lowassa wanaotokea Kanda ya Ziwa, waliona vema kumuibua mgombea anayeweza kuungwa mkono kutoka kanda yao na ndipo akainuliwa Ngeleja.

Katika harakati za chini kwa chini akawa miongoni mwa makada sita walionaswa na chama wakifanya kampeni za siri na wakazuiwa kwa miezi 12 kuanzia Februari mwaka juzi. Kamati ya Maadili inaendelea kuwachunguza.

Hata harakati zake za kuwapigania wachimbaji wadogowadogo wapate maeneo zaidi kwa ajili ya uchimbaji, kuwaanzishia mfuko maalum wa kuwasaidia, kupiga marufuku usafirishaji wa madini ghafi kwenda nje ya nchi, na hatua kama hizo, zilikuwa zinahusishwa na mbio hizo hasa kwa kuzingatia kuwa maeneo yenye madini yana wapigakura wengi sana. Hata hivyo, jambo hilo halijathibitishwa.


Watu walio karibu naye, miongoni mwao wakiwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, wanasema kwamba yeye huwa anajinasibu kuwa anaweza kuwa chaguo mbadala makada maarufu watakapokatwa majina yao kipindi cha mchakato we urais CCM.


NGUVU ZAKE
Ngeleja amewahi kuwa karibu sana na Lowassa, Kwa hiyo, anaujua vizuri mtandao wa ushindi ndani ya CCM hasa kwa sababu alishiriki pia shughuli kama hiyo wakati wa kumpigania Kikwete mwaka 2005.

Jambo hili linampa nguvu kubwa. Nguvu nyingine ya Ngeleja inatokana na umri wake, kwani anaonekana bado kijana sana. Ikiwa CCM itahitaji mgombea
mwenye umri wa “usasa” na ambaye ana kaliba inayoweza kuwavutia vijana na watu wengine, Ngeleja atakuwa miongoni mwa watu wenye sifa hiyo.


Tukija katika uzoefu, eneo hili pia linampa Ngeleja nguvu kubwa. Tangu mwaka 1994 Ngeleja ameweza kutumika serikalini na katika mashirika binafsi na ya kimataifa kama mwanasheria. Uzoefu huo una maana kuwa anaifahamu vizuri nchi na mazingira ya kazi katika sekta ya umma na sekta binafsi. Hakika kigezo hiki kinampa nguvu ya kipekee tofauti
na wagombea wengine ambao labda wamewahi kufanya kazi serikalini tu. Nguvu nyingine ya Ngeleja inapatikana kwenye taaluma yake. Sheria ni taaluma ya “kipekee” na ina tofauti kubwa sana na masomo ya sanaa. Mara nyingi viongozi wanasheria wanatarajiwa kujiamini na kutenda masuala ambayo yanaweza kutohojiwa kirahisi. Ikiwa itachukuliwa kwa mtazamo huo na kwamba CCM inahitaji msomi mzuri mwenye taaluma ya kipekee na inayoweza kumfanya mtu afanye kazi katika mazingira yoyote kwenye sekta nyingine, basi Ngeleja atakuwa miongoni mwa wanaofuzu.

HITIMISHO
Naona kama Ngeleja atakuwa na wakati mzuri sana kisiasa huko mbeleni, cha msingi aendele kuwa mkimya na mchapa kazi.
Jisifu tu lakini hiyo siyo historia ya maana sana kuisaidia nchi. hata hivyo hebua angalieni:
https://www.jamiiforums.com/members/ajol.345112/
Ajol JF-Expert Member

Joined😀ec 22, 2015

Kafuata mwingine:
Kumbe jamaa ana CV nzuri hivi..... Sikujua kabisa
Huyu naye:
Njaro Member
Joined:Mar 19, 2016
Mwingine kaja na kusema haya:
what a great CV

Mbona munasifu wale wale na kurudishiana maswali? Sponsored for political gain? Nyota imeshachafuka ndugu zangu. Hiyo munayoita CV haitusaidii sana maana hana mafanikio ktk uendeshaji wa serikali.
 
Ina maana dalili zimeonekana kwamba Magufuli amefeli mpaka watu wanaanza kutangaza nia mapema hivi?
 
NGELEJA ni Jembe kutoka Sengerema.
Wewe acha upuuzi huyu ngeleja in jizi tu pale sengerma hakuna Maji mpaka tasisi za umma, still unasema jembe kivipi? nn kakifanya pale Zzaidi ya wizi?
 

Tena hili ni FISADI lililokubuhu; limeiba sana likiwa pale wizara ya Nishati kiasi kwamba lilikwenda kununua BENZ pale D.T. dobie kwa bei mbaya lakini mara gari lilipowasili ,hili fisadi likaogopa kwenda kulichukua hilo gari na gari likakaa pale mwaka mzima!!! Hivi sasa nadhani hilo gari limefichwa mahali au hata ameliuza kwa kuogopa kuulizwa!! Mwizi mkubwa huyu hata kwenye ESCROW alikuwemo!!! Huyu ni boi mkuu wa fisadi Rostam Azizi.
 
Kilichochafua CV yake ni huu wizi wa pesa za uma uliofanywa kupitia ESCROW....mwambie afute ndoto ya kuwa Rais wa nchi hii.
 
Back
Top Bottom