Mfahamu Mh. William Mganga Ngeleja

Ajol

Senior Member
Dec 22, 2015
140
75
HISTORIA YAKE:
William Mganga Ngeleja alizaliwa Oktoba 5, 1967 mkoani Mwanza, ana miaka 48 alitimiza mwezi Oktoba mwaka jana.

Ngeleja alisoma katika Shule ya Msingi Bitoto mwaka 1976 – 1982 kabla ya kuelekea mkoani Dodoma kwa masomo ya kidato cha kwanza mpaka cha nne katika Shule ya Sekondari Mpwapwa kati ya mwaka 1983 –1986.

Baada ya kufaulu vizuri aliendelea na masomo ya kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Ihungo mkoani Kagera kati ya mwaka 1987 – 1989.

Ngeleja alifaulu vizuri masomo yake na akajiunga moja kwa moja Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) sehemu ya Mlimani akichukua kozi ya sheria mwaka 1991.
Alihitimu na kutunukiwa shahada ya kwanza ya sheria (LLB) mwaka 1994 na kuajiriwa serikalini kama Mwanasheria wa Serikali mwaka 1994–1996. Ngeleja aliamua
kujiendeleza zaidi, akarejea UDSM mwaka 1996 kusomea shahada ya uzamili ya sheria
(LLM) na kuhitimu mwaka 1999.


Kati ya mwaka 1995 hadi 2000 Ngeleja pia alifanya kazi na kampuni maarufu ya uwakili duniani ya Price WaterHouse Coopers, ambayo ina matawi mengi ulimwenguni ikiwamo Tanzania.
Mwaka 2000 aliacha kazi Price WaterHouse Coopers na kujiunga na kampuni ya Vodacom ambako alifanya kazi kama mwanasheria wa kampuni, kwa miaka mitano, hadi 2005.


Katika kipindi chote hiki Ngeleja aliendelea na kazi huku akikisaidia chama chake, CCM, katika masuala mbalimbali na wakati huohuo akifikiria kuingia katika siasa za ushindani.

MBIO ZA UBUNGE
Safari ya kuusaka ubunge aliianza mwaka 2005 alipojitosa kuomba ridhaa ya ubunge
katika Jimbo la Sengerema; akapita mchujo wa kura za maoni na kuwa mgombea wa CCM.

Kwenye uchaguzi alikumbana na Essau Balalukuliliza Pelece wa UDP, Stella Cosmas Chetto wa CUF na Joshua Zebrone Subi wa Chadema akawashinda kwa kupata asilimia 69.3 ya kura zote. Baada ya kuwa mbunge alitumikia nafasi hiyo, kwa mwaka mmoja, kabla yakuongezewa wadhifa wa unaibu waziri katika Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, kwenye wizara ya Nishati na Madini kutokea Januari 2007 hadi Agosti 2008.

Mwaka 2008 kulipofanyika mabadiliko katika Baraza la Mawaziri, baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Ngoyayi Lowassa kujiuzulu kutokana na kashfa ya Richmond, Rais Kikwete aliunda Baraza la Mawaziri jipya na kukuza “ngekewa” ya Ngeleja ambaye alipewa uwaziri kamili wa Nishati na Madini kukamilisha miaka miwili iliyokuwa imebakia kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwkaa 2010. Mwaka 2010 Ngeleja alijitosa tena kwenye kinyang’anyiro cha ubunge kutetea nafasi yake; alishinda kura za maoni na kwenye uchaguzi wenyewe akawa hana mpinzani, yaani wagombea wa upinzani waliingia “mitini” na kumpa “zawadi ya ushindi”.

Baada ya kupita bila kupingwa aliteuliwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini, nafasi
aliyoitumikia hadi Juni 2012 mwaka ambao Rais Kikwete alifanya mabadiliko madogo kwenye Baraza la Mawaziri na Ngeleja hakubahatika kuwepo.

Nafasi yake ilichukuliwa na Profesa Sospeter Muhongo. Pamoja na kuwa nje ya uwaziri, safari yake kisiasa iliendelea kukumbwa na mawimbi mengi. Mwanzoni mwa mwaka jana,
alilazimika kuachia ngazi katika nafasi ya uenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala kutokana na kuwa miongoni mwa viongozi waliopokea mgawo wa fedha zilizochukuliwa kutoka kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.

Alipoitwa kujieleza kwenye Tume ya Maadili, Ngeleja alikiri kuwekewa shilingi 40.4milioni na mmiliki wa Kampuni ya VIP Engineering & Marketing, James Rugemalira lakini mwenyewe alisisitiza kuwa fedha hizo hazikuwekwa kwa nia mbaya. Na kibaya Zaidi yeye mwenyewe hakutoa taarifa kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.


MBIO ZA URAIS

Ngeleja ni mmoja wa watu waliotajwa sana kama watu wanaomuunga mkono Lowassa katika safari ya kuisaka Ikulu tangu alipokuwa Waziri Mkuu chini ya Rais Kikwete na hata
baada ya kujiuzulu nafasi hiyo mwaka 2008.
Na hata Ngeleja alipoteuliwa tena kuwa Waziri wa Nishati na Madini, mara baada ya kuteuliwa kwa mara ya pili Januari 2011, ilisemekana kuwa anamuunga mkono waziri mkuu huyo aliyejiuzulu. Lakini katikati ya mwaka 2013, inasemekana wanamtandao wa urais katika kundi la Lowassa wanaotokea Kanda ya Ziwa, waliona vema kumuibua mgombea anayeweza kuungwa mkono kutoka kanda yao na ndipo akainuliwa Ngeleja.

Katika harakati za chini kwa chini akawa miongoni mwa makada sita walionaswa na chama wakifanya kampeni za siri na wakazuiwa kwa miezi 12 kuanzia Februari mwaka juzi. Kamati ya Maadili inaendelea kuwachunguza.

Hata harakati zake za kuwapigania wachimbaji wadogowadogo wapate maeneo zaidi kwa ajili ya uchimbaji, kuwaanzishia mfuko maalum wa kuwasaidia, kupiga marufuku usafirishaji wa madini ghafi kwenda nje ya nchi, na hatua kama hizo, zilikuwa zinahusishwa na mbio hizo hasa kwa kuzingatia kuwa maeneo yenye madini yana wapigakura wengi sana. Hata hivyo, jambo hilo halijathibitishwa.


Watu walio karibu naye, miongoni mwao wakiwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, wanasema kwamba yeye huwa anajinasibu kuwa anaweza kuwa chaguo mbadala makada maarufu watakapokatwa majina yao kipindi cha mchakato we urais CCM.


NGUVU ZAKE
Ngeleja amewahi kuwa karibu sana na Lowassa, Kwa hiyo, anaujua vizuri mtandao wa ushindi ndani ya CCM hasa kwa sababu alishiriki pia shughuli kama hiyo wakati wa kumpigania Kikwete mwaka 2005.

Jambo hili linampa nguvu kubwa. Nguvu nyingine ya Ngeleja inatokana na umri wake, kwani anaonekana bado kijana sana. Ikiwa CCM itahitaji mgombea
mwenye umri wa “usasa” na ambaye ana kaliba inayoweza kuwavutia vijana na watu wengine, Ngeleja atakuwa miongoni mwa watu wenye sifa hiyo.


Tukija katika uzoefu, eneo hili pia linampa Ngeleja nguvu kubwa. Tangu mwaka 1994 Ngeleja ameweza kutumika serikalini na katika mashirika binafsi na ya kimataifa kama mwanasheria. Uzoefu huo una maana kuwa anaifahamu vizuri nchi na mazingira ya kazi katika sekta ya umma na sekta binafsi. Hakika kigezo hiki kinampa nguvu ya kipekee tofauti
na wagombea wengine ambao labda wamewahi kufanya kazi serikalini tu. Nguvu nyingine ya Ngeleja inapatikana kwenye taaluma yake. Sheria ni taaluma ya “kipekee” na ina tofauti kubwa sana na masomo ya sanaa. Mara nyingi viongozi wanasheria wanatarajiwa kujiamini na kutenda masuala ambayo yanaweza kutohojiwa kirahisi. Ikiwa itachukuliwa kwa mtazamo huo na kwamba CCM inahitaji msomi mzuri mwenye taaluma ya kipekee na inayoweza kumfanya mtu afanye kazi katika mazingira yoyote kwenye sekta nyingine, basi Ngeleja atakuwa miongoni mwa wanaofuzu.

HITIMISHO
Naona kama Ngeleja atakuwa na wakati mzuri sana kisiasa huko mbeleni, cha msingi aendele kuwa mkimya na mchapa kazi.
 
Ngeleja, kaisha sana kisiasa.

Hivi sasa atakuwa ananyoosha mkono kuomba nafasi ya kuuliza maswali ya nyongeza kama wengine
 
Ngeleja, kaisha sana kisiasa.

Hivi sasa atakuwa ananyoosha mkono kuomba nafasi ya kuuliza maswali ya nyongeza kama wengine

Kumbuka NGELEJA ni MBUNGE wa Jimbo la Sengerema, anaelekea kutumiza miaka 15 Jimboni. Sasa unasema kaisha kisiasa, hebu tufafanulie. Kaisha kivipi?
 
Kumbuka NGELEJA ni MBUNGE wa Jimbo la Sengerema, anaelekea kutumiza miaka 15 Jimboni. Sasa unasema kaisha kisiasa, hebu tufafanulie. Kaisha kivipi?
Ngeleja huyu huyu anayezomewa majukwaani jimboni kwake kila siku.

Huyu huyu aliyekuwa waziri kwenye sekta tamu lakini akaishia kupigwa chini.

Huyu huyu aliyekuwa kambi ya Lowassa ambaye ni hasimu wa Magufuli??

Huyu dogo siasa zimemkataaa
 
Sio mtu wa maadili kabisa pamoja na cv yake nzuri amejiharibia sana kwani ni mtu wa 'ma deal' asie na uzalendo wa Nchi yake!
 
Ngeleja huyu huyu anayezomewa majukwaani jimboni kwake kila siku.

Huyu huyu aliyekuwa waziri kwenye sekta tamu lakini akaishia kupigwa chini.

Huyu huyu aliyekuwa kambi ya Lowassa ambaye ni hasimu wa Magufuli??

Huyu dogo siasa zimemkataaa

Hata Yesu, alizomewa na wayahudi lakini Mwisho wa siku aliwakomboa.
Kazi aliyofanya akiwa Waziri inajulikana na wataalamu wanasema Ngeleja ni Baba wa Nishati na Nadini.
Mbona wewe ulikuwa kambi ya Membe? Kwani Membe ni rafiki yake Magufuli.
Nakushauri uendele kula mahindi, kubeba maboksi ili upate ujira dogo.
 
Sio mtu wa maadili kabisa pamoja na cv yake nzuri amejiharibia sana kwani ni mtu wa 'ma deal' asie na uzalendo wa Nchi yake!
Niamini Mimi, kama kuna mzalendo kijana aliebakia TZ Mzalendo huyo ni WILLIAM MGANGA NGELEJA.
 
Back
Top Bottom