Mfahamu mdudu kunguni (bedbugs) na jinsi ya kumuangamiza

Hizo sehemu zote ndo uchafu wenyewe maana kwenye kona za kuta maana yake usafi wa mara kwa mara haufanyiki na kwa upande mwingine pia mazingira ambayo kunguni anakaa ni kwenye nyumba yenye vitu vingi kwenye chumba kimoja hasa ukizingatia Watz wengi wanaishi stoo, chumba kina kitanda na viroba vya mahindi uvunguni na kwenye pembe za kuta kuna makwanja na majembe.

Kimsingi wakati watu wanapambana na kunguni, wakumbuke kuondoa mazingira rafiki ya kunguni kuishi kwenye nyumba zao kwa kupunguza makorokoro na kukumbuka kupiga kuta rangi na kuruhusu mwanga wa kutosha kuingia ndani vinginevyo utawaua kunguni ipo siku tena watarudi (kila mtu anajitetea kuna wageni walikuja wakawaleta)
 
Sio kila mtu anajitetea, ni kweli mimi sikuwah kuwaona kunguni hadi nilivyotoka home kwenda kupanga mtaani, na nilikuwa bachela msafi sana tuu ila walikuja baada ya washkaji weengi kuingia na kutoka, nilivyopiga dawa nikamwingiza mama mtu geto washkaji hawakuja tena na wadudu sikuwaona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu sio kama najisifia mimi msafi saana, lakini ni msafi kwa hakika natamani hata nikupigie picha tu uangalie angalau mazingira utaona hakuna hata moja ya uliotaja hapo, madirisha makubwa ya kutosha chumbani nina kitanda na kabati dogo tu la nguo
Sebuleni kuna set ya kochi na meza ya kioo friji na tv ukutani, sebule kubwa haswa

Kuhusisha kunguni na uchafu labda iwe kwa maana wachafu hawajali uwepo wa kunguni na wanishi nao hivyo hivyo na kusababisha waendelee kuwepo na kusamba

Nakihakikishia wewe msafi ukija kubeba kunguni ukaingia nao ndani kwako utajua ninalojaribu kukueleza hapa
Kunguni sio sawa na nzi au mende wanaokula uchafu, hawa wahuni wanakula damu yako tuu hata uwe msafi vipi as long as wamepata access ya kuingia kwako utajuta
Hata uwe mchafu kiasi gani kama hawajaingia kwako utakua salama

Ubaya mwingine kasi yao kuzaliana ni balaa yani ukiona mayai kwenye kitanda godoro makochi ni sehemu ambazo usafi wa kawaida hauwagusi kabisaa
Baada ya maoni ya wadau ilibidi ni google..... aisee hawa jamaa ni janga la dunia
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na wakiwa hajajiandaa kutoka nduki ukiwamulika taa wanazuga km wamekosea njia wanavyohangaika kutafuta chochoro


Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa wadudu wana akili kweli.
I think sumu ya wadudu iitwayo fiprofam (haina harufu ila ni sumu) ikipigwa sehemu husika (kingo za kuta, kitanda, shelves watateketea tu). Care should be taken kuepusha madhara kwa binadamu.
 
Mkuu sijasema mie msafi na hakuna Mtanzania ambae haja experience kunguni ila ukweli unabaki palepale kunguni anasababishwa na uchafu na mazingira flani flani ya hali nyumba kuwa na giza hivyo wakiingia ndani na mwenye nyumba akawachukulia poa hapo ndio chanzo cha tatizo na ndio maana mpaka dakika hii uzi umefika page kadhaa maana inaonyesha tatizo bado lipo na mazingira ya uchafu bado yapo na ndio humo wanapozaliana ambapo wakienda kutembelea ndugu zao wanahama na kuwahamisha (kama nyumba ipo kama yako ulivyoielezea maana yake hapo wamepita na zoezi la kuwaondoa nadhani limekuwa simple tofauti na nyumba ambayo nimeielezea mie. (mie Mtanzania mzawa nyumba zetu nazijua tuliowengi unakuta kochi set 3 ndio maana akiingia mdudu unashituka wameenea)

Nawafahamu vizuri kunguni mkuu na magodoro yetu ya zamani yalikuwa hayana foronya na wenyewe wanajificha kwenye vile vitobo vya godoro, nilichokisema mie ni solution tu yaani zoezi la kuwaondoa liende sambamba na kuweka mazingira ya nyumba kuwa na mwanga wa kutosha na nyumba isiwe na makorokoro mengi, na hiyo ni kwa wadudu wadogo wadogo wote wakiwemo mende hata mbu.
 
 
Kunguni ni mdudu ambae hafi kirahisi sana hivyo basi usitegemee kuweka dawa siku moja tu haitotosha kuwamaliza,chakufanya kila wiki weka dawa kwa muda wa wiki tatu au nne mfululizo bila shaka watapotea kabisa.
 
Hawa wadudu wana akili kweli.
I think sumu ya wadudu iitwayo fiprofam (haina harufu ila ni sumu) ikipigwa sehemu husika (kingo za kuta, kitanda, shelves watateketea tu). Care should be taken kuepusha madhara kwa binadamu.
Kosa moja kubwa sana ambalo wengi wetu tunalifanya ni kutumia nguvu nyingi sana kumuangamiza kunguni mwenyewe, mimi naamini bado tunakuwa hatujaondoa tatizo.
Kwa kuwa kunguni kama kunguni ni rahisi sana kumuua, mfano chukua sabuni ya unga changanya na maji ukimwagia kunguni anakufa au maji ya moto au juani anakufa mara moja.
Lakini mpaka hapo bado tutakuwa hatujaondoa tatizo kwa kuwa wengi wetu tunasahau mayai yake! hili ndio janga halisi.
Huwezi kuangamiza mayai yake juani au kwa maji ya moto ni lazima yatabaki, kwa hiyo utakapo anika juani au kutia maji moto ni sawa na kuyaweka kwenye INCUBATOR na baada ya siku tatu au nne vitaibuka vitoto kibaaao na hivi vikija utakoma, maana vinakuwa ni vikali sana.

USHAURI:
Usianike au kutumia maji moto kuwamwagia kwa maana utawauwa kunguni na wakati huohuo unazalisha wengine, cha kufanya tafuta sumu ya kuwauwa na uipulizie humohumo mdani bila kuhamisha chochote, kwa maana kitendo cha kuhamisha hamisha vifaa ni kuawasambaza, piga dawa chumbani pqmoja na godoro na kitanda usisahau madirishani na milangoni na kutani na kwenye matundu na nyufa zote.
Hili tendo lirudiwe zaidi ya mara mbili ili kuhakikisha mayai yote na kunguni wameangamia.
Nimepata ufahamu huo baada ya kunisumbua sana, nilianika juani haikufaa, nlitia maji moto haikufaa, nilitia mafuta taa hola niliwachoma na hair dryer haikufaa nilitumia mchanganyiko wa sabuni na jik kunguni wenyewe wanakufa fasta lakini mayai ni tatizooo mpaka upate sumu ya uhakika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huko Kenya matatu (sawa na daladala hapa kwetu ).ilivamiwa na kunguni mapaka abiria wakaogopa kuitumia . Kuna siri gani ya hawa kunguni ? Naomba Mshana atueleze katika ulimwengu wa roho .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo BITO ni Aka Tu
 
Mkuu mi sijawah kuwa hata na nzi wala mbu geto kwangu wala mende, na nilikua bishoo ila najua kuna mpuuzi mmoja tu alikuja nao tuu maana siwez kujua ntawazalishaje mwenyewe na niliishi home fresh tuu tangu nazaliwa ndo nije kuwa nao ukubwani, theory ya uchafu ni uongo, maana nakumbuka utotoni sikuwa msafi, na boarding nimesoma sijawaona, na chuo hosteli sijawaona ndo nimekuja kuwaona baada ya kupanga uswazi na kukaribisha washkaji tu wanachill wanacheki muvi nini wanaenjoy mara haaaooo,

Sent from my TECNO W1 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…