Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 375,728
- 870,464
Kuna kitu huwa nakiepuka sana! Kuvaa nguo zenye maandishi na michoro nisiyojua maana wala tafsiri yake.. Kwakuwa huwezi jua umevaa kitu kilichoandikwa nini na tafsiri yake ninini
Lakini zamani kama miaka 15 hivi iliyopita niliwahi kununua Tshirt yenye kikaragosi kinachopuliza zumari kikiwa kimetanguliza mbele vikaragosi vingine vidogo kama vitoto na chini yake kukiwa na maandishi ya kokopeli/cocopeli
Kwa mahaba makubwa na kile kikaragosi na maandishi yake T-shirt ile ilipochakaa niliichukua mpaka kwa mchoraji anichoree ile picha ibaki kama kumbukumbu! Sikuwahi kumuona tena!
Leo nimepita mitandaoni na kukutana na kokopeli na hii ndio tafsiri yake!
Kokopeli ni pepo anayeonyeshwa kama mpiga filimbi mwenye nundu (mara nyingi akiwa na manyoya kichwani), ambaye ameheshimiwa na baadhi ya tamaduni za Wenyeji wa Amerika Kusini-Magharibi mwa Marekani.
Kama miungu mingi ya uzazi, Kokopelli anasimamia uzazi na kilimo. Yeye pia ni mungu wa hila(figisu) na anawakilisha roho ya muziki.
Utamaduni wa Hopi unaamini kwamba yeye hubeba watoto ambao hawajazaliwa mgongoni mwake na kuwasambaza kwa wanawake.
•Mpagani wa Ulimwengu wa Kusini
KOKOPELLI
Sent using Jamii Forums mobile app