Mfahamu Dr. Makongoro Mahanga kiundani

Mfahamu Dr. Makongoro Mahanga kiundani

MeinKempf

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2013
Posts
11,092
Reaction score
7,236
WATU wengi wanamfahamu Dk. Milton Makongoro Mahanga kama mwanasiasa ambaye amekuwa mbunge wa Jimbo la Ukonga kupitia CCM na baadaye Segerea kwa jumla ya miaka 14 sasa kuanzia mwaka 2000, na Naibu Waziri wa Miundombinu na baadaye Kazi na Ajira kwa jumla ya miaka 9 kuanzia mwaka 2006.

Wiki hii Raia Mwema lilifanya naye mahojiano kwa ajili ya kufahamu maisha yake binafsi na ya kitaaluma kabla hajawa mwanasiasa.

Swali:1. Ingawa wewe ni mwanasiasa kwa takribani miaka 15 sasa, watu wengi hawajui kwamba wewe ni mwanataaluma wa fani kadhaa zikiwemo Kodi, Fedha na Ununuzi na Ugavi. Kabla ya kutueleza mchango wako kwa taifa hili kwenye fani hizo, labda kwanza utueleze historia yako kwa ufupi.

Jibu 1:
Mimi nilizaliwa katika kijiji cha Mugeta wilaya ya Mara Kusini (sasa Bunda) tarehe 3 Aprili 1955. Akina mama wawili wa kabila la Waikizu waliomsaidia mama yangu kujifungua, waliwaomba wazazi wangu wakubali kunipa jina la Makongoro ambaye alikuwa Chifu wa Waikizu ingawa asili yetu sisi ilikuwa ni wilaya ya Mara Kaskazini (sasa Rorya).

Wazazi wangu walikubali na mpaka sasa natumia jina hilo la Makongoro. Baadaye tulihamia wilaya ya sasa ya Serengeti ambako nilisoma katika Shule za Msingi za Kyambai (sasa Matare) na Mugumu katika wilaya hiyo ya Serengeti na Bukama Ikizu katika wilaya ya Bunda kati ya mwaka 1965 na 1971. Mwaka 1972 hadi 1975 nilisoma kidato cha Kwanza hadi cha Nnne katika Shule ya Sekondari Mara na baadaye kumaliza masomo ya Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari Tambaza jijini Dar es Salaam.

Swali 2: Vipi kuhusu masomo yako ya juu?

Jibu 2: Kuanzia mwaka 1978 hadi 1980 nilichukua masomo ya Shahada ya Kodi na Uhasibu katika Chuo cha Fedha (IFM) jijini Dar es Salaam. Kupitia Bodi ya Ununuzi na Ugavi ya NBMM (sasa PSPTB) nilikuwa Mtanzania wa kwanza kupata Stashahada ya Juu ya Ununuzi na Ugavi CSP (sasa CPSP) inayotolewa na NBMM mwezi Mei 1980. Aidha kwa mara nyingine nilikuwa Mtanzania wa Kwanza kuwa na CSP na CPA kwa pamoja pale nilipofanikiwa kupata Stashahada ya CPA inayotolewa na Bodi ya Uhasibu (NBAA) mwezi Mei 1983. Baadaye, nikiwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) niliamua kusoma na kutunukiwa cheti cha uzamili kwenye masuala ya fedha (MSc Finance) mwaka 1997 kupitia Chuo Kikuu cha Strathclyde cha Glasgow nchini Uingereza.

Aidha kupitia utafiti wa kina nilioufanya nchini Tanzania na nchi nyingine kama Uingereza, Kenya na Uganda kuhusu mahusiano kati ya umasikini na makazi duni mijini, nilifanikiwa kutunukiwa Shahada ya uzamivu (PhD) kupitia Chuo cha Washington International University cha nchini Marekani Julai mwaka 2000. Kwa umahiri wake, utafiti wangu huo uliweza kuchapishwa mwaka 2002 na wachapishaji wa Dar es Salaam University Press (DUP) kama kitabu: "Urban Housing and Poverty Alleviation in Tanzania" kwa namba ISBN 9976-60-343-6.

Swali 3:
Sasa tueleze kidogo uzoefu wako wa kazi, hasa mchango wako kwa Serikali na taasisi zake kwenye taaluma zako za kodi, fedha na ugavi.

Jibu 3: Labda nianze kwa kusema kwamba mpaka sasa nimefanya kazi kwa miaka ipatayo 37. Miaka 23 nilifanya kazi serikalini na taasisi zake na miaka 14 kama mbunge. Nilianza kazi katika Idara ya Kodi ya Mauzo (Sales Tax Department) Wizara ya Fedha katika Ofisi ya Kodi Mkoa wa Dar es Salaam mwaka 1977 hadi 1980.

Nakumbuka nilipokuwa idara hiyo (wakati huo VAT haijaanza) nilitoa mchango mkubwa kwa Serikali kama mhakiki wa kodi zilizokuwa zinatozwa kwenye makampuni na mashirika mbalimbali. Kutokana na umahiri wangu wa kufuatilia na kukagua nyaraka za walipa kodi ya mauzo, mkuu wa kitengo changu, Bwana Mwanjali chini ya Ofisa Mkuu wa Kodi wa Mkoa wa Dar es Salaam (RFO), Mzee Rugakingira waliamua kunikabidhi mashirika na makampuni yote makubwa ya mkoa wa Dar es Salaam ili nikague ulipaji wao wa kodi kwa miaka mitano ya nyuma.

Kwa umahiri wangu niliweza kugundua kodi iliyokuwa ipotee ya mamilioni ya fedha kutoka makampuni na mashirika haya makubwa na wakatakiwa kulipa malimbikizo hayo. Aidha kuanzia hapo walianza kulipa kodi stahiki iliyokuwa mara mbili ya kodi waliyokuwa wakilipa kabla sijawakagua kutokana na udanganyifu.

Nakumbuka makampuni na mashirika makubwa niliyokabidhiwa kukagua na kugundua udanganyifu mkubwa ni pamoja na Shirika la Bia Tanzania (sasa TBL), Shirika la Usagishaji (NMC), Konyagi, Blanket Manufacturers na Matharu Woodworks. Siku moja kwenye mwezi wa Aprili au Mei 1977 nilifurahi sana nilipoitwa Wizarani Hazina ofisini kwa Kamishina wa Kodi ya Mauzo, Bw. Mang'enya aliyeagiza kwamba anataka kumwona na kumpongeza "huyo kijana" aliyeweza kuokolea serikali mamilioni ya fedha zilizokuwa zipotee kwa udanganyifu kwenye ulipaji wa kodi ya mauzo.

Swali 4: Sasa, kwa umahiri huo kwenye ukusanyaji wa kodi, ukizingatia ulitueleza kwamba ulikwenda kusoma Diploma ya Kodi Chuo cha IFM, ilikuwaje tena ukaacha sekta ya kodi na kwenda kwenye masuala ya ugavi na uhasibu? Na huko ulitoa mchango gani?

Jibu 4: Mwaka 1978 nilipokuwa nasoma hiyo diploma ya kodi katika chuo cha IFM, na kwa kupitia taarifa mbalimbali za Serikali na mashirika, niligundua kwamba eneo ambalo fedha nyingi sana zinapotea katika nchi hii, kuliko hata kwenye kodi za Serikali, ni eneo la ununuzi na ugavi.

Wakati huo, baadhi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi waliosomea fani hiyo nje ya nchi, wakiongozwa na Marehemu Donald Tumbo, wakishirikiana na Wizara ya Fedha, waliamua kuanzisha chombo cha kusimamia masomo na fani ya ununuzi na ugavi hapa nchini. Chombo hicho (Materials Management Caretaker Committee) kilipoanza tu kuendesha kozi za fani hiyo mwaka 1977 nilikuwa mmoja wa wanafunzi wake wa kwanza, na ilipofika mwezi Mei 1980 nilikuwa mtanzania wa kwanza kumaliza masomo ya fani hiyo hapa nchini kupitia chombo hicho ambacho mwaka 1981 kilikuja kubadilishwa na Bunge kwa kuanzisha Bodi na Sheria ya Ununuzi na Ugavi (NBMM). Kwa kupata hiyo Certified Supplies Professional (CSP) ya kwanza kabisa nchini niliweka historia. Kwa kuona umuhimu wa kueneza haraka fani hii muhimu sana nchini, niliamua niingie kwenye fani hii na nianze kwa kuwafundisha wanafunzi na maafisa wanaofanya kazi kwenye taaluma hii. Hivyo mwishoni mwa mwaka 1980 nilitoka serikalini na kujiunga kama Mhadhiri kwenye Chuo cha Nyegezi Social Training Institute (sasa SAUT) mara tu baada ya chuo hicho kuanzisha kozi ya stashahada ya ununuzi na ugavi (ADMM), na nikawa mmoja kati ya walimu wawili walioanza kufundisha kozi hiyo hapo chuoni.

Nilifundisha chuoni hapo miaka karibu minne hadi 1984. Na hata baada ya kutoka chuoni hapo niliendelea kufundisha masomo ya fani hiyo nyakati za jioni (part-time)kwa miaka mingine 10.

Unaweza kufuatilia mchango wangu kwa Taifa hili kwenye fani hii kwa kuona kwamba kuna wakati asilimia karibu 70 ya idara za ununuzi na ugavi kwenye wizara zote za Serikali na mashirika na makampuni makubwa nchini ziliongozwa na waliokuwa wanafunzi wangu (kwa sasa wengine wamestaafu). Aidha wakati nikifundisha masomo haya ya ununuzi na ugavi (kwa miaka 14) niliweza kutunga na kuandika vijitabu zaidi ya vinne kwenye fani hii, na hivi viliwasaidia sana wanafunzi wa fani hii nchini kusoma na kushinda mitihani yao. Lakini pia nilichangia sana kuendeleza Bodi ya taaluma ya ununuzi na ugavi nchini (NBMM) kama mtaalamu, mjumbe na Mwenyekiti wa Bodi hiyo kwa jumla ya miaka 25. Lakini pia nimeshiriki katika uanzishwaji na uendelezaji wa Sheria ya Ununuzi wa Umma (PPA) hapa nchini kama mtaalamu wa fani hii.

Swali 5: Na taaluma ya Uhasibu na Fedha uliingiaje huko?

Jibu 5: Nilipoamua kuacha fani ya kodi, niligundua kwamba fani za uhasibu na fani ya ununuzi na ugavi zilikuwa zinafanana, na hivyo nikaamua kuzisoma zote mbili kwa pamoja.

Wakati nikimaliza CSP mwaka 1980 tayari nilishamaliza cheti na diploma ya uhasibu (NABOCE na NAD) na ilipofika Mei 1983 nilitunukiwa stashahada ya CPA na Bodi ya NBAA na hivyo nikaweka tena historia nchini kwa kuwa mtanzania wa kwanza kuwa na CSP na CPA kwa pamoja. Kwa kuwa nilikuwa tayari ni mtaalamu aliyeidhinishwa kwenye fani ya Ugavi na Uhasibu (Certified Supplies Professioinal na Certified Public Accountant), baada ya kuacha kufundisha Nyegezi, mashirika yote niliyofanya kazi niliongoza idara zilizokuwa zinasimamia masuala ya fedha na pia masuala ya ununuzi na ugavi.

Kwa miaka sita (1985-1991) nilikuwa Mhasibu Mkuu wa Bima Motors nikisimamia pia Idara ya Ununuzi na Ugavi. Mwaka 1991 hadi 1994 nilikuwa Msarifu (Bursar) wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nikiongoza Idara za Fedha na pia idara ya Ununuzi na Ugavi, na kwa miaka sita (1994 hadi 2000) nilikuwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) nikisimamia pia Idara ya Ununuzi na Ugavi.

Katika taasisi hizi tatu za mwisho niliweza kutoa mchango mkubwa wa kurekebisha na kusimamia masuala ya fedha kwa faida ya taasisi hizo na serikali kwa ujumla. Nikiwa Mhasibu Mkuu na mwanzilishi wa kanuni na taratibu za matengenezo katika kampuni tanzu ya Bima Motors niliweza kulipunguzia Shirika la Bima la Taifa (NIC) gharama kubwa za kutengeneza magari ya wateja yaliyowekewa bima na kupata ajali.

Badala ya kuyapeleka kwenye karakana za watu binafsi, magari haya yalitengenezwa kwenye karakana hiyo ya umma ya Bima Motors kwa gharama nafuu. Nilipoingia Chuo Kikuu cha UDSM mwaka 1991 nilikuta mahesabu ya Chuo hicho yakiwa hayajakaguliwa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa miaka karibu 10.

Kwa muda wa miaka minne tu nikiongoza Idara ya Fedha na Ugavi kama Msarifu, mahesabu yote hayo yalikaguliwa na hatimaye mahesabu ya mwisho kupata hati safi, na mwaka 1994 nilipokuwa naondoka mahesabu ya 1993 yalikuwa yanakaguliwa.

Hivyo nilipoingia NHC mwaka 1994, nilikuta mahesabu ya shirika yako nyuma toka Shirika la Msajili wa Majumba na Shirika la Nyumba yaungane mwaka 1990. Kwa usimamizi wangu, mahesabu yote ya nyuma yalikaguliwa na wakati natoka NHC kugombea ubunge mwaka 2000, CAG alikuwa amekamilisha ukaguzi wa hesabu za NHC za mwaka 1999 na zilipata hati safi.

Aidha nikiwa UDSM na NHC niliwataka wahasibu na maafisa ugavi wote wasome wapate vyeti vya kitaaluma na wasiotaka au kushindwa niliomba uongozi uwaondoe kwenye idara yangu.

Ndiyo maana wahasibu wenye CPA na maafisa ugavi wenye CSP/CPSP kwa sasa wako wengi UDSM na NHC tofauti na kabla sijaingia kwenye taasisi hizo.

Kama ulivyosema mwanzoni, wengi wanajua kazi zangu kama mbunge wa Ukonga na Segerea kuanzia mwaka 2000 hadi 2014. Majimbo haya mwaka 2000 yalikuwa na kero kubwa sana za miundombinu, barabara, maji, elimu, afya na umeme, lakini sasa hali inaridhisha sana. Lakini haya tunaweza kujadili siku nyingine.

J e, una kipi cha kujifunza juu ya hayo uliyoyasoma?

SOURCE:
Raia Mwema
 
Attachments

  • dr makongoro.jpg
    dr makongoro.jpg
    9.6 KB · Views: 496
  • MAHANGA 1..jpg
    MAHANGA 1..jpg
    7.9 KB · Views: 465
huyu jamaa alishawahi kuchukua nyota ya ndugu yangu, tulipoenda kwneye kioo tulimwona laivu na tukamtandika balaa. hukumu yake ipo inakuja tena haraka sana. kule misri tulishaondoka tupo kaanani na hukumu yake atamhukumu Mungu mwenyewe. kuna viongozi wengi tu wakiwa mawaziri nk wanafanya kazi kwa kuiba nyota za watu, wanatumia waganga wa kienyeji kuiba nyota za watu. wakifanya kazi utafikiri wao kumbe wamewaacha masikini makopo huko mtaani. Mungu ni wa haki na atatoa haki siku ikifika. Mungu mwenyewe atakuhukumu.
 
Mkuu sijakusoma vile... au mazombi yamekukurupusha kutoka usingizini? sioni uhusiano wa ulichokijibu na maelezo ya maswali hayo 5.
Au ndo kusema umegeuka kuwa Dr.Manyau Nyau au prof. Maji marefu?
 
Huyu Dr namfahamu kama mwizi wa kura jimboni Segerea mwaka 2010 zaidi ya hapo mengine nimeyajua baada ya kusoma huu Uzi.......
 
huyu jamaa alishawahi kuchukua nyota ya ndugu yangu, tulipoenda kwneye kioo tulimwona laivu na tukamtandika balaa. hukumu yake ipo inakuja tena haraka sana. kule misri tulishaondoka tupo kaanani na hukumu yake atamhukumu Mungu mwenyewe. kuna viongozi wengi tu wakiwa mawaziri nk wanafanya kazi kwa kuiba nyota za watu, wanatumia waganga wa kienyeji kuiba nyota za watu. wakifanya kazi utafikiri wao kumbe wamewaacha masikini makopo huko mtaani. Mungu ni wa haki na atatoa haki siku ikifika. Mungu mwenyewe atakuhukumu.

Du! Mulienda kwenye kioo mkakuta nyota imeibwa? Sasa kwa nn hamkuirudisha kimyakimya hyo nyota? Pia unaenda kwa mganga halafu unamtaja Mungu aliye hai? A u siriaz? Unafikiri Mungu anapenda washirikina? Acha kumchafua mzee wa watu.
 
huyu jamaa alishawahi kuchukua nyota ya ndugu yangu, tulipoenda kwneye kioo tulimwona laivu na tukamtandika balaa. hukumu yake ipo inakuja tena haraka sana. kule misri tulishaondoka tupo kaanani na hukumu yake atamhukumu Mungu mwenyewe. kuna viongozi wengi tu wakiwa mawaziri nk wanafanya kazi kwa kuiba nyota za watu, wanatumia waganga wa kienyeji kuiba nyota za watu. wakifanya kazi utafikiri wao kumbe wamewaacha masikini makopo huko mtaani. Mungu ni wa haki na atatoa haki siku ikifika. Mungu mwenyewe atakuhukumu.

Mkuu funguka,me najua jamaa ni fisadi wa migodi na Ardhi,ana migodi kuanzia Morogoro hadi njombe huko plus michepuko ile yenye Bantu figure,mmoja wapo kamkodishia mbezi kule karibu na kwa Mbona!!!
 
he! :A S-eek: .........
 
Big ego ... Kwa umahiri wangi etc... Even though this was a paid interview one does no to talk the way he does.
 
Huyu Dr namfahamu kama mwizi wa kura jimboni Segerea mwaka 2010 zaidi ya hapo mengine nimeyajua baada ya kusoma huu Uzi.......

Licha ya unayo yasema ...ila nadhani mnyonge mnyongeni ila haki ya mpeni.... jamaa ni kichwa .
 
Mkuu funguka,me najua jamaa ni fisadi wa migodi na Ardhi,ana migodi kuanzia Morogoro hadi njombe huko plus michepuko ile yenye Bantu figure,mmoja wapo kamkodishia mbezi kule karibu na kwa Mbona!!!

Kwa hiyo unataka kusema kuwa ASIFUYE MVUA UJUE.... ahahaaa... jiwe la kutupa gizani utajua majibu yake kwa yowe utalosikia baada ya sekunde kadhaaa.
 
Kwa hiyo unataka kusema kuwa ASIFUYE MVUA UJUE.... ahahaaa... jiwe la kutupa gizani utajua majibu yake kwa yowe utalosikia baada ya sekunde kadhaaa.

Wacha hoja muflisi,kimada wake alikuwa haiishi ofisini kwangu,mara ya mwisho aliomba nimpatie dola 700 kwa nusu tani ya kopa toka Ludewa,nikampa 500$,usitake tuandike na ya ndani kwa kutetea upuuzi!!!
 
Washington International University ni MKANJANJA tu....ni MAKANJANJA ya mfukoni tu na wala hakiko accredited. Naona ameamua kuweka black & White kuhusu PhD yake.
 
Hii ni interview au tangazo? Sidhani kama mwandishi wa raia mwema alifanya hii kazi, zaidi itakuwa Mahanga alijiandikia na kununua space kwenye gazeti.Mhariri anajua ukweli wa hili
 
(1) Niliamua kusoma na kutunukiwa cheti cha uzamili kwenye masuala ya fedha (MSc Finance) mwaka 1997 kupitia Chuo Kikuu cha Strathclyde cha Glasgow nchini Uingereza.
Chuo hiki (mpaka sasa)kinatoa shahada iliotajwa kupitia Chuo cha Usimamizi wa fedha (IFM). Hii ni kweli, ila isieleweke kuwa ALIKWENDA Glasgow kusoma.....

(2)...
Kwa umahiri wake, utafiti wangu huo uliweza kuchapishwa mwaka 2002 na wachapishaji wa Dar es Salaam University Press (DUP) kama kitabu: "Urban Housing and Poverty Alleviation in Tanzania" kwa namba ISBN 9976-60-343-6.

Hapa ieleweke kuwa DUP ni wachapishaji wafanya biashara. Alipeleka muswada, akalipia na kupata hiyo ISBN, na asitudanganye kuwa ni kutokana na umahiri wake. Kama ingekuwa hivyo, chuo alikotunukiwa Shahada (kama kipo) ndicho kingechapisha huo utafiti kama kitabu.
 
(1) Niliamua kusoma na kutunukiwa cheti cha uzamili kwenye masuala ya fedha (MSc Finance) mwaka 1997 kupitia Chuo Kikuu cha Strathclyde cha Glasgow nchini Uingereza.
Chuo hiki (mpaka sasa)kinatoa shahada iliotajwa kupitia Chuo cha Usimamizi wa fedha (IFM). Hii ni kweli, ila isieleweke kuwa ALIKWENDA Glasgow kusoma.....

(2)...
Kwa umahiri wake, utafiti wangu huo uliweza kuchapishwa mwaka 2002 na wachapishaji wa Dar es Salaam University Press (DUP) kama kitabu: “Urban Housing and Poverty Alleviation in Tanzania” kwa namba ISBN 9976-60-343-6.

Hapa ieleweke kuwa DUP ni wachapishaji wafanya biashara. Alipeleka muswada, akalipia na kupata hiyo ISBN, na asitudanganye kuwa ni kutokana na umahiri wake. Kama ingekuwa hivyo, chuo alikotunukiwa Shahada (kama kipo) ndicho kingechapisha huo utafiti kama kitabu.

all u Say are true
 
Back
Top Bottom