Mfahamu Binti Mfalme wa Dola ya Mongolia Aliyefahamika kwa Jina la Khutulun

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
FB_IMG_1636920183637.jpg

BINTI MFALME WA DOLA YA MONGOLIA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA KHUTULUN.

Khutulun alikuwa binti wa pekee wa Kaidu Khan ambaye alikuwa ni kizazi cha mfalme wa dola ya mangolia Ganghis Khani shujaa aliyeogopwa kwa ukatili dunia nzima.

Dola hiyo ilipatikana Asia ya kati na ilikuwa ikijulikana kwa uvamizi wa dola nyingine na mauaji ya watu wengi zaidi.

Khutulun alizaliwa mwaka 1260 wakati huo familia yake ilikuwa ikitawala eneo lote la Asia ya Kati na sehemu za India na Mashariki ya Kati.

familia ya Kaidu ilikuwa na watoto 15 lakini Khutulun ndiye aliyekuwa binti pekee na mtoto wa mwisho wa familia hiyo , kwa sababu alionekana kuvutiwa na masuala ya kivita alipata mafunzo yote ya kijeshi kama ilivyokuwa kwa wanaume.

Inasemekana kuwa Khutulun alikuwa na uwezo wa ajabu tangu ikiwa mdogo alionekana mwenye nguvu na mpenzi wa michezo ya mieleka mchezo ambao ulikuwa maarufu kwenye dola yao ya mangolia.

Iaelezwa kuwa binti huyo aliweza kuwapiga wanaume wengi katika mchezo huo wa mieleka hivyo sifa yake ilijulikana kwa watu wengi zaidi

Upo wakati ambao aliweza kuwapiga wanaume kadhaa waliokuwa na nguvu katika himaya yao pia aliweza kupigana na wanaume wawili kwa wakati mmoja lakini bado aliibuka kinara.

Pia kwa mda mfupi Khutulun alijifunza jinsi ya kuendesha farasi , kutumia mapanga na matumizi ya upinde na mishale katika vita.

Alipofikisha umri wa miaka 20 alikuwa mrembo na shujaa katika uwanja wa vita historia inaeleza kuwa Khutulun alikuwa mpiganaji shujaa ambaye alikuwa na uwezo wa kuwaokoa mateka kwa haraka zaidi kama vile mwewe anavyonyakua kifaranga kutoka ardhini.

Kwa ushujaa aliokuwa nao Khutulun alimuwezesha baba yake kushinda vita nyingi sana alivyokuwa akipigana na wapinzani wake kwa lengo la kulinda na kutanua dola yake .

Kwa sababu malkia huyo alikuwa mrembo wanaume wengi walipeleka maombi yao ya kutaka kumposa alikuwa akiyakataa na kuyatupilia mbali maombi hayo.

Baaada ya kushawishiwa kwa mda mrefu na baba yake kuhusu suala la kuolewa hatimaye alikubali lakini kulikuwa na masharti kwa mtu ambaye alikuwa na nia ya kumuoa binti huyo.

Masharti hayo aliyaweka Khutulun mwenyewe na yalikuwa magumu sana kama vile Khutulun alitaka kuolewa na mtu ambaye alikuwa na ujuzi na nguvu zaidi kuliko yeye.

Hivyo alitoa sharti kwamba ataolewa na mtu ambaye atampiga katika mieleka, baada ya miaka kadhaa wanaume wengi walijaribu nguvu zao na bahati zao lakini walitoka kapa kwani walipigwa vibaya na malkia huyo hakuna mtu aliyefanikiwa.

Pia malkia Khutulun alitoa masharti kuwa kwa mtu ambaye angeshindwa kwenye tamasha hilo alitakiwa kulipa farasi 100 kama faini , ndani ya miaka michache Khutulun alikuwa anamiliki kundi kubwa la farasi 100000

Mpaka alipofikisha miaka 30 hakuna mwanaume ambaye alifanikiwa kumshinda katika mashindano aliyoyaweka kama mtihani kwa wale ambao walijitokeza wakiwa na nia ya kutaka kumuoa .

Baba yake alipatwa na wasiwasi baada ya yote hayo kutokea pia alimhofia binti yake kuwa asingeweza kuolewa maisha yake yote hivyo alimtafuta mpiganaji mahili na shujaa ambaye alitakiwa kushindana na Khutulun.

Mwanaume huyo alikuwa na uwezo mkubwa wa kupigana mieleka kwa dhana hiyo Khutulun alipandisha dau badala ya farasi 100 aliweka farasi 1000 endapo angemshinda mwanaume huyo cha kushangaza zaidi mwisho wa mchezo huo Khutulun alirudi kwa baba yake akiwa na farasi 1000 yaani yule bwana alipigwa haswa.

Baada ya tukio hilo Khutulun aliamua kuchagua mchumba
aliyempenda mwenyewe japo kuwa inaelezwa kuwa aliolewa mara mbili , mmoja wa wanaume hao alitokea katika jeshi la baba yake.

Khutulun alikuwa kipenzi cha baba yake kwani alipendwa sana kuliko kaka zake wote hivyo hata kiti cha ufalme Kaidu alitaka kumrithisha binti yake ambaye alikuwa mdogo na kwa sheria zao ilikuwa haikubaliki , alipata upinzani mkubwa kutoka kwa watoto wake wa kiume mpaka unakufa mwaka 1301 bado wanawe walikuwa na chuki naye.

Khutulun alikuwa mwanamke jasiri na mpambanaji wengi hudhani kuwa alikuwa na nguvu za mwili zisizo za kawaida kwani hakuna mtu ambaye aliweza kumshinda walipokuwa kwenye mashindano.

Khatuluni alikufa mwaka 1306 akiwa na miaka 46..
 
Nasubiri wa tandale na gongolamboto waje kutuongopea huyo khultun hakuwa muAsia bali alikuwa ni mtu mweuc, hawachelewi aise.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom