Mfahamu Angela Merkel

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Dk. Angela Dorothea Merkel
PicsArt_09-30-11.11.50.jpg
(amezaliwa tar. 17 Julai 1954, mjini Hamburg) ni mwanafizikia na mwanasiasa wa Kijerumani, na ni Chancellor (kansela/Waziri mkuu) wa Ujerumani tangu 22 Novemba 2005.

Familia na elimu
Alizaliwa 1954 mjini Hamburg katika familia ya Horst na Herlind Kasner. Babake alikuwa mchungaji wa Kanisa la Kiluteri, mama alikuwa mwalimu. Mwaka uleule familia ilihamia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani (ambayo ilikuwa Ujerumani ya Mashariki, kabla ya Ujerumani zote mbili kuungana na kuwa moja) ambapo aliishi huko hadi Muungano wa Ujerumani ulipofanyika mnamo mwaka wa 1990. Tangu 1957 familia iliishi mjini Templin katika kaskazini ya nchi ambako mchungaji Kasner alikuwa mkuu wa chuo cha theolojia. Mamake Angela alizuiliwa kufanya kazi ya ualimu kwa sababu serikali ya kikomunisti haikutaka mke wa mchungaji kuwa shuleni.

Alisoma shule ya sekondari kwake Templin alipofaulu hasa katika masomo ya Kirusi na hisabati. Aliingia pia katika Umoja wa Vijana wa Chama cha Kikomunisti FDJ. Alipomaliza shule kwenye mwaka 1973 wastani ya maksi zake ilikuwa A+.

1973 hadi 1978 alisoma fizikia kwenye chuo kikuu cha Leipzig. 1977 alifunga ndoa na mwanafunzi mwenzake Ulrich Merkel lakini ndoa hii ilitalikiwa 1982 Na kubaki hivyo pasipo mume.

Tangu 1978 aliajiriwa kwenye Taasisi Kuu kwa Kemia ya Kifizikia katika Berlin ya Mashariki. Hapa alimaliza tasnifu ya uzamifu mwaka 1986 iliyokubaliwa kwa heshima kuu "magna cum laude". Aliendelea na kazi kweye taasisi ya kemia ya kichanganuzi.

Mwaka 1984 alikutana kwenye Taasisi ya Taaluma ya Sayansi ya Berlin na mwanakemia Joachim Sauer akaolewa naye 1998. Angela hajazaa watoto bali alilea watoto wa Sauer akiendelea kutumia jina la Merkel.

Siasa
Wakati wa masomo na kazi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ujerumani Angela hakuingia katika chama cha kikomunisti wala chama kingine lakini alihudhuria katika kazi ya umoja wa vijana wa chama hiki.

Baada ya kuporomoka kwa ukomunisti na anguko la ukuta wa Berlin mwaka 1989-1990 Merkel alijiunga na chama kimoja kilichoundwa upya Demokratischer Aufbruch (DA - "uamsho wa kidemokrasia") akianza kazi kwenye ofisi ya chama hiki na baadaye kuwa afisa mawasiliano wa chama; baada ya kuingia kwa chama hiki katika serikali huru ya kwanza ya Ujerumani ya Mashariki alikuwa makamu wa afisa mawasiliano wa serikali.

1990 chama chake kiliamua kujiunganisha na chama cha magharibi CDU (Chama cha Kikristo cha Kidemokrasia cha Ujerumani) kilichokuwa chama cha chansela Helmut Kohl aliyeendelea kumwangalia na kumsadia katika siasa maana wanasiasa wa magharibi walitafuta wananchi wa mashariki ambao hawakuwa wanachama wa chama cha kikomunisti jinsi walivyokuwa karibu wote wenye madaraka kabla ya kuporomoka kwa utawala wake katika mwaka 1989. Mwisho wa 1990 Merkel aligombea kwenye uchaguzi wa bunge kwa niaba ya CDU katika jimbo la Mecklenburg-Pomerini Magharibi akachaguliwa. Baada ya uchaguzi chanselor Kohl alimpa wizara ndogo kwa wanawake na vijana. Mwaka uleule alichaguliwa kuwa makamu wa mwenyekiti wa chama cha CDU kama mwakilishi mmojawapo wa mashariki ya Ujerumani. 1994 alichaguliwa tena kuwa mbunga akapewa wizara ya Ujenzi na Mipango ya Miji.

1998 CDU ilishindwa katika uchaguzi wa bunge ikatoka serikalini. Sasa Merkel aliteuliwa kuwa katibu mkuu wa chama. Aliendelea kuwa mwenyekiti wa CDU katika mwaka 2000 lakini hakuongoza chama kwenye bunge. Uongozi huu alichukua baada ya chama kilishindwa tena katika kura ya 2002.

Baada ya uchaguzi wa 2006 vyama vilivyotawala yaani SPD na Green vilikosa kura za kutosha lakini CDU ilikuwa na wabunga wachache wengi kuliko SPD. Hapa Merkel alifaulu kupatana na viongozi wa SPD kuunda serikali ya umoja chini ya uogozi wake.

Hivyo Merkel amekuwa mwanamke wa kwanza kuwa Kansela kunako tar. 22 Novemba 2005 Hadi mwaka huu 2021 ambapo anaenda kuachia nafasi hiyo kama habari zilivyo letwa humu na kasomi TV.
katika serikali ya mseto wa vyama viwili vya kisiasa vya Kijerumani, yaani kati ya CDU/CSU na SPD.

Mwaka 2009 alitangaza ya kwamba alielekea kuaachana na SPD akitafuta ushirikiano na chama cha FDP (liberali). Uchaguzi wa bunge wa Septemba 2009 ulirudisha chama chake cha CDU tena kama chama kikubwa akaendelea kuunda serikali mpya pamoja na FDP. Katika kipindi hiki kulikuwa na maazimo mawili yaliyoendelea kuwa na umuhimu kwa baadaye

mwezi wa Mei 2010 Ujerumani ilikubali mpango wa nchi za Umoja wa Ulaya kusaidia uchumi wa Ugiriki kwa kuikopesha bilioni 80 za Euro baada ya nchi hii kushindwa kupipa madeni yake. Msaada huu kwa Ugriki na nchi kadhaa nyingine zilizotumia hela ya Euro ilipaswa kurudishwa ikaunda uchungu kati ya sehemu ya wananchi waliosikia hapa Ujerumani unalipa madeni ya mataifa mengine yasiyojali kanuni za kiuchumi.
Merkel aliwahi kurahisisha masharti ya kuendesha matanuri nyuklia lakini baada ya ajali ya kinyuklia ya Fukushima (Japani) serikali ya Merkel ilisimamisha matanuri nyuklia ya zamani mara moja na kuamua mpango wa kusimamisha matanuri nyuklia zote hadi mwaka 2022 na kubadilisha uzalishaji wa umeme wa Ujerumani kufanywa kwa nishati mbadala pekee.
Katika uchaguzi wa 2013 Merkel alifaulu kuboresha matokeo ya kura kwa ajili ya chama chake cha CDU lakini chama kidogo cha FDP kilishindwa kupata asilimia 5 za kura kikatoka bungeni. Merkel aliunda upya serikali ya mseto na SPD akaendelea kuongoza nchi. Mwaka 2015 aliamua kufungua mipaka ya Ujerumani kwa idadi kubwa ya wakimbizi hasa kutoka Syria, Irak na Afghanistan waliokuwa njiani wakitembea kutoka Uturuki kuelekea Ulaya ya Magharibi katika hali gumu. Alisifiwa na wengi kwa hatua hii lakini alipingwa pia vikali ndani ya nchi baada ya kufika kwa takriban milioni 1 wageni katika muda mfupi. Kwa jumla alibahatika ya kwamba hali ya kiuchumi ya Ujerumani ilikuwa vizuri lakini hakuchukua hatua za kuondoa hali gumu ya wananchi wasio na elimu ya kufaa kwa mahitaji ya uchumi na kudumu maisha yao kwa mapato madogo kulingana na mazingira ya Ujerumani.

Katika uchaguzi wa Oktoba 2017 vyama vya serikali ya mseto vilipotea kura nyingi hata kama CDU bado ilitoka kuwa chama kikibwa zaidi.
Hivyo Angela Dorothea Merkel anatarajia kuachia ngazi yake ya kama Chancellor mwaka huu.

Soma zaidi>>>> Wajerumani wapiga kura leo kuanza mchakato wa kumtafuta mrithi wa Angela Merkel

Chanzo: Angela Merkel - Wikipedia, kamusi elezo huru
 
Huyu Mwanamke hua hastaafu yeye maana wa kitambo.
Yupo mbioni kutoka
 
ndomana na Putin walikua wanaelewana enzi ujerumani mashariki ndiko putini alikua anafanya yake huko
 
Back
Top Bottom