Mfaham masai mtanzania anaye tikisa India kwa sasa na kujitwalia u star nchini humo.

Mangole Valles Michael

JF-Expert Member
May 30, 2021
333
671
Anaitwa kili -Paul

Kili-Paul ni kijana mwenye asili ya kimasai Kutoka mkoani Pwani - lugoba nchini Tanzania. Amezaliwa lugoba mkoani pwani ambapo alianza elimu yake ya msingi mpaka kufikia darasa la tatu na kuhamia dodoma ki masomo.
Alihitimu darasa la saba na kufauru kujiunga na elimu ya sekondari lakini kitokana na changamoto za kimaisha alishindwa kuendelea na elimu na kuamua kurudi nyumbani Pwani kuendelea na shughuli za kilimo na ufugaji.

Kili-Paul ameonekana kua na kipaji kikubwa cha kuimba nyimbo (nachi) za kihindi na kuzifanyia video clip ambazo amekua akimshirikisha Dada yake Neema Paul. Licha ya kuishia darasa la Saba kili-Paul anauwezo wa kuongea lugha ya kingereza, anasema alijifunza kwa juhudi zake mwenyewe kutoka mitandaoni lakini pia baba yake mzazi alimnoa katika kukizungumza.

Amekua akiimba nyimbo za wasanii wakubwa nchini India na kuzipost katika mitandao yake ya kijamii hasa TIKITOK ambazo zimekua na mapokeo makubwa na kuwavutia watu na wasanii wakubwa nchini india.

Kili-Paul na Neema Paul Wameanza kuzunguziwa na vyombo vikubwa vya habari nchini humo na kupambwa kwenye kurasa za magazeti kila kukuchapo. Hii imekua bahati nzuri sana kwao kwakua Kwakua wasanii wakubwa nchini humo wamekua wakimpgia video call wakimpongeza kwa kile anacho kifanya hata kupelekea baadhi yao kutaka kufanya nae kazi.

Haikuishia hivyo tu hata kwa wananchi wa kawaida pia wameonesha mahaba yao kwa kijana huyu ambapo wamekua wakifollow kwa kasi kila siku katika mitandao yake ya kijamii na mupokea comments za pongezi pamoja na makopa kopa kutoka kwa wadau nchini india.

Moja kati ya wasanii walio mpigia video call ni pamoja na Jubin Nautiyal, shah rukh khan n.k hata hivyo katika interview yake kill-Paul amethibitisha kufatwa dm na wasanii wakubwa na kumtaka wafanye kazi pamoja. Alipo hojiwa na SNS kuhusu mapokeo ya kazi yake nchini India amesema "hata mimi nashangazwa na jinsi wahindi wanavyo nionesha upendo ambao sikuutegemea kwakua nilikua nafanya video kwakua Mimi mi mapenzi wa nachi.

Mpaka sasa Kili-Paul kasha hojiwa na vyombo vikubwa vya habari kama BBC Swahili,BBC Africa, BBC india lakini pia amekua akipokea wageni kutoka uzunguni na barani Asia wanao mtembelea nyumbani kwao lugoba.

Dunia inahitaji watu creativity sana ili uweze kutusua

Fb @VAMI News
 
Back
Top Bottom