Mfadhili wa mbio za Arusha Marathon 2014 ajiondoa!

Mfadhili wa mbio za Arusha Marathon 2014 ajiondoa!

Mfikirishi

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Posts
11,426
Reaction score
13,767
Ukitaka maajabu njoo Tanzania yapo mengi tu!
Eti intelijensia inaonesha kuwa kuna hali tete ya usalama mkoani Arusha hivyo mbio za marathon zinazofanyika kila mwaka mjini Arusha hazitakuwepo mwaka huu!

Huu ni ujinga uliopitiliza! Yaani unaitangizia dunia kuwa Arusha si sehemu salama ya kumtembelea kwa sasa! Are you serious!
Alafu Kenya wafanye nini sasa kama Tanzania imeshatangaza hali ya hatari kwa usalama wa watu!

Hivi maaskari wanakazi gani kama si kulinda maisha ya raia na mali zao???

What a Shame!?!

===========
UPDATE:

Imebainika kuwa Tatizo ni kwamba mfadhili wa hayo mashindano amewambia kwamba hana fedha kwa hiyo hawezi kudhanini mwaka huu na kwamba hakuna aliyewasiliana na polisi kuhusu kuahirishwa kwake kwa hiyo hayo maneno ya kwamba ni sababu za Kiusalama si sahihi.
 
tanzania tunaua utalii wetu wenyewe kwa kushirikiana na wakenya wenye matatizo kwao ... halafu tunasema tuungane east africa ... U.J.I.N.G.A mtupu
 
Tangu Arusha imepata mbunge kutoka kile chama ambacho kinasema kina Mungu lakini cha kushangaza Mungu hakuwai kuwa ruhusu kwenda ikulu,Arusha imekuwa si sehemu salama.
Poleni wana Arusha.
 
Nadhani wanatengeneza mazingira ya kupiga marufuku mikusanyiko(mikutano ya kusiasa) hasa ukizingatia kwa Mkoa wa Arusha ccm imeparanganyika kila kona

Sasa wanataka kuyaleta yale ya Mtwara, Naaamini kwa kuanza na hili la mbio za Marathon wamepata pa kuanzia. Itakapofika wakati wa kupiga marufuku mikusanyiko, watadai mbona hata marathon tulipiga marufuku Manyan'gau yaliyoishiwa ushawishi na hoja kwa Wananchi hawa

cc Mungi Crashwise Filipo Jiandaeni kwa drama hizi za hawa punguani

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:
Polisi wanasema kuna mikutano mingi mikubwa inafanyiwa kwa sasa Arusha ya Kimataifa na ya Kitaifa na iko ndani na mingine hufanyika hadi usiku.

Kwa hiyo hiyo marathon tena barabarani ambayo inaongozwa na polisi mbele na nyuma hawawezi kuogopa.

Hilo hapo juu kuwa Mfadhili Kujitoa ndio tatizo kubwa inawezekana mfadhili au waandaaji wametumia issue ya usalama kama kisingizio bila kujua madhara yake kiuchumi. Hata polisi hawajawauliza.
 
Kuna habari inayosema kwamba mji wa Arusha sio shwari ndio maana mfadhili wa mbio za marathon amejiondoa, ukweli ni kwamba mji wa Arusha upo shwari kabisa na sababu za kujiondoa kwa mfadhili wa mbio za marathoni ni kwamba mfadhili huyo amekosa pesa za kuwezesha kudhamini mbio za marathoni na sio kwa sababu za mji huo kutokuwa salama. hizo taarifa ni za kututia hofu tu wananchi na wakazi wa mji wa Arusha.
 
Uongo mtupu, arusha ni shwari kabisa mfadhili huyo kwa sasa hana fedha za kudhamini mbio za marathon usiwatie hofu watanzania bhana
 
ukitaka maajabu njoo tanzania yapo mengi tu!
Eti intelijensia inaonesha kuwa kuna hali tete ya usalama mkoani arusha hivyo mbio za marathon zinazofanyika kila mwaka mjini arusha hazitakuwepo mwaka huu!

Huu ni ujinga uliopitiliza! Yaani unaitangizia dunia kuwa arusha si sehemu salama ya kumtembelea kwa sasa! Are you serious!
Alafu kenya wafanye nini sasa kama tanzania imeshatangaza hali ya hatari kwa usalama wa watu!

Hivi maaskari wanakazi gani kama si kulinda maisha ya raia na mali zao???

What a shame!?!

===========
update:

imebainika kuwa tatizo ni kwamba mfadhili wa hayo mashindano amewambia kwamba hana fedha kwa hiyo hawezi kudhanini mwaka huu na kwamba hakuna aliyewasiliana na polisi kuhusu kuahirishwa kwake kwa hiyo hayo maneno ya kwamba ni sababu za kiusalama si sahihi.

huyo mfadhili hana mpunga wa kutosha wajameni na sio sabababu za kiusalama
 
Tangu Arusha imepata mbunge kutoka kile chama ambacho kinasema kina Mungu lakini cha kushangaza Mungu hakuwai kuwa ruhusu kwenda ikulu,Arusha imekuwa si sehemu salama.
Poleni wana Arusha.

Nani anasababisha machafuko??
 
Tangu Arusha imepata mbunge kutoka kile chama ambacho kinasema kina Mungu lakini cha kushangaza Mungu hakuwai kuwa ruhusu kwenda ikulu,Arusha imekuwa si sehemu salama.
Poleni wana Arusha.
kwa hiyo nini kifanyike
 
Back
Top Bottom