Meya wa Kigoma Manispaa akataa gari la milioni 150

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
620
1,543
Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Hussein J Ruhava amekataa kununuliwa gari ya tshs 150m na kuelekeza fedha hizo kwenda kwenye matumizi ya maendeleo na haswa miundombinu ya mji.

Wakati chama chenu cha ACT Wazalendo kinaomba kura nchi nzima za urais, ubunge na udiwani, pamoja na mambo mengine kiliahidi kupunguza matumizi ya anasa ya serikali ili fedha hizo zielekezwe kwenye maendeleo, Manispaa ya Kigoma inaongozwa na Act na yale tuliyo yaahidi tutayatekeleza kwa vitendo katika manispaa hii.

Watanzania tunaomba mtuunge mkono.
 
tuko pamoja...achana na Meya anayelialia kwenye media...oohoo Makonda ananiingilia!!! atakuingilia kweli unacheza na hii awamu ya 5!!
Viongozi wako busy na kutatua kero za wananchi.
 
Mwenzie wa Kinondoni kakerwa na Kitendo cha Makonda kuwaambia wananchi kuwa kuna dola kadhaa toka kwa Wajerumani sijui walikusudia nini
 
Mwenzie wa Kinondoni kakerwa na Kitendo cha Makonda kuwaambia wananchi kuwa kuna dola kadhaa toka kwa Wajerumani sijui walikusudia nini
Mioyo in awauma hamlali hamli juu ya ile halmashauri lkn ndo basi tena, mwatamani hata afe Leo huyo meya, lkn ndo basi tena
 
Ni hatua. Baada ya kukataa kununuliwa gari la bei hiyo, kanunuliwa la bei gani? na pia zilizobaki ni kiasi gani na zimepelekwa kwenye shughuli gani hasa za maendeleo?
 
Kidogo naweza amini kwamba nyie mnaweza kuwa wapinzani wakweli lakini sio wale chaga dema wamesababisha mpaka chama changu CUF kipoteze mvuto kwenye ulimwengu wa siasa
 
Hivi ni Meya gani ailiesema hahiitaji pesa Magufuli, eti halmashauri yake inapesa za kutosha. !
 
Kukataa gari tu haitoshi bali hakikisheni mnadhibiti matumizi mabaya ya rasilimali maeneo yote ili maisha ya wanakigoma yawe bora
 
kununua gari ya Halmashauri siyo anasa. Kuna mtu ameniambia Kigoma Manispaa haina gari zake. Gari zote zilizopo ni DFP ni za miradi hizo na ni makosa Meya kutumia DFP. Tena WB wakiona bendera ya Meya kwenye DFP lazima mtumbuliwe majipu.

Nadhauri waangalie kama wanaweza kupata gari ya bei ya chini ikapata usajili SM hiyo ndiyo halali Meya kutembelea.
 
Hivi ni Meya gani ailiesema hahiitaji pesa Magufuli, eti halmashauri yake inapesa za kutosha. !
Mkuu nafikiri huyo Meya alielekeza fedha za Magufuli lilipie lile hekalu la Dr..si unajua mambo ya siasa huwezi kuyajua yote..
 
tuko pamoja...achana na Meya anayelialia kwenye media...oohoo Makonda ananiingilia!!! atakuingilia kweli unacheza na hii awamu ya 5!!
Viongozi wako busy na kutatua kero za wananchi.
Ni viongozi wachache sana wa Ukawa ambao wanajielewa, wengi wao ni vichwa maji tu, Huyu jamaa hastahili hata kuwa mjumbe wa nyumba kumi.
 
Back
Top Bottom