Kigoma: TAKUKURU yabaini Upotevu wa Tsh. Milioni 800 za Mikopo ya 10%

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,616
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Kigoma imebaini upotevu wa fedha Tsh. milioni 800 za mikopo ya 10% kutokana na vikundi vilivyoomba mikopo hiyo kutorejesha kabisa.

Akiongea na Ayo tv Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoani humo John Mgala amesema fedha hizo ni za Halmashauri za Kasulu, Kibondo, Kakonko, Buhigwe na Kigoma Ujiji na kuzitaka Halmashauri hizo kufungua kesi za Wadaiwa sugu.

Katika uchunguzi uliofanywa katika kipindi cha January hadi March mwaka huu Taasisi hiyo imebaini kuwa vikundi hivyo havifanyi shughuli ambazo wamekuwa wakiombea mikopo hiyo bali hugawana baada ya kuzipata pesa na hivyo kuwa vigumu katika marejeshi.

Watumishi watatu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Kigoma Ujiji wanatajwa kuhusika katika mchakato wa upotevu wa fedha hizo ambao nao wanaendelea kufanyiwa uchunguzi.

Chanzo: Millard Ayo
 
Hii Manispaa ya Kigoma/Ujiji hapana kwakweli uhuni ni mwingi mno uwajibikaji wao ni mdogo sana nadhani wazawa wengi kuwa ofisini ndio shida kubwa
 
Mh Waziri mkuu,shikmooo Kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Baada ya salamu naomba nikutonye new habari yakuwa Milioni 800/= zilizotokana na 10% ya mikopo ya vijana na akina mama zimepigwa na vijana wa umoja wa vijana wa ccm mkoani kigoma.

Hii taarifa mkuu wangu ni Kwa mujibu wa kamanda wa Takukuru mkoa wa kigoma je umeelewa?
 
PM 0777 000 003 mpigie mkuu
 
Sifi leo acha chokochoko huo ni utaratib wa kawaida tu kula fweza za inji hii!!!
 
Back
Top Bottom