Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 302
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa, yupo jijini Mwanza kuongeza nguvu kwa madiwani wa chama chake kumpata meya wa jiji.
Katibu wa Chadema Mkoa Mwanza, Willson Mshumbusi na Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje, walisema kwa nyakati tofauti kuwa, Dk Slaa alikuwa akiendesha vikao kuwanoa madiwani wa chama chake, ikiwamo kutoa maelekezo jinsi ya uendeshaji halmashauri na ufuatiliaji maendeleo.
"Katibu mkuu kwa siku ya leo alikuwa na kikao na madiwani wa chama, baadaye aliendesha kikao cha wajumbe wa Kamati Tendaji ya Chama Mkoa na baada ya kikao hicho, jioni alikuwa na kikao cha madiwani wote na wajumbe wa kamati ya utendaji," alisema Mshumbusi.
Mshumbusi alisema kwa mujibu wa utaratibu wa chama, Dk Slaa atashuhudia uchaguzi wa chama kumpata mgombea wa umeya, kisha atashughulikia na masuala mengine ya chama na kurejea Makao Makuu Dar es Salaam.
"Alikuwa akitoa maelekezo ya sifa za kiongozi na namna ambavyo meya anatakiwa kuwa, lakini pia amebainisha vigezo vya kupatikana kwa meya wa jiji, baada ya kukamilisha hayo kesho (leo) atakuwa na kikao cha wagombea wa nafasi ya umeya, kuhojiwa kisha kupigiwa kura," alisema.