Elections 2010 Meya wa Jiji la Mwanza kutoka Chadema?

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa, yupo jijini Mwanza kuongeza nguvu kwa madiwani wa chama chake kumpata meya wa jiji.

Katibu wa Chadema Mkoa Mwanza, Willson Mshumbusi na Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje, walisema kwa nyakati tofauti kuwa, Dk Slaa alikuwa akiendesha vikao kuwanoa madiwani wa chama chake, ikiwamo kutoa maelekezo jinsi ya uendeshaji halmashauri na ufuatiliaji maendeleo.

"Katibu mkuu kwa siku ya leo alikuwa na kikao na madiwani wa chama, baadaye aliendesha kikao cha wajumbe wa Kamati Tendaji ya Chama Mkoa na baada ya kikao hicho, jioni alikuwa na kikao cha madiwani wote na wajumbe wa kamati ya utendaji," alisema Mshumbusi.

Mshumbusi alisema kwa mujibu wa utaratibu wa chama, Dk Slaa atashuhudia uchaguzi wa chama kumpata mgombea wa umeya, kisha atashughulikia na masuala mengine ya chama na kurejea Makao Makuu Dar es Salaam.

"Alikuwa akitoa maelekezo ya sifa za kiongozi na namna ambavyo meya anatakiwa kuwa, lakini pia amebainisha vigezo vya kupatikana kwa meya wa jiji, baada ya kukamilisha hayo kesho (leo) atakuwa na kikao cha wagombea wa nafasi ya umeya, kuhojiwa kisha kupigiwa kura," alisema.
 
Jamani kuna mwenye taarifa ya matokeo ya kata za Mikuyuni na Nyegezi huko Mwanza atujuvye.
 
Nilisikia zimechukuliwa na CUF na CCM

Kwani ukiacha kwa kata hizo mbili uwiano wa madiwani ukoje?

Ni kweli CDM haikupata kiti kati ya viwili vilivyobaki lakini tayari Chadema kabla ya uchaguzi huo mdogo, ilikuwa imeshazoa viti 11 kati ya 21 vilivyomo katika majimbo ya Nyamagana na Ilemela, ambavyo vinaunda Halimashauri ya Jiji la Mwanza.

Kwa maana hiyo viti 11 ukiongeza na za wabunge wawili wa Nyamagana na Ilemela ambao wanahesabika kama madiwani CDM itakuwa na madiwani 13, hata CCM waunganishe na CUF hawawezi kufikia viti vya CDM.
 
Wajipange vizuri na kuiongoza hiyo halmashauri vizuri!ili iwe mfano mzuri ifikapo 2015!!
 
I see a great prospects for Mwanza, they seem to understand their rights and the meaning of democracy; way to go Mwanza....and hpefully many more will follow their model...a democratic society upholds rule of law-and respects human rights
 
Hongera watu wa mikoa ya Ziwa mna akili sana ninyi hamdanagnyiki? You gonna reap the fruits soon na huyo jamaa mkurugenzi wa Jiji kibaraka wa CCM mtaitini sana
 
hiki chama kinaitwa Chama cha demokrasia na maendeleo kifupi chake ni Chadema na si >CDM na inapendeza ikibakia chadema.
 
Back
Top Bottom